Mkutano umeisha muda mfupi uliopita baada ya mgombea wetu kueleza sera zake.
Leo ameyameza maneno yake ya jana na hivyo ametueleza sera zake ni nzuri ila kuna sehemu anarudiarudia sana.
Kilichonisikitisha ni kuwa bado jambo lile la jana limejitokeza na leo kwa kuchangishwa michango ila leo aliyesema tutoe simu na kuchanga ni John Mrema, na sijui ni nani aliwaambia tunaokuja kwenye mkutano tuna namba za Voda tu.
Hatujachanga, kwa sauti ya unyonge sana tumesingizia tena network.
Watu ni wachache sana ila tukutane kesho Segerea.