Tumpigie kura Rais Magufuli kuwa "Best Political Leader of the Year 2020"

Tumpigie kura Rais Magufuli kuwa "Best Political Leader of the Year 2020"

Huyo nana si ndio huyu???
Screenshot_20210106-155327.png
 
Baadhi ya Vijana usipokuwa na msimamo na utadondoka kwa kila jambo.

Inakuaje mtu yupo kwenye chama cha upinzani then akajitoa kwenye chama hicho.

Sababu ya msingi ni kutokubaliana na Chama chake kwenda kukubali serikali ya Umoja wa kitaifa.

Kwa maana kwamba zoezi zima la Uchaguzi na kupata viongozi wa kutuongoza halikuwa wazi na la haki.

Hivyo zao zima la Uongozi halikubeba msingi wa uadilifu.

Sasa tukirudi kwenye mada, kijana huyo huyo aliekataa uovu anaanza kutetea misingi hii ya ouvu kwa kuhamasisha watu wamchague mtu na kumpa sifa za uongo ili mradi matakwa yake yatimie.

Ni jambo la kustaajabisha kwa mustakabali wa Taifa, tunatengeneza watu wanafiki wanafiki.
 
Shida ya hiyo award ni kipengele cha democrasia, yaani tuzo hiyo inatakiw iende kwa rais anayeamini katika utawala wa kidemokrasia na kuheshimu haki na uhuru wa watu, sasa je, tunachagua aliye bora kuliko mwingine au tunachagua mwenye sifa hizo? Kwani ni lazima tuzo hiyo itolewe mwaka huu?[emoji848]
 
Huko ghana kuna platform moja ambayo ni kama jamii forum huku. Nao wanasema bora wampe shetani kula kuliko huyo mzee akufoh. So mnayosema hapa wala hayashtui.
Tunachokisema hapa ni kuwa bora tumchague shetani tusiyemjua kuliko kumchagua shetani tunayemjua!

Wengi wa Watanzania walio piga kura sio kwamba wanamjua Nana,ila wanamjua Magufuli!Kwa mtazamo huo,hicho ni kipimo kibaya sana kwa namna mtu asivyokupenda!

Kura yangu kwa Nana,maana JPM namfahamu kwenye demokrasia na uhuru wa kujieleza na masuala ya utawala bora si mtu sahihi!
Awamu yake wananchi wamepata mateso sana,hasa wanaomkosoa!Kubambikiziwa kesi,kuwekwa mahabusu,kupigwa risasi na kutekwa vilitawala sana miaka 5 ya JPM!
So siwezi kumchagua mtu mwenye sifa hizo,heri nichague nisiyemjua!
 
Tija ya jumla ndio kipimo sahihi,
Kuwasomesha namba watu wako Ili wawe masikini ili uwatawale unakuaje bora.Bora ni kuwainua wa chini wapande juu na sio kuwashusha watu chini
Chadema ndio wanataka kuwashusha chini akina Halima James Mdee badala ya kuwainua wakawatetee wananchi bungeni!
 
Tunachokisema hapa ni kuwa bora tumchague shetani tusiyemjua kuliko kumchagua shetani tunayemjua!Wengi wa Watanzania walio piga kura sio kwamba wanamjua Nana,ila wanamjua Magufuli!Kwa mtazamo huo,hicho ni kipimo kibaya sana kwa namna mtu asivyokupenda!
Kura yangu kwa Nana,maana JPM namfahamu kwenye demokrasia na uhuru wa kujieleza na masuala ya utawala bora si mtu sahihi!
Awamu yake wananchi wamepata mateso sana,hasa wanaomkosoa!Kubambikiziwa kesi,kuwekwa mahabusu,kupigwa risasi na kutekwa vilitawala sana miaka 5 ya JPM!
So siwezi kumchagua mtu mwenye sifa hizo,heri nichague nisiyemjua!
Umeandika pumba tupu. Hivi una uhakika Magufuli ndio mtekaji???
Utaendelea kujifariji kwa comment kama hizi na member wenzio humu ndani usiporuhusu ufahamu wako ufanye kazi mpaka akili ikukae sawa.
 
Huu ni ukweli mchungu watu hawataki kuukubali
Watu wanafanya mzaha, viko vituo watendaji kata waliamrisha kura za lissu zipunguzwe apewe tanotano tu kila kituo.Kilichofanyika mwaka Jana ni uchafuzi mkuu Sio uchaguzi.Binafsi nimeshangaa jpm amekuwaje wa pili kwa afrika kwa utawala wa kidemokrasia?
 
Pascal yuko chuo kikuu cha Uongozi cha chama pale Kibaha ananolewa!

Ahamie kabisa na familia yake hapo chuoni wakati anaendelea na hiyo course. Kichekesho ni pale anapokwenda kusomea uongozi, kisha anategemea kura za kwenye mabeg ili apate uongozi!
 
Ukipata platform inahitaji dakika 5 za kuimba kwaya Ili kesho asubui uletewe v8 tumeona kwa mollel,bashe,mwigulu kwa uchache.Pasco ana cv zote ikiwemo kubebwa na kabila lkn ateuliwi lile swali alilouliza day one ndo lilimuharibia
Lile swali naona Jiwe alili mind vibaya sana,ndiyo maana Pascally uteuzi atausikia kwenye uhuru na mzalendo
 
Back
Top Bottom