Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Hii ni katiba ya CHADEMA kila anayejiunga na chama hiki nikuwa amesoma ameikubali, na unapochukua fomu ya kugombea uongozi ni lazima unakuwa uneikubali kwanza Katiba ya Chama.
Sasa kelele za Lijualikali hazina maana zaidi ni propaganda za waliomrubuni asaliti chama tu na mkumbuke Lijualikali alianza jeuri na kupingana na Chadema baada tu ya kumuoa binti wa Job Ndugai, Yaani huyu ni mkwe halisi wa Spika wa Bunge, Nimshauri tu bado ni kijana mdogo, awe na akiba ya maneno, haijui kesho! Na kama amejiunga na ccm bila kusoma katiba ya chama hicho atajikuta mikononi mwa wasiojulikana siku za usoni kwakuwa huko huruhusiwa hata kujaribu tu kufikiria juu ya kumkosoa mwenyekiti au vyovyote vile ambavyo ndani ya Chdema unauhuru navyo. Sisi tunaipenda Katiba ya Chadema kwakuwa inatujali vijana tunapotaka kugombea ubunge, udiwani ambapo chama kinatoa support, Lakini chama chetu kinaweza kujiendesha vizuri hata ikiwa hakitakuwa na ruzuku ya kutosha.
Kwakumsaidia Lijualikali na wanaccm wengine, Ripoti ya CAG 2018/19 imetoa HATI SAFI kwa Chadema, hii inamaana kwamba hakuna huo upotevu wa bilioni 8 anaousema. Chama cha upinzani kupewa hati safi ndani ya utawala huu ni jambo linalitakiwa chama hicho kisiwe na kwere hata ya punje ya mchere, Sasa muulizeni Lijualikali na CAG nani anaakili? Zingatia mwaka huu wa hesabu za CAG chama anachokwenda Lijualikali cha CCM kimepewa HATI CHAFU.
Iko hoja inajirudiarudia mara kadhaa, na hata Lijualikali leo kaizungumza, kwamba hakupewa nafasi ya kusikilizwa, ama kujitetea kabla ya kufukuzwa. Hili Lijualikali na wabunge hawa wanapotosha umma, na wengi wa wananchi hawasomi katiba ya Chadema. Yeye Lijualikali na wenzake 8 chama kimewapa nafasi ya kujitetea, Wabunge wanne Rwakatare, Silinde, Komu, na Selasini ndio wamefukuzwa direct kwakutumia kifungu cha katiba kinachotoa mamlaka kwa CC kufukuzwa bila kusubiri waangushe Chama. Atekeleze agizo la chama kujitetea asilete uongo.
Chadema inaendeshwa kwa misingi ya katiba, si Mbowe, Lissu, Mnyika wala yoyote kwamba ndie mwenye uamuzi. Uamuzi wowote katika taasisi hii ni uamuzi wa kikatiba.
Wasome Katiba ya Chadema ya 2006 Toleo la 2019, Ibara ya 6.5.1(d) kuhusu mamlaka ya Kamati Kuu kuamua jambo la dharura kwa maslahi ya chama.
Jambo la dharula linaamliwa bila kusubiri mtu anayehatarisha maslahi ya chama asikilizwe.
Niwakumbushe wabunge hawa, walipoamua kurubunika walitakiwa kujiridhisha kuwa wanakinga madhubuti. Taasisi ni kubwa kuliko mtu yoyote.
Na Yericko Nyerere