#COVID19 Tumpuuze Askofu Gwajima kuhusu Chanjo ya Corona

#COVID19 Tumpuuze Askofu Gwajima kuhusu Chanjo ya Corona

Mars 12

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2021
Posts
221
Reaction score
349
Nimeamua kuandika ili wananchi tujue ya kuwa hata baadhi ya watunga sheria na pia ni viongozi wa dini hawajui kinachoendelea duniani.

Huyu Mbunge (Askofu )wa jimbo la Kawe ETI anaona chanjo vaccine ya corona ni upuuzi.Labda hana kitu kinachoitwa BRAIN ana maji kichwani. Dunia nzima inagombania chanjo hiyo ya ugonjwa hatari wa corona. Tayari ukiachilia nchi zilizoendelea kama Uingereza tayari asilimia 99 ya watu wanaoishi washachanjwa, Nchi za Afrika kama Ghana, Kenya, Rwanda wanaendelea na zoezi hilo.

Huyu Mheshimiwa akatembelee hospitali za Dar tu akaone zilivyofurika. Wakati wa awamu ya tano tulikuwa tunaambiwa ni ugonjwa wa kushindwa kupumua.

Sasa awamu ya sita kwa kufuata ushauri wa WHO sijui kama anajua kirefu chake imeamua kufuata kwa manufaa ya wananchi na wageni. India watu kwa mamia wanateketea vivyo hivyo Brazil, Afrika ya Kusini baada ya kuumizwa sana na hatua za kuuzuia ugonjwa huu sasa ni afadhali kwani tayari nao wanachanja. Wameshusha hadi grade 1.

Sisi tumesaidiwa sana na nchi jirani kufunga mipaka yake vingenevyo Askofu sijui angekimbilia wapi.Uchumi wetu umedondoka anajua hilo? Watalii hasa Warusi waliokuwa wanajazana Zanzibar wamekimbia wa Serengeti hawapo kabisa kisa washaambiwa Tanzania kuna Corona na serikali inaficha ukweli.wawekezaji nao hawaonekani kutokana na uoga wa corona na ukandamizaji wa kodi na utaifishaji wa mali.analijua hilo? Dada Mdee mpe Elimu kidogo Mh Askofu hapo Bungeni.

Tanzania sio kijiji.Mwenzio akinyolewa wewe tia maji.Tukiwasikiliza akina Askofu Gwajima Hakutakalika nchini. Serikali iache kusikiliza upuuzi wa akina Askofu Gwajima.

#Kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

#Kazi iendelee.

Soma: Askofu Gwajima: Ni ujinga kuruhusu Taifa zima kuwa 'experiment' kwa sababu tuna haraka ya Corona
 
Kuna mwaka ilizuka homa ya dengue.

Ikasumbua kwelikweli, kuna watu maarufu tukawapoteza na wengine wakalazwa kisha serikali ikaweka wazi kwamba ikikupata popote ulipo kbla ya hospitali ukihisi dalili tu anza kunywa maji kwa wingi na Panadol.

Kisha audio klipu ya Gwajima ikasambaa kwa kasi akisema hakuna ugonjwa wa homa ya dengue, ugonjwa gani unawapata watu maarufu pekee? Ugonjwa gani unaoua dawa yake panadol? Hakuna huo ugonjwa ni danganya toto ya serikali.

Mlitarajia katika hili awe na msimamo gani? Yaani acha kwamba ameunga mkono juhudi, kwa maoni yake ya tangu enzi za dengue unadhani sasa hivi angesema nini?
 
images (13).jpeg
Karma itawafikia mmoja mmoja hivi ndivyo aliingia madarakani ! Unatarajia aongee nini?

Umesahau yule mzee kipindi cha kampeni alivyomuuliza swali kuhusu bei ya sukari na alivyokosa majibu hadi kipara kikatiririsha jasho?
 
Mimi Naona hujajibu hoja,ame-quote data halali kabisa,hivi unavocheza na DNA na mRNA Unajua madhara yake mbeleni...Unajua kitu kinaitwa 'autism',hii kitu watoto wengi uzunguni miaka ya karibuni wanazaliwa nayo,na there is a strong link na vaccinations walizopitia wazazi wao,hata babu na bibi zao..Hebu tuache siasa ktk kila kitu..

FDA na CDC wanasema chanjo hizi zipo kwenye trial mpka 2023,kwanini tusisubiri wamalize majaribio yao...
 
Kuna mwaka ilizuka homa ya dengue.

Ikasumbua kwelikweli, kuna watu maarufu tukawapoteza na wengine wakalazwa kisha serikali ikaweka wazi kwamba ikikupata popote ulipo kbla ya hospitali ukihisi dalili tu anza kunywa maji kwa wingi na panadol.

Kisha audio klipu ya Gwajima ikasambaa kwa kasi akisema hakuna ugonjwa wa homa ya dengue, ugonjwa gani unawapata watu maarufu pekee? Ugonjwa gani unaoua dawa yake panadol? Hakuna huo ugonjwa ni danganya toto ya serikali.

Mlitarajia katika hili awe na msimamo gani? Yaani acha kwamba ameunga mkono juhudi, kwa maoni yake ya tangu enzi za dengue unadhani sasa hivi angesema nini?
Ni tapeli hivyo ni lazima awe mambo ya kitapeli. Nawahurumia waumini wake anaowapora sadaka kila siku na kwenda kula na wanawake kwa kufanya ukahaba huku akijirekodi.
 
Huyu askofu ana akili kweli? Hajui kama 'wakomunist'na 'wajamaa' rafiki zetu vipenzi China na Urusi wana chanjo? Kama tatizo ni Ulaya kwa nini hajashauri tukazifate huko. Kama anakataa au tunakataa tukatae kwa sababu ya nyingine sio tu kwa sababu zinatoka Ulaya.

WHO iko chini ya influence ya China, ndio maana Trump alijitoa.

Twendeni kwa fact tuache mentality za kishamba, mbona boss wake wachina walikuja kumchanja kule kijijini
 
Kawe ni jimbo pekee lenye wabunge wawili. Kiongozi wa Covid19 a.k.a shangazi Halima na mzee wa video za kikubwa Sheikh Askofu Rashid a.k.a mfufuaji.
 
Huyu askofu ana akili kweli? Hajui kama 'wakomunist'na 'wajamaa' rafiki zetu vipenzi China na Urusi wana chanjo? Kama tatizo ni Ulaya kwa nini hajashauri tukazifate huko. Kama anakataa au tunakataa tukatae kwa sababu ya nyingine sio tu kwa sababu zinatoka Ulaya.

WHO iko chini ya influence ya China, ndio maana Trump alijitoa.

Twendeni kwa fact tuache mentality za kishamba, mbona boss wake wachina walikuja kumchanja kule kijijini
Umemsikiliza lakini?
 
Huyu ndiye yule askofu wa wajinga aliyekuwa akiwahamasisha wasukuma kwa kilugha wamsapoti dikteta aliyekwenda?!! Askofu huyu anaamini katika kufufua ndondocha na misukule lakini haamini korona inaua?!!!!
 
Back
Top Bottom