Tumebakisha siku 4 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.a.w): Niulize chochote kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) Nitakujibu

Tumebakisha siku 4 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.a.w): Niulize chochote kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) Nitakujibu

Swahili Muslims kuna chanzo chochote cha kihistoria kuhusu kuwepo kwa Muhammad rasul Allah, na kwamba aliishi na kufanya kama inavyoelezwa kwenye Quran, Sunnah na Sira? Angalau kilichoandikwa ndani ya miaka hata 50 baada ya uwepo wake, au kilichoandikwa na watu walioishi zama zake?

Nimejaribu kutafuta naona vingi vimeandikwa miaka mingi sana baadaye, angalau miaka 200 baadaye.
Ukinisaidia hii nitashukuru!
Kitabu cha kwanza ni QUR'AN yenyewe, Wakati Mtume Muhammad alikufa, Quran ilikuwa imeandikwa kikamilifu. Haikuwa katika fomu ya kitabu, hata hivyo. Ilirekodiwa kwenye ngozi na vifaa tofauti tofauti, na nyingine ilikuwa imehifadhiwa kichwani na Masahaba wa Mtume.

Ali Ibn Abi Talib huyu ni swahaba wa Mtume na aliandika vitabu vingi ikiwemo Nahjul Balagha, Al-Saheefah Al-Alawiyah , Nahj al-hikma wa ul-balagha na vingine vingi.
 
Cha ajabu wachangiaji watakuwa wa upande mwingine na kukejeli kwa kashfa na matusi

Ni ajabu moja nimeiona JF uzi ukiletwa wa wakristo wachangiaji wengi wanakuwa ni wakristo kwa mfano jana uzi kuhusu RC na ndoa
Waislamu walipita kushoto kwani hauwahusu

Ila sasa uzi wa kiislam ndio utajua wakristo wana chuki mbaya tena ya wazi
Kuuliza maswali ni sawa ila kama hayakuhusu unapita kimya sio mpaka uonyeshe chuki kwa wengine
Unajuaje Kama wanaouliza wote ni wakristo au ni kujistukia mkuu wakt unajua kabisa majina yenyewe hayaeleweki haya.
 
baada ya jibu hili nimesitisha nilichotaka kuuliza, nimepata ukakasi na ujuzi na uadilifu wa mtoa mada.....kuna kitu kinaniambia tofauti, the guy is here just to make fun of islam!!!
Hiyo ni hoja mkuu imeukusanya na mawazo yangu ndani yake. Kama una hoja weka hapa tuwe na bainisho la mawzo yako ndani ya maandiko kama sehem ya udadavuaji wako.. Simpo
 
Kuna ukweli wowote kuhusu Mtume kumuoa mke wa mwanaye, lingine kwanini yeye alioa wake zaidi ya 7 ila kwa Waislam wengine mwisho wanne kwann yeye wawe wengi
Alioa wake wengi baada ya kufariki kwa mke wake wa kwanza Bi Khadija, mtume alioa kwa sababu ya kijamii au kisiasa; vile alitaka kuwaheshimu wanawake wacha Mungu, au alitaka uaminifu wa makabila fulani ili Uislam uenee kati yao. Wake wote ambao Muhammad alioa hawakuwa bikra, wala hawakuwa vijana au wazuri. Sisi waisilamu wengi MUNGU ametutaka kuoa mwisho wa 4 nasio zaidi, bali nafasi hiyo alipewa mtume pekee kutokana na sababu nilizokupatia
 
Je ni kweli mtume alizaliwa akiwa ametahiriwa?

Je ni kweli mtume hakuwa na kimvuli hata alipotembea juwani?

Je Uislami unaamini Masia ndio atahukumu wazima na wafu siku ya mwisho.?
Ahsante ndugu.
Ndio ni ukweli Muhammad s.a.w alizaliwa bila ya govi (tayari alikuwa ameshatahiriwa) na alama au muhuri wa unabii alikuwa nao mabegani.

Ndio, ni kweli kivuli chake hakikuwahi kukanyaga ardhini, Inaaminika kwamba kila nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu alikuwa na alama yake kwenye sehemu fulani ya mwili wake. Muhammad hakuwa na kivuli ardhini, ilitafsiriwa kama ishara ya "nuru" yake. Pia Muhammad alikuwa akisikia sauti za watu ambao walikuwa wakiteswa katika makaburi yao.

