Tumesahau alichofanywa Dkt. Ulimboka, Mwangosi na Said Kubenea. Nchi hii ni ya kinafiki sana

Tumesahau alichofanywa Dkt. Ulimboka, Mwangosi na Said Kubenea. Nchi hii ni ya kinafiki sana

Nimemwambia nani anyamaze?

Nmemwambia mbali na kukosoa ila atafute hela aondokane na umasikini unaomsababishia kuwa na stress na kuandika vitu vya kijinga
Wewe ndiye maskini ndiyo maana umejipa kazi ya kumsifia mwenda zake ukitegemea utateuliwa, safari hii teuzi za kimalaya malaya mlizozoea enzi ya mwendazake hakuna. Sisi tulishazoea kuishi bila mbeleko na maisha tumeyapatia kitambo tu.
 
Hii nchi hakuna kundi la "wanafiki" kama CHADEMA.
Hili ni genge wa "wahuni" na "wanafiki" kupindukia.
Sasa hivi wanamshabikia Madam SSH utafikiri yeye siyo mwana-CCM. Kila analofanya SSH wanampa sifa na kumtukuza as if she is one of them.

Wamesahau kwamba mvinyo ni ule ule, kilichobadilika ni chupa tu basi.
Ccm pia imewapa vyeo wapinzani
 
Na Dr Sengondo Mvungi je?

Na kubenea na Boss wa GSM na sakata la tindikali je?
Segondo mvungi ni vibaka,,,boss wa GSM ni mauhasama labda mambo ya kibiashara,,,kubenea yule ni afiea kipenyo sasa sijui aliudhi nani,,
Kumbuka na chadema enzi hizo pia walikua na mbinu za kuteka,ile kashifa ya slaa kutuma watu wakamteke jamaa gani sijui,,
Kiufupi,kuna special interest groups pande zote mbili zilikua zina operate with impunity
 
Acha kujisumbua wewe, kaa ukijua kuwa 80% ya Watz akili zao wanazijua wenyewe, wamejaa ujinga hadi wanatisha..
 
Nakumbuka kulikuwa na mzungu alipewa kazi ya kusimamia menejimenti, Ulimboka akawaongoza madaktari kumtoa ofisini mzungu yule.

Alifanya fujo akisahau kuwa JK alikuwa kashika mpini. Picha yake akiwa amelala kitanda cha hospitali iliwatia huruma watu wengi walioitazama.
Marais wote duniani wana power sana kisheria,ndo maana za kuitwa Rais au mfalme,,ana mamlaka ya kutangaza vita,kusaini hukumu za vifo na hata kuamuru mtu awe eliminated iwapo maslahi ya nchi yanatishiwa,,mamlaka yanaruhusu,,sasa hapo inategemea hekima za kiongozi,husika,,
Kiongozi wa nchi hawezi kuona wananchi wanapoteza maisha kwa ajili ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache,,kuna redline ukivuka hata mtu awe mwanademokrasia kiasi gani,,atakupoteza tu,na hii iko dunia nzima..
 
Namaanisha kuelekea 2015 watanzania waliikataa ccm na kikwete. ikapelekea kikwete kuangushwa kwenye uchaguzi yaliyoendelea baada ya uchaguzi ni historia
Umekosea,2015 aligombea chuma sio jk
 
Unaongelea watz hawa waliojaa unafiki, hata Rais akiwa Kingwendu utawaona wanavyosifia kama mazuzu. Wanaojiita wasomi sasa ndio balaa kusifu mwanzo mwisho
 
Marais wote duniani wana power sana kisheria,ndo maana za kuitwa Rais au mfalme,,ana mamlaka ya kutangaza vita,kusaini hukumu za vifo na hata kuamuru mtu awe eliminated iwapo maslahi ya nchi yanatishiwa,,mamlaka yanaruhusu,,sasa hapo inategemea hekima za kiongozi,husika,,
Kiongozi wa nchi hawezi kuona wananchi wanapoteza maisha kwa ajili ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache,,kuna redline ukivuka hata mtu awe mwanademokrasia kiasi gani,,atakupoteza tu,na hii iko dunia nzima..
Ni kweli kabisa rais ni cheo kikubwa sana, ukimchezea unashughulikiwa tena na watu ambao hata yeye mwenyewe pengine hafahamu sura zao zinafananaje.

Kombe wa usalama wa taifa alinyoosha mikono kukubali akamatwe lakini wapi, waliotumwa wakimpelekea shaba na kummaliza.

Apson alichukuliwa mzobe mzobe kutoka pale mbezi beach na kwenda kufungiwa oysterbay baada ya JK kuchukua nchi.

Mzee Mwinyi alikuwa muungwana sana, ilikuwa vigumu kwa watu kuzichezea hasira zake. Mkapa mpaka aliomba msamaha kwa yale yaliyotokeaa visiwani Zanzibar.

Nyerere enzi zake pale wizara ya mambo ya ndani ukipita barabarani ulikuwa unaviona vibanda fulani vya mbao zenye rangi nyekundu, kuna muda unasikia sauti za watu wanaolia wakiwa wanapokea mateso.

Siungi mkono unyama wa viongozi lakini upo, rais ni cheo kikubwa sana. Madonna aliongea shombo kumhusu Trump mamlaka za kipolisi zikamwambia afute kauli na akaifuta.
 
