Tumeshaachana wivu na vituko vyanini? Ila ke wembamba wana visa sana.

Tumeshaachana wivu na vituko vyanini? Ila ke wembamba wana visa sana.

Jana night nikatoka na chaguo la moyo tubadili hata dinner tuupumzishe ugali dagaa kidogo, hao tukaenda kiwanja fulani jina kapuni kwa ajili ya kulinda brand.

Tukiwa tunaingia pale tunaangalia wapi pa kukaa ukizingatia ni sikukuu watu ni wengi karibia kila meza imejaa wadau, ghafla mbele yetu nashangaa kuna ke wawili wanatuangalia sana, kutupa jicho vizuri mmoja wao nikamtambua ni dear Ex ambae wiki iliyopita tulikutana kwenye usafiri tukaishia kukodoleana macho tu. Huyu alinileteaga habari za kutaka kunipanda kichwani nikampotezea baada ya muda akanitumia ujumbe anaolewa nisimtafute, hata sikuhangaika kumjibu kitu kwa sababu tangu tutengane sikuwahi kumtafuta, baada ya muda alitaka kurudi ila sikumpa nafasi.

Alichokifanya ndio nilikiona kituko, sijui alikuwa anathaminisha kama huyu nilienae sasa kamzidi au la, alimuangalia ke wangu juu mpaka chini, zaidi ya mara tatu huku akijiangalia nayeye akiteta jambo na dada aliekuwa nae huku wakiniangalia pia. Sikutaka ke wangu ahisi chochote kama tunafahamiana kwahiyo nilitulia nikaona nafasi ya kukaa nikamshika mamtu mkono hao tukaenda kukaa kungoja huduma.

Sijui walidhamiria nini tulivyokaa tu nao wakaja kusimama jirani na meza tuliyokuwa huku bado akimuangalia sana ke wangu mpaka akaniuliza mbona hao wadada wanatuangalia sana hadi naogopa unafahamiana nao? nikajibu siwajui huenda washalewa sisi tuhusike na yetu upo na mimi usiogope chochote atafuliwa mtu bila sabuni akitaka kuleta shido, akacheka nikamwambia yes napenda ukiwa na furaha na chanzo cha furaha yako kikiwa ni mimi napenda zaidi(maneno mazuri na matam hapa ndio pake), uzuri huwa ananielewa situmii nguvu kubwa kumuaminisha jambo.

Kichwani najiuliza maswali bila majibu hivi huyu nguchiro anataka nini? Mbona anatuangalia sana anaplan gani asije akaleta shida maana wanawake wembamba kwa kupenda ugomvi na kalivyo na kamdomo asijeakatuvurugia usiku wetu. Nikajisemea tu athubutu aone, tukala tukamaliza tukaondoka zetu salama.

Mishale ya saa 7 kasoro usiku ikaingia text no ngeni inayosomeka "sawa bhana si unajifanya mjanja na huyo kiumbe wako " nikaifuta chap kuepusha mengineyo. Hapa atafululiza kunitafuta kwa kila namna mpaka aniharibie, sijui ni kashirikina haka kamshale.
Kbabaake 😃😃😬😬
 
usipende kuhukumu kundi zima la watu kwasababu ya mtu mmoja tu

umejuaje wanawake wembamba wote wana visa?

yaani hasira zako unahamishia wadada wembamba?

huyo mdada mwembamba si ulishamfaidi, ila sasa unamponda
Kwa asilimia kubwa wapo hivyo, simsemi vibaya ila ni mwanamke ambae ni vigumu sana kuishi nae kwenye mahusiano ana drama nyingi sana.
 
Ke wembamba kumbe ndio vitu vyako mkuu, hata me nawakubali.
 
Mimi nilimfukuza geto na moyoni ke wembamba jau sana.Nguchiro yangu ilipata likizo kazini kwake mkoani ikaja nilipo.Kesho ameamka afanye usafi na kuweka sawa mazingira mimi nilienda kujaza gas ya kupikia.Simu niliiacha chaji,akachukua namba ninazoongea nazo sana zenye majina ya kike karibia kumi mpaka bimkubwa,akawa anawavutia waya mmojammoja.Kidogo aniharibie hadi michongo ya hela,aisee aliondoka muda huohuo hakupata hata muda wa kunawa uso na usafi nilimalizia mwenyewe.
Mipango ya ndoa iliishia hapohapo japo kelele zilikuwa nyingi ila nashukuru zilitulia.
 
Hivi mtu mwembamba mwenye gubu akibongeka gubu linaisha au?
 
Mimi nilimfukuza geto na moyoni ke wembamba jau sana.Nguchiro yangu ilipata likizo kazini kwake mkoani ikaja nilipo.Kesho ameamka afanye usafi na kuweka sawa mazingira mimi nilienda kujaza gas ya kupikia.Simu niliiacha chaji,akachukua namba ninazoongea nazo sana zenye majina ya kike karibia kumi mpaka bimkubwa,akawa anawavutia waya mmojammoja.Kidogo aniharibie hadi michongo ya hela,aisee aliondoka muda huohuo hakupata hata muda wa kunawa uso na usafi nilimalizia mwenyewe.
Mipango ya ndoa iliishia hapohapo japo kelele zilikuwa nyingi ila nashukuru zilitulia.
Mnatuonea wadada wembamba, huyo wako ni yeye ndio hajielewi ila si wote wana hiyo tabia.
 
Back
Top Bottom