Nimeamua kuandika ili wananchi tujue ya kuwa hata baadhi ya watunga sheria na pia ni viongozi wa dini hawajui kinachoendelea duniani.Huyu Mbunge (Askofu )wa jimbo la Kawe ETI anaona chanjo vaccine ya corona ni upuuzi.Labda hana kitu kinachoitwa BRAIN ana maji kichwani.Dunia nzima inagombania chanjo hiyo ya ugonjwa hatari wa corona.Tayari ukiachilia nchi zilizoendelea kama Uingereza tayari asilimia 99 ya watu wanaoishi washachanjwa,Nchi za Afrika kama Ghana,Kenya,Rwanda wanaendelea na zoezi hilo.Huyu Mheshimiwa akatembelee hospitali za Dar tu akaone zilivyofurika.Wakati wa awamu ya tano tulikuwa tunaambiwa ni ugonjwa wa kushindwa kupumua.Sasa awamu ya sita kwa kufuata ushauri wa WHO sijui kama anajua kirefu chake imeamua kufuata kwa manufaa ya wananchi na wageni.India watu kwa mamia wanateketea vivyo hivyo Brazil,Afrika ya Kusini baada ya kuumizwa sana na hatua za kuuzuia ugonjwa huu sasa ni afadhali kwani tayari nao wanachanja.wameshusha hadi grade 1.Sisi tumesaidiwa sana na nchi jirani kufunga mipaka yake vingenevyo Askofu sijui angekimbilia wapi.Uchumi wetu umedondoka anajua hilo?Watalii hasa Warusi waliokuwa wanajazana Zanzibar wamekimbia,wa Serengeti hawapo kabisa kisa washaambiwa Tanzania kuna Corona na serikali inaficha ukweli.wawekezaji nao hawaonekani kutokana na uoga wa corona na ukandamizaji wa kodi,na utaifishaji wa mali.analijua hilo?Dada Mdee mpe Elimu kidogo Mh Askofu hapo Bungeni.Tanzania sio kijiji.Mwenzio akinyolewa wewe tia maji.Tukiwasikiliza akina Askofu Gwajima Hakutakalika nchini.Serikali iache kusikiliza upuuzi wa akina Askofu Gwajima.#Kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania #Kazi iendelee.