Lengo ni kuongeza mapenzi yetu kwa Mtume, Mtume (saw) alisema, "Hakuna hata mmoja wenu atakayekuwa na imani mpaka anipende mimi kuliko baba yake, watoto wake na wanadamu wote. .
Kulingana na mila ya Kiislamu, wanyama, miti na hata vitu visivyo na uhai kama milima vilionyesha upendo kwa Nabii Muhammad (saw), na pia aliwaonyesha upendo pia. Kwa hivyo, kuongeza upendo wetu kwake na kuionyesha ni sawa na maumbile yote na hutuunganisha na nishati ya kiroho ya ulimwengu.
40.HUKMU YA MAWLID
Written by
Said Al Habsy
KHALFAN SALIM from
Kenya
--------------------------------------
Swali:
asalam alaikum warrahamatu Allah wabarakatu je maulid (mazazi ya mtume) yako katika dini yetu ya kiisilamu.
JAWABU:
Walaykum Salaam warahmatullah wabarakatuh.
Maulidi haikuwepo katika zama za Mtume s.a.w. wala masahaba wala wafuasi
wao. Ni kitu kimeanzishwa baada ya muda kupita kama uanzishaji wa vingine
kama mashindano ya Quran, kuweka Maquba msikitini, n.k.
Na kuhusu nani muanzishaji wake kuna khilafu baina ya wanachuoni, na kumjua au kutomjua si muhimu kwani kinachotazamwa ni kuwafikiana na sheria.
Hukmu ya Maulid itategemea malengo na namna ya kuyafanya hayo maulid yenyewe. Ikifanywa vizuri itakuwa nzuri na kinyume chake ndio ubaya wake.
Maulid zinazofanywa katika nchi zetu za Kiafrika na Asia, nyingi zinakuwa na mambo yasiyokubalika kisheria mengi na kuleta madhara hasa katika
kufanyika kwake usiku, kutoka kwa mabinti wa kiislam wari, kuenea kwa
zina, n.k.
Hivyo yakirekebishwa hayo na yakafanyika maulid kwa namna bora kama
kukutana msikitini kukatolewa historia ya Mtume au mawaidha na anasheed za
bila kuruka na kurukaruka, bila madufu, na bila ya kuchanganyika wanaume
na wanawake hakuna dhambi katika hilo bali watapata thawabu.
Na kwa hivyo ametoa fat wa Sheikh wetu Shaban Albattashi - Allah mtukufu amuhifadhi- kuhusu uharam wa maulid hizo zenye hayo makosa tuloeleza.
Na ametazama Sheikh wetu Ahmed Alkhalili - Allah amuhifadhi - uzuri wa yapatikanayo katika maulid zenye nidhamu, na taratibu nzuri akatoa fat wa ya kujuzu kwake, pamoja na kuelekeza kuwa iwe ni msimu wa kujipima kimaendeleo, na njia ya kuelekea katika mapenzi ya vitendo na kumuiga yeye Mtume s.a.w.
Amesema Allah mtukufu:
Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu. 3:31
Pia Amesema Allah mtukufu:
"Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana." 33:61
Wallahu aalamu.
Abu Muslim Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com