DOKEZO Tumevunjiwa maeneo yetu ya biashara Tungi Mnadani - Kigamboni bila taarifa, tunaomba msaada wa Serikali

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Poleni sana .lakini serikali mnayoiomba msaada ndiyo imewapa ruhusa ya kubomoa vibanda vya biashara yenu
 
Uchaguzi umeshaisha
Uchaguzi umeshaisha na tumeshinda kwa 99%
 
Ene
Eneo mlipewa na nani??
 
Maamuzi yaluyotolewa ni kufanya tathmini na kulipwa fidia, hakuna uamuzi mwingine isitoshe kwenye kikao Cha tarehe 9 World Oil hakuhudhiria
Hayo maamuzi ya kulipa fidia yalitolewa na nani? Jiridhishe kama aliyetoa huo uamuzi ana mamlaka hayo kisheria.......(angalia namna migogoro ya ardhi inavyotatuliwa kisheria)........na kama kilikua ni kikao cha usuluhishi tu na upande mmoja haukutokea, je tunaweza kusema kwamba hiyo suluhu ya kulipa fidia ina mashiko yoyote?
 
Endeleeni kushangilia kwamba upinzani unakufa

First they came for the socialists, and I did not speak out—because I was not a socialist.

Then they came for the trade unionists, and I did not speak out—because I was not a trade unionist.

Then they came for the Jews, and I did not speak out—because I was not a Jew.

Then they came for me—and there was no one left to speak for me.

—Martin Niemöller
 
Uelewa wangu ni kwamba ili ulipwe fidia inabidi eneo uwe unalimiliki lakini likatafutiwa matumizi mengine na serikali hapo sasa ndiyo utastahili kulipwa fidia.

Kama mmeanza kufanya biashara miaka 2 nyuma na hao World Oil wapo tangu muda sielewi kwanini walitakiwa kuwalipa fidia.

Lakini unasema World Oil walikubali kulipa fidia, kama walikubali kulipa fidia kwanini wahangaike kuvunja vibanda? Hata wakivunja si bado watatakiwa kulipa?

Kuna kitu tunamiss kwenye hii ishu?
 

Unaomba msaada mvunjaji?
 
Kwanini mlipwe fidia na eneo siyo lenu?
 
Ni kweli kabisa, lakini RA na WO walisema hii kesi ipo mahakamani, Sasa kwanini watuingize sisi???? Kwanini sisi ndio tuvunjiwe biashara wakati hata hatujui ugomvi wao??????? Kwanini WO asiende kugombana na RA badala yetu
Kwanini mnaamini hili eneo linawahusu ikiwa wewe mwenyewe unataja mmiliki ni WO na RA?

Yaani nije tu uani kwako na godoro nianze kulala siku mkeo ananifukuza niseme nilipwe fidia.
 
Basi wangetumia busara, siku 1 kabla ya kubomoa, wangewapa taarifa.
Wangetumia utu wa kibinadamu.
Siwakandii lakini watu weusi sisi kadri tunavyozidi kupewa muda zaidi tunaona ni haki kuendelea kuwepo. Tunapenda kuhurumiwa hurumiwa sana bila kujali kuwa ni gharama. Ni mwaka juzi walivunjiwa tena ila bado hawaelewi.
 
Hii nchi ni matatizo kuanzia mwanzo kati mpaka mwisho..., Hata kama mwanzo hawa walikuwa wavamizi (wavunja sheria) na wa kati mmiliki hata akawa hajulikani (wawili wanagombania) na baadae kufuata utaratibu ikaonekana mmoja wapo wakae mezani wakakaa (na mwisho wakati wamekubaliana kukaa mwingine anavunja na kuharibu mali za watu)

In short the mtiririko mzima umefeli, kuanzia mwanzo mipango, watunga sera kushindwa kutengeneza sera za watu kuweza kupata ujira hadi kuwa wachuuzi na kuzagaa zagaa kutafuta riziki, hadi mtu kuvamiwa na wavamizi wa eneo lake na wakati wanavamia hakuna wa kuwakataza...

In short the whole system is rotten na Aliyesababisha tatizo ndio huyo mnamuomba kusaidia (The leg is rotten and needs amputation sio kufungwa a Band Aid)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…