Nana addo si ndo amejiongezea muhula wa kugombea Ghana?
Hapana
Rais Nana Akufo Addo, wa Ghana ameshinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, kwa kupata asilimia 51.6 ya Kura, dhidi mpinzani wake wa karibu, Rais wa Zamani wa taifa hilo, John Mahama aliyepata asilimia 47.4 ya kura zote.
Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya Uchaguzi Ghana, Jena Mensa, ndiye aliyetangaza matokeo mjini Accra
Rais Akufo Addo ametetea nafasi yake hiyo,dhidi ya mpinzani wake huyo ambaye tangu awali alionyesha wasiwasi wake wa kutumika kwa nguvu ya Jeshi kwenye uchaguzi huo.
Bwana Mahama amelalamikia wizi wa kura. Akiongea muda mfupi baada ya tangazo hilo, Rais Akufo Addo amewashukuru raia kwa kumchagua.
"Nimeguswa tena sana na kuaminiwa nanyi na sichukulii hili kuwa jambo dogo...labda ipo tabia ya kuwa rais aliyepo madarakani akichaguliwa tena muhula wa pili anachukulia hilo kiurahisi na kuanza kupumzika ...lakini mimi ni wa tofauti.
Ninawashukuru sana , Waghana wenzangu kwa ushindi huu".
Ingawa Mahama hajakubaliana na matokeo hayo.
Hii ni mara ya pili kwa wapinzani hawa wa kisaiasa kukabiliana katika uchaguzi mkuu wa rais.
Ghana inasifika kuwa taifa lenye demokrasia barani Afrika.
Matokeo ya wabunge hayajatangazwa bado lakini yanatarajiwa kukaribiana pia.
Awali polisi walisema kulikuwa na kesi 21 wakati wa uchaguzi huo zinazohusiana na ghasia tangu Jumatatu, huku watu watano wakiwa wamefariki
Huu ni uchaguzi wanane wa urais tangu katiba ilivyoandikwa mwaka 1992.
Sent using
Jamii Forums mobile app