Tumebakisha siku 4 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.a.w): Niulize chochote kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) Nitakujibu

Tumebakisha siku 4 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.a.w): Niulize chochote kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) Nitakujibu

sio siku ya kiama ila ni kwa wale watakaofanikiwa kuingia peponi.siku ya kiama ni hukumu kwa watenda mema na maovu sio siku ya kupeana mabikira
kwahiyo shehe, mwanaume akitenda mema hapa dunianiakiwa amekufa anasubirki kiama ndio analetewa watoto mabikra 70? na je baada ya kuwavunja bikra hao wanawake wanaenda wapi?
 
Cha ajabu wachangiaji watakuwa wa upande mwingine na kukejeli kwa kashfa na matusi

Ni ajabu moja nimeiona JF uzi ukiletwa wa wakristo wachangiaji wengi wanakuwa ni wakristo kwa mfano jana uzi kuhusu RC na ndoa
Waislamu walipita kushoto kwani hauwahusu

Ila sasa uzi wa kiislam ndio utajua wakristo wana chuki mbaya tena ya wazi
Kuuliza maswali ni sawa ila kama hayakuhusu unapita kimya sio mpaka uonyeshe chuki kwa wengine
Udini utakupeleka wapi
 
Kwa nini alioa binti mdogo khadja?
Je, hii ni sawa?
Ahsante ndugu,
Khadija binti Khuwaylid alikuwa mke wa kwanza na mfuasi wa kwanza wa nabii wa Kiislam Muhammad. Khadija alikuwa binti wa Khuwaylid ibn Asad, kiongozi wa kabila la Quraishi huko Makka, na mwanamke mfanyabiashara aliyefanikiwa kwa haki yake mwenyewe.

Khadija mara nyingi hujulikana na Waislamu kama "Mama wa Waumini". Yeye ni mmoja wa watu muhimu zaidi wa kike katika Uislamu.] Muhammad s.a.w alipofikisha miaka 25 ndio alimuoa Bi Khadija naye kwa mke mmoja kwa miaka 25, wakati huo Bi Khadija alikuwa na umri wa miaka 40. Na walizaa watoto sita akiwemo Qasim ibn Muhammad, Abdullah ibn Muhammad, Umm Kulthum, Ruqayyah, Zaynab, na Faṭmah.
 
وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ

Na hawatoridhika nawe Mayahudi wala Manaswara mpaka ufuate mila zao. [Al-Baqarah (2: 120)]

Cha ajabu, kwa upande wa waisilamu wa jamiiforum n.k mada muhimu kama hizi huwezi waona ila wachache sana, hata kuchangia tuu hamna. Mleta mada anajikuta kaambulia wachangiaji wachache sana kama 2onavyo manaswara wameingia kuuliza maswali, na wengine wanapitisha kejeli,,,,. Lakinii nenda jukwaa la siasa, mapenzi, sports, jokes, international furum n.k utawakuta waislamu kama co wengi bac ni wachache wao wakichangia.
Umeongea nini
 
Yeye (Muhammad Ibn Abdullah) alizaliwa katika nyumba ya ami yake, Abu Talib, katika “mtaa wa Bani Hashim” huko Makka, tarehe 12 Rabil-awal ya ule Mwaka wa Tembo, tarehe ambayo inaoana na tarehe 8 Juni 570.

Mama yake na mtume Muhammad (s.a.w), Bi Amina, alituma habari za uzazi huu wa kheri kwa babu yake na Muhammad, Mzee Abdul Muttalib, ambaye alikuja, akamchukuwa mikononi mwake, na akampa jina hili la Muhammad.” Lenye maana ya MSIFIWA.

Nawakaribisha kuuliza maswali kuhusu mtume wetu huyu MUHAMMAD "amani na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake".

View attachment 1975182
Samahani Sheikh! Aliye anzisha vita vya Jihads ni Mtume mwenyewe, au ni Wafuasi wake waliomfuata baada ya kifo chake?
 