Masia ukimaanisha nini ?
 
Jitahidi kupitia marejeo yako(vitabu).
Buraq alitumika kutoka Macca hadi Jerusalem (Israa). Kutoka Jerusalem hadi mbinguni ilitumika ngazi(mi-iraaj).
Ndio sababu ya kuitwa safari hiyo "israa na mi'iraaj)
Ni sahihi kabisa ndugu yangu, sema naandika kwa haraka sana. Shukran ulamaa
 
Cha ajabu wachangiaji watakuwa wa upande mwingine na kukejeli kwa kashfa na matusi

Ni ajabu moja nimeiona JF uzi ukiletwa wa wakristo wachangiaji wengi wanakuwa ni wakristo kwa mfano jana uzi kuhusu RC na ndoa
Waislamu walipita kushoto kwani hauwahusu

Ila sasa uzi wa kiislam ndio utajua wakristo wana chuki mbaya tena ya wazi
Kuuliza maswali ni sawa ila kama hayakuhusu unapita kimya sio mpaka uonyeshe chuki kwa wengine
Manaswara hawatakua radhi nanyi hadi mfuate mila zao

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Kitabu cha kwanza ni QUR'AN yenyewe, Wakati Mtume Muhammad alikufa, Quran ilikuwa imeandikwa kikamilifu. Haikuwa katika fomu ya kitabu, hata hivyo. Ilirekodiwa kwenye ngozi na vifaa tofauti tofauti, na nyingine ilikuwa imehifadhiwa kichwani na Masahaba wa Mtume.

Ali Ibn Abi Talib huyu ni swahaba wa Mtume na aliandika vitabu vingi ikiwemo Nahjul Balagha, Al-Saheefah Al-Alawiyah , Nahj al-hikma wa ul-balagha na vingine vingi.
Unaweza kuweka chanzo cha kihistoria kuwa Quran ilikuwa compiled Karne ya 7? Data zote nilizoziona ni kuwa ilikuwa compiled angalau miaka 200 baadaye. Kitu kinachomaanisha hakukuwa na shuhuda hata mmoja.

Huyu swahaba aliandika vitabu vyake karne ya ngapi?
 
Alikuwa na umri gani?

Hadija pia alikuwa na umri gani?

Je ni kweli alishapita na mke ya "jamaa flani" alipoenda kumtembelea na akakuta jamaa hayupo?
Aisha alikua na miaka 6 lakini aliamza kulala nae kama mke akiwa na miaka 9.
Hadija alikua na miaka 40 pindi anaolewa na mtume ambaye alikua na miaka 25 .
Kuhusu kupita na mke wa jamaa alipomtembelea sijui ingawa alimuoa mke wa zayd lakini baada ya kuachwa na zayd
 
Ahsante ndugu, Kuolewa kwake na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ilikuwa kwa Amri ya Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) baada ya kufa mke wakwanza wa mtume Bi Khadija Mama wa Waumini Khadiyjah (Radhiya Allaahu ‘anha). Aisha alikuwa msichana aliyekomaa na alikuwa anakua kiakili na kimwili kwa uharaka wa ajabu walionao watu wachache sana.

Lakini pia ndoa hii ilikamilika Aisha alipokuwa na umri wa 17 au 19 wakati huo. Kama waandishi wote wa wasifu wa Mtume wanavyokubali kwamba alikamilisha ndoa yake na Hazrat Aisha katika mwaka wa 2 Hijri inaweza kusemwa kabisa kuwa alikuwa na umri wa miaka 19 wakati huo na sio tisa kama inavyodaiwa katika hadithi zilizotajwa.
Miaka 19 ndipo mtume alifariki akiwa na miaka 63
 
Kwasababu aliyo yaleta Muhammad s.a.w ni mfano wa yale yale yaliyoletwa na mitume wengine waliokuwa kabla yake.
Kijografia na kiteolojia kwann kunautofauti?
Namaanisha mitume yoote (mayahudi) iliyotangulia mafundisho yao hawakutofautiana, kwann yeye amekuja tofauti pamoja na kukubali au kuyabeba baadhi ya mafundisho ya kiyahudi?
 
Back
Top Bottom