DOKEZO Tumevunjiwa maeneo yetu ya biashara Tungi Mnadani - Kigamboni bila taarifa, tunaomba msaada wa Serikali

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mie nimeelewa sana maelezo yako,
Kwann msingeomba mkutane na WO na huyo Rostam ili mpate ukweli nani mwenye eneo.

Huenda mngepata suluhisho.
Siku tunaenda kukutana World Oil waliitwa hawakuja, na kama umesoma hapo barua ya wito Kwa world Oil, Sasa mtu ameitwa amekaidi kuja tutapata jibu Gani?
 
Hilo eneo hata kama lingekuwa la Rostam kweli hakuna utaratibu wa kukabidhiana ardhi kienyeji hivyo, lazima kuwepo na nyaraka kwamba Rostam aliwakabidhi mfanyie biashara hapo. Mnazo hizo nyaraka au uthibitisho wa kulipa kodi kwake ya kupanga hapo?
Kwa nini mnataka awalipe fidia wakati hamjajua nani atashinda hiyo kesi kati ya World Oil na Rostam? Vipi kama hilo eneo halikuwa la Rostam kihalali kwa kuanzia bali ni la World Oil??
 
Sasa wangekua wanawapa taarifa kua tunataka eneo letu lasivyo tunabomoa mabanda yenu.

Sasa kufanya hivyo usiku ndo nn?
Kwa taarifa za chini n kuwa walishapewa taarifa ila kama kawaida tunangojaga ngojaga.

Kama kikao kilifanyika mwezi wa 9 ni wazi kuna maamuzi yaliyotolewa, hayo mabanda hayana muda tangu yavunjwe.
 
Anayetakiwa kulipwa fidia kwa maelezo yako ni Rostam Aziz, kama hajadai fidia mahakamani basi World Oil haiwezi mlipa.

Nyinyi sio wamiliki wa eneo, mnalipwa fidia kwa lipi?
Kama unadai Rostam aliwapa eneo mfanye biashara basi hakuwapa hati, na kama World Oil wanataka hilo eneo hawajakurupuka yawezekana wanaumiliki nalo. Kuondoa mkanganyiko uko wilayani idara ya ardhi mtafute mmiliki wa eneo nani kama atakuwa Rostam basi aliyevunja awape fidia ya uharibifu provided mtatoa ushahidi usio na shaka kwamba Rostam aliwapa ruhusa kutumia eneo lake. Kama mmiliki sio Rostam hamstahili kulipwa.
 
Ni kweli kabisa, lakini RA na WO walisema hii kesi ipo mahakamani, Sasa kwanini watuingize sisi???? Kwanini sisi ndio tuvunjiwe biashara wakati hata hatujui ugomvi wao??????? Kwanini WO asiende kugombana na RA badala yetu
Ili kujua ukweli kwamba hilo eneo ni la RA mlitakiwa mjue WO kalinunua toka kwa nani
La sivyo mtakuwa mli sukumiziwa huko baadae muwe kama kinga 😆
 
Kwa taarifa za chini n kuwa walishapewa taarifa ila kama kawaida tunangojaga ngojaga.

Kama kikao kilifanyika mwezi wa 9 ni wazi kuna maamuzi yaliyotolewa, hayo mabanda hayana muda tangu yavunjwe.
Maamuzi yaluyotolewa ni kufanya tathmini na kulipwa fidia, hakuna uamuzi mwingine isitoshe kwenye kikao Cha tarehe 9 World Oil hakuhudhiria
 
Maamuzi yaluyotolewa ni kufanya tathmini na kulipwa fidia, hakuna uamuzi mwingine isitoshe kwenye kikao Cha tarehe 9 World Oil hakuhudhiria
Pambanieni mnachoona ni haki yenu ila hapo ni pagumu, tukirejea na ile kauli ya Rostam kuhusu mahakama zetu ndio ugumu unazidi.
 
Sijasoma ila nakupa taarifa kwamba serikali ndo imebomoa hivyo hivyo vibanda. Labda msaada uende ukapate kwa wapinzani.
 
very sorry mkuu, nilipita hili eneo siku moja kbla ya kuvunjwa nika spot kitanda kimoja cha mtumba kikali sana nimpelekee Dogo wangu anaanza maisha, the next day nimepita nikaona kama sielewi kumbe ndo hiki kilitokea. poleni sana
Mchekini yule waziri wa Ardhi personally kama vipi, lkn je eneo hilo mna umilik nalo?
Msalimie Happy!!
 
Hasemi kauziwa ila anasema tu tutoke kwenye sehemu yake. Na ROSTAM anasema hiyo sehemu tusitolewe kwasababu yeye ndio MMILIKI na Hana Taarifa za Hilo eneo kumilikiwa na worl oil
Nyie mna uthibitisho wa kupewa hilo eneo na Rostam? Kwa nini Rostam asitume watu wake mwenyewe au haendi polisi kumzuia World Oil kuwaondoa nyie wapangaji wake badala yake anawaambia tu msiondoke??
 
Hasemi kauziwa ila anasema tu tutoke kwenye sehemu yake. Na ROSTAM anasema hiyo sehemu tusitolewe kwasababu yeye ndio MMILIKI na Hana Taarifa za Hilo eneo kumilikiwa na worl oil
Poleni sana sana.

Ila Sasa hapa fidia anawalipaje mkuu? Huu ni mgogoro wa wamiliki wawili ninyi hamuhusiki, nakama mgogoro unaendelea hapaswi mmoja wao kuendelea kunufaika na hilo eneo hadi maamuzi yatapopatikana nani mmiliki halali.

Nachokiona hapo ninyi mnaingilia mgogoro ambao hauwahusu, ninyi sio sehemu ya umiliki wa hilo eneo waacheni wanaojiita wamiliki wapambane wenyewe hapo mtaishia kupata hasara na serikali haiwezi kuwasaidia chochote.
 
Poleni
Ila naomba nikuulize swali moja tu ambalo litasaidia sana kutatua hii shida yenu
Je kuna mkataba mliandikishana na “Bwana Rostam”???
Au kuna maandishi au kuna maneno walau yaliyorekodiwa ?
Wakati mnakabadidhiwa mlikua na kina nani kama mashahidi
Au ni my words against urs?
Kama kuna mkataba au maandishi ya makabidhiano wala huitaji serikali
NENDENI MAHAKAMANI
 
Ni kweli kabisa, lakini RA na WO walisema hii kesi ipo mahakamani, Sasa kwanini watuingize sisi???? Kwanini sisi ndio tuvunjiwe biashara wakati hata hatujui ugomvi wao??????? Kwanini WO asiende kugombana na RA badala yetu
Nyie mko upande Rostam Aziz kwa hiyo World Oil tayari anagombana na Rostam Aziz kwa kuwaondoa nyie kama wavamizi wakazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…