Tumsaidie Rais Samia kuzifuta Tozo na Kodi za dhuluma

Tumsaidie Rais Samia kuzifuta Tozo na Kodi za dhuluma

Sijawahi kuona popote duniani transaction moja iwe na tozo tatu tofauti.. Kwa umoja wetu tukiamua tunaweza

Kuna mengi wanafanya hayakubaliki.

Tunayo nafasi ya kuwaonyesha na kuyakataa kwa vitendo.

Hili nguvu moja siku 3 tu. Mbona wanabadili uelekeo?
 
Nyie ni wajinga Sana hivi mnadhani haya yote yanafanyika bila idhini ya raisi ?

Kwanini mnashindwa kusema kuwa huyu mama ni mzigo tu mnawapa lawama watu wengine wakati yeye ndio raisi.

Usiwahi sana kudhani wengine ni wajinga isipokuwa wewe.

Kiswahili ni kipana sana jombi. Hujawahi kuona mtu akisaidiwa kuondoka hata kama hajaaga?

Au nyie ni mpaka mtu aseme mtakavyo nyie? Rahisi zaidi si unaandika mwenyewe utakavyo?

Hiiiiii bagosha!
 
Hapa Mama itabidi atuelewe tu kuwa tumeamua hatimaye kumsaidia kwani hao waliomzunguka hawamsaidii.

View attachment 1855654

Kodi na tozo za dhuluma hazikubaliki. Hivyo:

1. Tunasimama kabisa kutumia miamala ya simu kutumiana pesa kwa siku 3.
2. Baada ya hapo tathmini itafuata ya nini zaidi.

Kutoka kwa Mama tutategemea kusikia:

1. Hatua anazochukua kupata kodi halali tokea kwa vigogo wote.
2. Hatua anazochukua kutokana na ripoti za CAG.
3. Hatua anazochukua kudhihibiti matumizi ya serikali zikiwamo takrima za magari na majumba wanazopeana.
4. Hatua anazochukua kuhusiana na mashirika yanayozalisha hasara kila uchao.

Wametufikisha mahali ambapo kwa hakika hatuna njia nyingine ila sasa kuwataka kuziondosha kero hizi kwa vitendo.

Kwa pamoja tunaweza.

Ninawasilisha.
Huko hutasikia
 
Huko hutasikia

Kuweza kusikia kote mbona ni uamuzi wetu tu? Kama mwuuza samaki yuko radhi samaki waoze? Sembuse kufanya muamala ambao tunaweka na ya kutolea?

Siku 3 tu, ukisikia Mwigulu nje usiseme miye nabii.
 
Hakuna kitu mkuu
Kikiumana mwigulu atakuwa Mbagusiro. Yamewakuta kina Msabaha na wengi tu.

Tatizo letu ni kutaka matokeo bila jitihada.

Usiende kufanya muamala wewe, mimi, yule na wote kwa siku 3. Hilo huwezi utakwenda kupambana na Muroto wewe kudai katiba mpya? Au yale yale ya nyuma ya keyboard?

Nani unataka akapambane barabarani kama hata guts za kutotuma muamala tu huna?
 
Usiwe na matumaini na hawa watu, manake aliyeondoka ni JPM waliobaki ni wale wale na usitegemee maajabu yeyote, ilani ni ile ile.

Kwani mkuu ni suala la kuwa na matumaini na mtu. Hili ni suala la kupambana kupata tunachotaka.

Tunachotaka hakitakuja kama hisani.

Huo ndiyo ulio ukweli mchungu.
 
Back
Top Bottom