Huwa nawatafakari sana Watanzania wa kizazi hiki wanaoimba kikwete alikuwa anapenda demokrasia. Najiuliza je Dr. Ulimboka au Mwangosi naye anasema hivyo hivyo Marehemu huyu?

Najiuliza waliouawa kwenye chaguzi ya Igunga nao wanasema hivyo hivyo au lile bomu lililolipuliwa kule Arusha kwenye Mkutano wa Chadema? Akina Alphonse Mawazo nao wanakubaliana na hoja hii?

Haya yalitokea katika Utawala wa kikwete. Kumwagiwa Tindi Kali na Kinusurika kuuawa Dr. Ulimboka baada ya kutupwa katika Msitu wa Mabwe pande.

Katika miaka kadhaa Tanzania haikuwahi kuwa salama. Isipokuwa Watanzania ni wanafiki kwa kiwango kikubwa. Kwani ni lini kauli za kuanza kusema Chadema itakufa zilianzishwa?

Kwani Dkt. Slaa na mkewe walipopigwa na kuvunjwa mkono Dr. Slaa ilikuwa lini? Mpaka Dr. Slaa kununuliwa kusaliti wapinzani ilikuwa Utawala upi?

Yaani tumesahau Richmond,Iptl,Tegeta Escrow na kashfa nyingi za kutisha? Madawa ya kulevya na ufisadi mkubwa na kisha Rais kuja sema wahusika wakikamatwa nchi itayumba akicheka mbele za umma wa watanzania?

Watanzania ni wanafiki kwa kiasi kikubwa sana. Ni watu wa kuogopwa sana. Kilichomfanya kikwete aonekane ni bora pia ni unafik wake wa kuweza kuuma na kupuliza.

Dkt. Magufuli hakuweza kupuliza. Aliuma na kuacha maumivu yaendelee kubak. Utawala wake ulikuwa ni ule ule wa Ubabe akilazimisha alichoamini kuwa ni maendeleo. Hakutaka kupingwa.

Jamani tumesahau Makonda alipewa zawadi ya Ukuu wa Wilaya baada ya kufanya kitendo gani cha kishujaa? Uhuni uliofanyika katika mchakato hewa wa Katiba na Mabilion ya pesa yaliyotumika?

Tunasahau kwa kuwa angalau wapinzania walikuwa wakipewa poshi kutulizwa n.k akina Zitto Kabwe na Mbowe mara kadhaa walipokuwa wakimbana sana kikwete alikuwa anaonana nao wanayamaliza.

Magufuli alikuwa hashirikiani nao katika misingi hiyo. Aligoma hata aliposhauriwa kuwa awe anaonana nao "kuwatoa kiaina" yeye aliwatenga kabisa. Hapa alikosea.

Leo hii ungewachukua akina Dr. Ulimboka, akina Mwangosi n.k ukawaambia Kikwete alikuwa mwanademokrasia wataangua kilio kikubwa. Aliyetuhumia kuhusika na hujuma ile ya Dr. Mwangosi alisemekana kuwa Ikulu. Hakushtakiwa akapewa zawadi ya Cheo.

Hili wanasiasa wengi hawazungumzi sababu Dr. Mwangosi hakuwa mwanasiasa. Kumbe angekuwa mwanasiasa angekuwa Tundu Lissu wa miaka ile. Tumesahau Madawa ya kulevya yalivyokuwa moja ya biashara kubwa nchini. Na vijana wetu wengi kuharibika mitaani wakiwemo wasanii.

Watanzania tutabadilisha nchi ikiwa tutaacha unafiki na kuamua kwa dhati kupambana na tawala zote dhalimu. Tupambane Katiba iweze tenga Nguvu kubwa wanayopewa marais juu ya kila sheria na kila mtu kufanya wapendavyo.

Tukiendelea na ubinafsi kuangalia watu kimaslahi, kidini na kikabila. Kila mwaka tutagawanyika kwa misingi hiyo na maadui watatutawala. Kama tutaendelea kusema moyoni huyu ni wa kwetu sisi. Nchi hii itasimama hapa huku wabunge wakitaka waongezewe mishahara bila woga kabisa.

Mimi nmeasi chama. Nmebaki na Utanzania wangu. Tumeona madhara ya kuwa na Katiba Mbovu sasa tuililie katiba mpya. Tunaweza jisahau kwa kulambishwa asali wakati tunaumwa Kansa na mguu unaoza. Tutapewa dawa ya usingizi tukija shtuka mwili wote umeoza kwa kansa.
ongea utakavyoweza, ila kamwe huwezi fananisha wakt wa kikwete na magufuli, ni sawa na kufananisha moto wa kibatari na moto wa gesi..
 
Wakukumbukwa na kuenziwa nchi hii ni Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere tu, hao wengine wote wametuingiza kwenye matabaka mabaya kabisa, hebu msikilize kwa makini Chipukizi huyu, he was the only President I can dare to call Hero of the Nation

Nyerere aliitwa Ndugu
Tena huyu ndio muasisi wa yote haya katuachia uozo mkubwa. Japo ukimlinganisha na hawa kenge maji he is far better. But trust me we have been brainwashed for decades kuhusu JKN. Dig deep na ruhusu akili yako kuwa flexible and elastic utagundua.
 
Back
Top Bottom