Tumsaidie Rais Samia kuzifuta Tozo na Kodi za dhuluma

Tumsaidie Rais Samia kuzifuta Tozo na Kodi za dhuluma

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Hapa Mama itabidi atuelewe tu kuwa tumeamua hatimaye kumsaidia kwani hao waliomzunguka hawamsaidii.

IMG_20210715_213635_704.jpg


Kodi na tozo za dhuluma hazikubaliki. Hivyo:

1. Tunasimama kabisa kutumia miamala ya simu kutumiana pesa kwa siku 3.
2. Baada ya hapo tathmini itafuata ya nini zaidi.

Kutoka kwa Mama tutategemea kusikia:

1. Hatua anazochukua kupata kodi halali tokea kwa vigogo wote.
2. Hatua anazochukua kutokana na ripoti za CAG.
3. Hatua anazochukua kudhihibiti matumizi ya serikali zikiwamo takrima za magari na majumba wanazopeana.
4. Hatua anazochukua kuhusiana na mashirika yanayozalisha hasara kila uchao.

Wametufikisha mahali ambapo kwa hakika hatuna njia nyingine ila sasa kuwataka kuziondosha kero hizi kwa vitendo.

Kwa pamoja tunaweza.

Ninawasilisha.
 
Hata wabanwe vipi hawawezi kupunguza matumizi yao, kama wale wabunge kule bungeni ndio wahujumu uchumi kabisa, na chanzo cha umasikini wa hili taifa.

Kutaka walipe kodi halali si takwa nje ya uwezo wetu.

Tuanzie hapa hakuna mapambano wala marumbano.

Tusimame kufanya miamala kama hatua ya kwanza kwa siku 3 tu kuwapa "flavor that we mean business!"

Hili linawezekana na bila gharama kubwa.
 
Usiwe na matumaini na hawa watu, manake aliyeondoka ni JPM waliobaki ni wale wale na usitegemee maajabu yeyote, ilani ni ile ile.

Kusitisha kufanya miamala kama njia ya kwanza kuwataka kuzifuta si kuwa na matumaini na mtu.

Something is better than nothing.
 
Titalipa kodi hadi ti....
  • Tozo la kuuza samaki
  • Tozo la kutuma muamala
  • Tozo la kupokea muamala
  • Tozo la wakala wa simu kukupa muamala wako
  • Tozo la kununua mafuta ya gari Tanroads warekebishe barabara
  • Tozo kwenye mafuta kujenga barabara vijijini
  • Tozo la kununua vocha ya simu
  • Tozo la mwenye nyumba kupitia luku
  • Tozo la SGR ukiingiza gari
Ngoja nasikia ku... nitarudi kumalizia maana siku hizi tinalipa kodi hadi tinaku... kila wakati
 
Kama tulimsaidia mapema Sana awaondoe sumu zote zilizoathirika na awamu pendwa watamhujumu na asuke safu yake mpya akusikia akawakumbatia sisi tumsaidije sasa zaidi ya kumsubiria kwenye sanduku la kura.

Ngoja wamuharibie,kina madilu wapo kisiasa zaidi udereva wanautaka.
 
Kwa maisha haya inawezekana anguko la ccm linakaribiaa na sio kwamba chadema watachukua nchi hapana kwa sababu wanasiasa wote cmm, CHADEMA, ACT, NCCR, nk hii nchi wanaifanya deal shamba la bibi.. mfano anglia awamu ya tatu ufisadi ulikuwepo kimya kimya. awamu ya nne ulikuwepo wazi wazi Richmond nk.

Awamu ya tano ubabe na ufisadi wa kimya kimya riport ya bot ilisomwa kimya kimya. Awamu hii ya Sita atujui mwisho wetu na picha lishaanza Je tutafika sisi Watanzania wenyewe kipato cha chini. Jibu wanasiasa wote wapiga deal.

CHADEMA, ACT, NCCR. Wanachotaka kwenye katiba mpya ni Masirahi yao wanachotaka kumpunguzia raisi mamlaka tu. Wanasiasa ndio wanao tukwamisha
 
Uongo!
Zile tozo za "airtime" za NDUGULILE ni kazi ya magufuli.

Jiwe angekuwepo saivi kupiga cm ingekuwa luxury🙄

Vigogo wasiolipa kodi walikuwa Po hata kwa mwendazake. Huko kulikuwa na pesa za kununua wapinzani pia. Kwa CAG 1.5tr hakuna ajuaye zilikwenda wapi.

Takrima za majumba ya mabilioni tulizisikia kuanzia kwake.

Hakuna miamala hapa!
 
Kwa maisha haya inawezekana anguko la ccm linakaribiaa na sio kwamba chadema watachukua nchi hapana kwa sababu wanasiasa wote cmm, cdm, act, nccr, nk hii nchi wanaifanya deal shamba la bibi....
Huelewi unachosema zaidi ya kubwabwaja!
 
Back
Top Bottom