PreGE2025 Tumekuwa a Failed State. Kila kitu kimekamatwa na Dola ya Chama. Si Mahakama, Si vyama vya Siasa, Si Majeshi, si Taasisi za Dini, Si Katiba

PreGE2025 Tumekuwa a Failed State. Kila kitu kimekamatwa na Dola ya Chama. Si Mahakama, Si vyama vya Siasa, Si Majeshi, si Taasisi za Dini, Si Katiba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
Its Official,
Tanzania sasa ni rasmi a failed state. Nchi imeanguka rasmi kwenye kikundi kidogo cha dola ya CCM. Kikundi hiki ndo kinaamua mambo yaendeje, lipi litokee na lipi lisitokee, kipi kifanikiwe na kipi kisifanikiwe. Yupi anastahili kuishi na yupi hastahili kuishi. Wananchi muone nini, muongee nini na msikie nini.

kuanzia vyombo vya ulinzi na usalama, mifumo ya uwajibikaji na kutazamana ( Accountability, Checks and Balances), Mifumo ya Haki (Mahakama), Mifumo ya Kisiasa (Vyama vyote vya Siasa kasoro Chadema), Bunge na Madhehehu ya Dini vyote vimekamatwa na kikundi hiki kidogo cha dola ya CCM.

Kwa sasa kikundi hiki hakiogopi kumshughulikia mtu yeyote anayejaribu kuwafungua macho wananchi awe Kiongozi wa Dini ( Mfano Gwajima na Father Kitima) awe mwanasiasa au chama cha siasa ( Mfano Tundu Lissu na Chama chake Chadema) au kiumbe yeyote yule.

Poleni sana Watanzania. Sasahivi hatuna tofauti na Congo DRC ( Nchi ya Uchawa,Mziki, Michezo, Starehe, Ufisadi wa Kutisha na Umasikini) na Eritrea ( Nchi yenye total control ya dola juu ya Wananchi na Maisha yao huku Wananchi wakiwa hawana haki yeyote na umasikini wa kutisha)

Tujiandae tu na matokeo ya haya.

Lord denning
Mwanza
 
Zile clip kuhusu tisheti za CCM zinavyokuwa printed huko China ndo karatasi za kura zinavyokuwa printed huko China.

Waambie na ndugu zako. Saivi ni akili kumkichwa, kila mtu anajua atakavyopambana
 
Simba anakoroma usingizini unatetemeka, akiamka akaunguruma?
 
Back
Top Bottom