Kwenye translation ya mwanazuoni wa kiislamu maarufu kama Ibn Ishaq, alimuelezea buraq kama mnyama ambaye ni mnyama nusu farasi nusu mtu akiwa na mabawa pembeni

image ambayo unaweza ukaijenga kwa sifa hizo alizoelezea huyo mwanazuoni unaweza ukapata picha hii

817896-29673797262_7baa39fbf7_z.jpg



Mimi nilikuwa nataka kuuliza tu, habari hiyo ni ya kweli au yakufikirika? Vigezo gani vilivyotumika kuthibitisha uhalisia wa hilo tukio?
HAYA NI MAMBO YA KIIMANI ZAIDI. KWANI NI VIGEZO GANI VILIVYOTUMIKA KUTHIBITISHA MIMBA YA YESU, KWAMBA ILIPATIKANA BILA BABA? MIMI NA WW TUNAAMINI ILIPATIKANA KWA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU, LKN WAYAHUDI MPK LEO WANAAMINI KWMB YESU NI MTOTO WA ZINAA
 
Je, Mtume alisema siku ya kiyama tutapewa mabikira 70?
Je, kama ndivyo tutatumia mkongo au alkasusu?
Khur-lain
Katika imani ya dini ya Kiisilamu, hawa ni wanawake ambao watafuatana na waumini waaminifu wa Kiislam katika Pepo. Wasomi wa Kiislamu wanatofautiana kuhusu ikiwa wanarejelea wanawake waumini wa ulimwengu huu au uumbaji wao ni tofauti, lakini kwa hakika wanawake wa peponi wapo.
 
Ni kweli malaika Gabriel (mwenyewe alimpachika Jibril) alimshushia mkong'oto wa nguvu pangoni alipokuwa ana muelekeza kuandika kurani kwasababu hajui kusoma na kuandika?
Yah ni kweli, lakini ukali w maneno hay "shushiwa mkong'oto" unawez kuleta taharuki hasaa. Mtume aliambiwa kusoma ilihali hajui. Na kuna nguvu kias ilitumika kulazimisha hilo
 
Mtume alikataliwa na karibia watu wote hata baba yake mdogo alipinga. Wengi tu kun hadithi zinasema alipigwa wakamtoa meno.
Kushushia maneno y mungu "wahayi" kuliendana sana na matukio. Hakukuw n sehem moja ya kupokea maneno ya mungu
Ahsante ndugu, mapigano yote ya mtume ilikuwa ni kujihami kutokana na vita alizokuwa akivamiwa, mtume hakuanzisha vita bali alikupovamiwa ndio alikuwa kijihamu. Mtume Muhammad (s.a.w) alipoteza meno manne kwenye Vita vya Uhud, baada ya kupigwa na shoka. Meno mawili yalidhaniwa yamepotea. Watu walimpinga kwasababu walikuwa wakiabudu masanamu na moto na wengine wakiabudu jua na mwezi, sasa yeye alikuja kutangaza MUNGU ni mmoja ndio ugomvi ukaanza hapo, ni sawa na leo mtu aje atangaze kwamba hakuna YESU, nadhani anaweza akapigwa.
 
Ni kweli hakutahiriwa alikuwa govi? Na kama ni kweli kwa nini aliiga vyote akashindwa kuiga kutahiriwa? Au alikuwa anaogopa kitu chenye ncha kali?
haya mengine ni maswali ya dhihaka ili tu kuonekana unachekesha mbele ya jamii ambayo kiuhalisia ni jamii ya kinadharia maana huioni.
Kama huna jema la kuuliza ama kusema, kukaa kimya napo pia ni uungwana. Nina yakini imani yako hata kama si ya kiislamu haifundishi dhihaka. Kuwa makini na maswala ya dini mkuu, unalolichukulia wewe kwa wepesi kwa wenye imani yao linamaanisha kila kitu.
 
Hapana si kweli,
Dini ya Kiyahudi, ya zamani kabisa katika dini kuu za kuabudu Mungu mmoja zilizoibuka Mashariki ya Kati, ndiye wa kwanza kumshutumu nguruwe kama mnyama mchafu katika Kitabu cha Mwanzo na Mambo ya Walawi.

Miaka 1,500 baadaye ni Mtume Muhammad ambaye pia anamwonyesha nguruwe kama mnyama mchafu. Bwana na Mwenyezi Mungu wamekataza nguruwe kwa mamilioni ya Wayahudi na mamia ya mamilioni ya Waislamu.
 
Back
Top Bottom