Tumsadie Lijualikali na wengine kuzijua Katiba za Vyama vya Siasa

Tumsadie Lijualikali na wengine kuzijua Katiba za Vyama vya Siasa

Lakini CDM mfikiri zaidi namna ya chama kufanya kazi na wabunge wake, suala la mwenyekiti wa chama kuwa pia KUB nadhani linaleta mkanganyiko wa kuadmnister cacus ya chama
usiingie kwenye mtego , soma katiba ya Chadema
 
Katika suala hili nadhani umefika wakati sana chama kwa maana ya Viongozi wake wakuu wakalitolea ufafanuzi wa kina tena bila kuacha alama yenye mashaka yoyote suala la matumizi ya RUZUKU na michango ya Wabunge namna ilivyotumika na mpaka sana au muda tuhuma hizi zilizotolewa BUNGENI chama wana akiba kiasi gani.

Ikiwa wabunge walichangia chama nafikiri si kosa lakini kama yapo matumizi ya hovyo kama alivyosema Mbunge kwa hakika anguko kubwa linakuja ingawa si kitu ambacho ningependa kukiona tena katika uhai wangu.

NCCR walituangusha sana waTanzania kipindi kileeee,baada ya kushindwa kutoa upinzani wa maana tulikuja kushuhudia viwanda na makampuni ya umma yakiuzwa kwa bei ya kutupwa kwasababu hapakuwa tena na sauti ya kuusemea umma.Ni vyema Mwenyekiti pamoja na team yake wakaachana na suala la CORONA kwakuwa tayari wananchi wengi wanaona serekali ipo sahihi.
 
Pia ukimaliza tuwasaidie chadema na wengine waijue katiba ya Tanzania na wakubal kua tume ya uchaguz ni huru kulingana na katiba yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Katiba sio msaafu wewe.. ujanjaujanja una mwisho mnaiba kura kibwege kama mnavyofanya.. Mwaka huuTrump atakuja kumaliza hasira za covid 19 kwenu[ref; ‎Koudou Laurent Gbagbo]
 
Yeriko nawewe waoneeni huruma wabunge wachadema.wanachangia fedha kwa hiari yao kwenye fixed acc sasa huko kwenye hiyo akaunti cag inamhusu nini.maana hizo sio pesa za serikali.wacha kutetea huozo mbunge hadi kalia.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Juakali ...amepoteza mwelekeo, naiona CCM ikikosa majimbo kwa upuuzi wakuwaweka wapinzani kugombea ubunge nakuwatema wafia chama wa CCM
2020 hii Chadema kutoboa ni ngumu sana kwa raisi huyu aliyepo,mkumbuke huyu sio JK.Watasimamishwa hao unaowaona wapuuzi sasa na watatoboa vilevile labda kama kuna tume nyingine ya uchaguzi Octoba sio mbali sana tusubiri na mungu atupe uzima
 
Tatizo Yericko mnajiona nyie ni bora kuliko vyama vyote nchi hii,watimueni wote tuu hao mnaoona wasaliti.Hii ni duru la mwisho kama ataikosa fursa ya kisiasa kupitia Chadema watapata kupitia vyama vingine.Na msiwaone wasaliti wakihamia vyama vingine.Kabla ya CDM kulikuwa na NCCR ilikuwa juu baadae ikaja CUF.Na baada ya uchaguzi mshingae kurudi kule mlikokuwa zamani.
 
Asante Yeriko kwa ufafanuzi, CDM mnapaswa kurusha posta ndogo vifungu katiba vinavyoipa maamlaka kamati kuu kuwafuta uanachama kwa dharula penye ushahidi hujuma kwa chama.
Lijuakali kali pia hongera zake katumia muda wake vizuri leo kupata huruma ya CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii mada ungeiacha tu wewe ni mtu mwenye heshima zako ... umeona hilo la katiba na hela wanazochukuliwa kila mwezi na hawajui ziendako nalo pia lipo kwenye hiyo katiba ?.
 
Kifungu ulichokinukuu kwa kuweka mabano kinazungumzia kumsimamisha sio kumfukuza. Sasa kama nyinyi wenyewe viongozi hamuielewi katiba yenu Msajili atawasaidia kuielewa.
 
Ndugu Yeriko naomba uniambie katika kifungu hivho wamesema watachangia kutokana na psho za kibunge, je mshahara ni posho za kibunge?
Je posho za kibunge kuna kiwango kamili anachopata au zinatokana na majukumu ya mbunge afanyapo kazi za bunge?
Kiwango kamili kinachokatwa kwa wabunge huwa kinatokana na posho au mshahara?
Yeriko naomba urudi hapa kisha utupe majibu.
 
Mnatumia nguvu nyingi kuhalalisha uozo wa Kaka wa Hai lakini siku zote unafiki na uongo haujifichi milele.

Pale alipo hana dola lakini anataka anyenyekewe vipi kama angekuwa na dola na mamlaka?.

Mnazidi kupoteza muelekeo kila kukicha na msipokuwa waangalifu mnakwenda kupotea mazima.
 
Back
Top Bottom