Chambusiso
JF-Expert Member
- Jul 11, 2007
- 2,592
- 4,640
Si mmeshamaliza kuwachagua wandugu? Mlitegemea ile petipeti itaendelea! Mnaposikia kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe mnafikiri ni mbinguni? No ni hapahapa wazee
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maandishi ya Rostam kuwapa hiyo ardhi yapo? Mna transfer documents ? Zilipita wizara ya ardhi? Ardhi huwezi kupewa kama unavyopewa pipi, hasa iliyopimwa.Aisee watu mnapenda kukurupuka sana, hivi we Kwa akili Yako unahisi mtu aende avamie sehemu hajui ya nani aanze kufanya biashara Tena ya pesa kubwa?????
Hii sehemu ni ya ROSTAM AZIZI.
NA kama mmesoma vizuri hapo hatimiliki ni jina la ROSTAM AZIZI, na sisi yeye ROSTAM ndio alikabidhi hii sehemu kwetu. Baadae jirani na sehemu hii ya ROSTAM ambapo ndio tunafanyia biashara akawa amenunua World Oil. Mara ghafla akaja anatwambia hii sehemu tulipo pia ni ya kwakwe, swali hii sehemu inakuwaje ya kwakwe wakati alietukabidhi hapa ni ROSTAM AZIZI?????
Kuja kufuatilia tukaambiwa ROSTAM na world Oil wana mvutano, na ndo maana Huyu MMILIKI WA WORD OIL anasema hii sehemu ni yake tuondoke.
Sasa na sisi kama wafanyabiashara hatukutaka kero tukakubaliana nae atulipe fidia tuondoke yeye akamalizane na ROSTAM Sasa inakuwaje badala ya kutulipa yeye anatuma watu wabomoe?????
Siku nyingine muwe mnasoma na kuelewa sio mnakimbilia kusema msoyajua
ommytk
chiembe
Msigazi Mkulu
Yoda
Na wengine punguzeni ujuaji
Mnakiri wazi eneo sio lenu.afu mna taka mlipwe fidia ? Amjui kama jamaa akikaza nyie ndo mta takiwa kumlipa fidia kwa kufanya uharibifu na ku trespassAisee watu mnapenda kukurupuka sana, hivi we Kwa akili Yako unahisi mtu aende avamie sehemu hajui ya nani aanze kufanya biashara Tena ya pesa kubwa?????
Hii sehemu ni ya ROSTAM AZIZI.
NA kama mmesoma vizuri hapo hatimiliki ni jina la ROSTAM AZIZI, na sisi yeye ROSTAM ndio alikabidhi hii sehemu kwetu. Baadae jirani na sehemu hii ya ROSTAM ambapo ndio tunafanyia biashara akawa amenunua World Oil. Mara ghafla akaja anatwambia hii sehemu tulipo pia ni ya kwakwe, swali hii sehemu inakuwaje ya kwakwe wakati alietukabidhi hapa ni ROSTAM AZIZI?????
Kuja kufuatilia tukaambiwa ROSTAM na world Oil wana mvutano, na ndo maana Huyu MMILIKI WA WORD OIL anasema hii sehemu ni yake tuondoke.
Sasa na sisi kama wafanyabiashara hatukutaka kero tukakubaliana nae atulipe fidia tuondoke yeye akamalizane na ROSTAM Sasa inakuwaje badala ya kutulipa yeye anatuma watu wabomoe?????
Siku nyingine muwe mnasoma na kuelewa sio mnakimbilia kusema msoyajua
ommytk
chiembe
Msigazi Mkulu
Yoda
Na wengine punguzeni ujuaji
huwajui waswahili wewe, huoni hata huyu eneo sio lake walala la bibi yake lakini kashajimilikisha eti anataka fidiaBasi wangetumia busara, siku 1 kabla ya kubomoa, wangewapa taarifa.
Wangetumia utu wa kibinadamu.
Mbona hadi leo naona vitu vyenu bado viko pale huku vinanyeshewa na mvua,mmevisusa au mna kesi Mahakamani hamtaki kuharibu ushahidi!!??Sisi Wafanyabiashara wadogowadogo tuliokuwa tukifanya shughuli zetu za biashara katika eneo lililopo jirani na ofisi za World Oil eneo la Tungi Mnadani, Kigamboni hapa Dar es Salaam.
Tulianza kufanya biashara kwa takribani miaka miwili iliyoputa na tukajenga vibanda vyetu eneo hilo, tulitumia biashara hiyo kuendesha familia zetu kwa kipato ambacho tulikipata hapo.
Miezi ya hivi karibuni kukatokea mvutano baina ya pande mbili ambazo zote zilijitambulisha kuwa zinamiliki eneo hilo.
Upande wa kwanza ni Ofisi ya World Oil ambao walitutaka tuhame eneo hilo wakidai ni la kwao, tuliwapinga na tukawasilisha malalamiko yetu kwa Ofisi ya Katibu Tawala Kigamboni, akawaandikia barua ya wito ili kujadili suala hilo.
Mazungumzo yakafanyika kati yetu Wafanyabiashara na World Oil tukakubaliana nao kuwa watatulipa fidia ili kuondoka eneo hilo, japokuwa kulikuwa na upande wa pili wa mmiliki mwingine ambaye ni mfanyabaishara maarufu naye alidai lile eneo ni lake.
Wakati tunasubiri kujua hatma ya eneo hilo, tumekuta miundombinu ya biashara zetu yote imebomelewa usiku, hatujui aliyebomoa lakini taarifa tulizopewa ni kuwa World Oil ndio wamehusika kubomoa maeneo yetu.
Tunaomba Serikali itusaidie kwani, kama ni mgogoro ulikuwa unaendelea kutafutiwa utatuzi ila kuna Wahuni wamejitokeza na kuvunja, wameharibu mitaji yetu, tumebaki na majuto.
Huyu ni nani ambaye ana nguvu kiasi cha kubomoa bila kibali na bila taarifa huku vitu vyetu vingi vikiwa ndani, kuna hasara kubwa imepatikana, tunaomba msaada wa Serikali Kuu inaonekana aliyefunja ana nguvu kuliko hata mamlaka za Serikali nyingine zilizowekwa huku Kigamboni.
Kumbe havijaondolewa?Mbona hadi leo naona vitu vyenu bado viko pale huku vinanyeshewa na mvua,mmevisusa au mna kesi Mahakamani hamtaki kuharibu ushahidi!!??
Yaani hata mvunjaji hajaendeleza chochote, hata usafi tu hakuna,mavitu yako pale yananyeshewa na mvua tu ila watu ndiyo hawapo!!Kumbe havijaondolewa?