DOKEZO Tumevunjiwa maeneo yetu ya biashara Tungi Mnadani - Kigamboni bila taarifa, tunaomba msaada wa Serikali

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Si mmeshamaliza kuwachagua wandugu? Mlitegemea ile petipeti itaendelea! Mnaposikia kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe mnafikiri ni mbinguni? No ni hapahapa wazee
 
Hii ndio serikali ya CHURA.watanganyika tutateseka MNO! Chini ya uyo znz.
All the best
 
Sa mnataka mlipwe fidia halafu eneo la azizi kawaeka Kwa hisan?
Mmejenga na kuwekeza kwenye eneo la mtu mwingine.mnalipwaje fidia.?
Hameni hapo katafuteni eneo jingine,mwacheni Aziz apambane na Wo.wakiyaweka sawa na muafaka uukifikiwa ndo mtajua mnarudi au la.
 
Poleni sana kwa yaliyowakuta. Mimi ningewashauri wafanyabiashara ndogondogo, badala ya kutumiwa na wanaiasa, hasa ccm, mitano tena, sijui mama anaweza n.k

Ni bora muungane, muombe maeneo salama, yanayokidhi biashara zenu mtulie. Serikali haikosi maeneo ya wazi ya kuwapa kufanya biashara, wakawa wanachukua ushuru.

Na uchaguzi wa mwakani ukiisha, mtakuwa na hali ngumu sana. Wa Kariakoo watatolewa, na nyote mliovamia maeneo ya wazi mtatolewa pia, sababu mtakuwa mmetumiwa, hamna kazi tena. Mjipange.
 
Maandishi ya Rostam kuwapa hiyo ardhi yapo? Mna transfer documents ? Zilipita wizara ya ardhi? Ardhi huwezi kupewa kama unavyopewa pipi, hasa iliyopimwa.

Mlipewa kama mtu mmoja mmoja? Mlifanya sub division ya viwanja? Mna kibali hicho? Nyaraka za kulipia kodi zinamtaja nani? Mlifanya search Wizara ya ardhi mkajua aliyewapa ni lake au kawaachia jumba bovu mjikinge mvua, na sasa limewadondokea?
 
Nikiwapa pole nitakuwa mnafki, ukweli ni kwamba eneo wanalo lalamika kubomolewa nila serikali? Je walikaa hapo na kufanya biashara kwa ruhusa ya nani? Waki itwa wavamizi ni sawa? Wanalipa pango?
Conclusion nikiwa kama Mtanzania najuwa matatizo ya watanzania wenzangu tuna penda kulalamika na kuonewa huruma sana kwa kisingizio wao ni maskini. Ukweli ni kwamba walivamia eneo wamejenga vibanda kimya kimya wamefanya biashara mwisho wakaona kama ni haki yao kuwa hapo,je hawa kujuwa kuwa walipo sio eneo la wazi, na hata kama ni eneo la wazi kuna utaratibu wa kwenda kufanya biashara eneo hilo. Wanapo taka fidia wao wanatoa fidia gani kwa kutumia eneo la mwenyewe kwa miaka miwili? tusipende sana kuwa watu wa kulalamika wakati ukweli upo wao ni wavamizi wasijitete kwa mgongo wa mikopo ndio mana kuna hasara sheria ikifwata mkondo na wao walipe fidia kuvamia eneo na kufanya biashara. Kuto kulizwa kwanini wamefanya biashara kwenye eneo miaka miwili hapa wapi nafasi wao kuona ni haki kufanya biashara ni eneo la watu watabaki kuwa wavamizi wa maeneo ya watu.
Mawazo yangu na niko tayari kurekebishwa
 
Mnakiri wazi eneo sio lenu.afu mna taka mlipwe fidia ? Amjui kama jamaa akikaza nyie ndo mta takiwa kumlipa fidia kwa kufanya uharibifu na ku trespass
 
Aliyekuwa RC wa Simiyu, Dkt Nawanda ashinda kesi ya “kumlawiti Mwanafunzi”, asema anamuachia Mungu
 
Basi wangetumia busara, siku 1 kabla ya kubomoa, wangewapa taarifa.
Wangetumia utu wa kibinadamu.
huwajui waswahili wewe, huoni hata huyu eneo sio lake walala la bibi yake lakini kashajimilikisha eti anataka fidia
 
Mbona hadi leo naona vitu vyenu bado viko pale huku vinanyeshewa na mvua,mmevisusa au mna kesi Mahakamani hamtaki kuharibu ushahidi!!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…