johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Rungu la Mbowe linakusubiri hapo Ufipa!Kwa tuliokuwa tukijadili afya ya Rais basi mimi ni mmoja wao ninaamini na itakuwa hivyo kuwa Rais hakuwa katika afya yake iliyozoeleka. Na hata ukimuona leo ni bado hakuwa vizuri.
Nimeona video akisalimiana na katibu mkuu kiongozi ndugu Kijazi kwakweli inaonekana kabisa ndugu Kijazi kama ananena mambo fulani hivi. Kwanza inaonekana hawakuwa pamoja kwa muda fulani.
Any way tushukuriwe sisi ambao tuliweza kujiongeza na kuulizia kuhusu afya ya Rais. Tulikuwa na wajibu huo na tutaendelea hivyo kwa kila litakapotokea jambo lisilo la kawaida.
Mkuu;
Huwezi kusema CHADEMA wote ni wapumbavu!
Ninadhani ni baadhi ya wanaCHADEMA.
Tatizo mnajifanya kujua mno humu mitandaoni.. Mmewashika akili wapumbavu kuamini vijineno vyenu. Mnaumbuka taratibu, tumieni vidole vyenu wisely kutafuta comments na likes kwa njia hizo mtapoteaVicky Emmanuel Nchimbi wrote this piece [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Taarifa zinazosambazwa kuwa JPM amefariki si za kweli. Ni uzushi Zipuuzeni. May be if he will die in future on God's will, but as for now he is alive. It's true alipata heart attack akiwa ziarani kusini na kukimbizwa Dar usiku kwa helcopter ya jeshi kisha akasafirishwa to SA then Germany. Mama Samia aliitisha cabinet jana to adress the situation and all security organs are alerted.
Taarifa rasmi haijatolewa kwa sababu ya kuhofia kuiweka nchi kwenye tention unnecessarily. Kwa hiyo ili kupunguza minong'ono iliyopo imebidi itolewe taarifa ya uteuzi aliofanya kabla hajaugua. Ni idea iliyotolewa na Mzee Lukuvi just to calm people down. Ndio maana watu wanahoji if he is okay kwanini asijitokeze hadharani hata kwenda kununua samaki kule ferry as he used to be? uteuzi haujafanywa leo, isipokuwa leo umetangazwa tu. And the one who announced is Gerson not JPM.
Kutumia uteuzi as derteminant that he is okay is wrong. He is not okay and he is not in the country. Ndio maana hata kwenye mkutano wa AALCO he will be represented by mama Samia. Lets pray for him for the quick recovery. I'm told leo kapata nafuu na kaweza kufungua macho usiku huu. These are good news lets keep push the prayers. Hata kina Bashe na Polepole wamepata ujasiri to speak it out baada ya mzee kufungua macho usiku huu. Lakini tangu juzi alipozidiwa they were quet as absent b'se they couldnt anticipate what nature could provide.
The most important thing let's keep praying for him, and send our gratitude to Germans kwa kupambania afya ya baba yetu. Tusimuombee mabaya just b'se of political dissimilarities. Our prayers, our unity, our nation, our President.
Wamejishushia heshima sana, tena katika wakati mbaya sana. wasubiri majibu ya kazi yao 2020Huo umoja wa kitaifa kuyumba sababu ya tweets za akina Zitto mzee? Yaani kakikundi ambacho tunajua hadi fake IDs zao ndio unasema taifa? Unajua mliheshimika sana kiasi kwamba sasa significant number imeanza kujua motives zenu!
Hakuna sehem nimekubali ya kigogoHahaha! Britanica Bhana.
Kigogo kawafanya watoto nanyi mmekubali
Mkuu mbona una conclude kwamba Rais ni mgonjwa, umejuaje? Kigogo kadanganya watu hadi kufikia kutaja chumba ambacho ati Mh Rais alilazwa huko Ujeremani! Bado unasema Kigogo siyo muongo kwa 100%!! Ajabu
Dah...Acha ujinga bana..watampendaje mtu aliyekata mirija yao ya ufisadi na wizi? [emoji44]daah sijaamini yani kuna wananchi walifurah sana raisi wa nchi kuumwa yani kuna wengi sana wasiompenda Jamaa aisee
Huo umoja wa kitaifa kuyumba sababu ya tweets za akina Zitto mzee? Yaani kakikundi ambacho tunajua hadi fake IDs zao ndio unasema taifa? Unajua mliheshimika sana kiasi kwamba sasa significant number imeanza kujua motives zenu!
mkuu pls ongea ukweli, zote tunajua hali ya tz, taifa liko katika janga kubwa, kisiasa, kiuchumi na hata kielimu, magufuli is EVIL1.Watu wengi tena waliosoma bado wanaamini tatizo linaweza kutatuliwa kwa kumtakia mtu jambo baya, dhana ya kuwa sisi ndio nahodha wa maisha yetu na maisha tunayoyaishi ni uamuzi wa machaguo tuliyochaguo na sio bahati nasibu wala mtu mwengine kusababisha tuwe tulivyo.
2.Upinzani bado hawajakua, bado hawajawa mbadala wa CCM, Wengi wanamchukia Magufuli kwasababu ya kuminywa mirija yao na sio wana uchungu na Watanzania.
3.Serikali imefanya jambo lililosahihi, kwa wakati sahihi katika namna sahihi kabisa.
4.Inawezekana kukawa na mageuzi makubwa ya vyombo vyetu vya usalama na ile mianya ya kuvuja kwa siri ambazo wengine hatupaswi kujua imeanza kuminywa kimya kimya, watu wenye kazi zao wapo kazini.
5.Watanzania tunapenda sana umbeya na Majungu, zamani tulikaa katika vijiwe vijiwe sasa hivi Teknolojia imeturahisishia kuendeleza tabia zetu za umbeya na Majungu.
Amina. Na tunazidi kuomba awepo hata zaidi 2025 kwa ajili ya kushirikiana na watanzania wenzake kwa namna yoyote ile inayofaa kuiboresha Tanzania kwa nyanja zote.Ni kweli afya ni mgogoro. Ila sio kama walivyozusha kuwa kafa. Yaani hafi leo wala 2020.Tunaye mpaka amalize 2025.
Mimi nilichojifunza ni kuwa serikali ya sasa imeanza kubadilika kwenye nyanja ya mawasiliano kwa umma hasa namna ya kukabiliana na tuhuma na uzushi wa kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa jinsi ambavyo serikali/Ikulu imekabiliana na uzushi uliofanyika kwa muda wa siku tatu kuhusu afya ya Rais Magufuli imeonyesha mabadiliko makubwa sana!
Nakumbuka wakati Rais Magufuli anaingia madarakani alikuwa anapenda kujibu kwa maneno kila tuhuma na uzushi uliohusu yeye au serikali yake bila kujua kwa kufanya hivyo alikuwa anawapa umaarufu wale ambao walikuwa wanatoa uzushi au tuhuma.
Kujibu kila uzushi na tuhuma kwa maneno ndio kulimpa umaarufu Mwana Mama aitwaye Mange Kimambi ambaye alijikuta akipata wafuasi zaidi ya milioni 1.2 kutoka laki 300000.
Kanuni moja ya kukabiliana na uzushi ni kuupuuza na kama ukiona bado unaendelea basi unachofanya ni kuonyesha ukweli kwa vitendo katika muda mwafaka kwa sababu uzushi ukiachwa kwa muda mrefu uendelee kuwepo huanza kuaminisha jamii.
Uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli imejibiwa kwa muda mwafaka lakini kikubwa zaidi njia iliyotumika katika kujibu imeondoa imani (credibility) yote ya yule aliyeuanzisha na kuushupalia lakini vile vile waliouamini wameonekana ni wajinga au wapumbavu.
Kitu kingine nilichojifunza baada ya kuona baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kama Zitto Kabwe, Dkt Vicent Mashinji na Godbless Lema wakiamini uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli ni kuwa viongozi wa vyama vya upinzani hawajui linaloendelea Ikulu. Kwa maana nyingine, siri za Ikulu kwa sasa hazitoki kwa urahisi. Fikiria viongozi wa vyama vikuu vya upinzani hawajui hata alipo Rais wa nchi achilia mbali afya yake!
Mwisho kabisa nimejifunza kuwa inatakiwa kwanza kuchukua muda kabla ya kuamini kile ambacho kimeandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ukweli hukawia kufika.
Nimalizie kwa kuandika, Nimeamini Uongo hupanda kwa lifti. Ukweli hupanda kwa ngazi ili kumfikia mlengwa!