Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Amemaliza chuo kikuu ngazi ya Shahaada mathalani 2015. Amejitahidi kusaka ajira serikalini na kwenye sekta binafsi tangu wakati huo, mpaka sasa bila bila, na anaelekea kukosa sifa za kuajirika kwa mujibu wa sheria kutoka na kigezo cha umri na uzoefu.
Mambo ni mengi na ni Magumu, na muda ni mchache.
Uzuri wa kijana huyu, ni kwamba hajakata tamaa hata kidogo, ila anaelekea huko taratibu maana mvi zimemzonga hasa.
Na kinachomchochea kukata tamaa ni kwamba, anajiuliza hana hata ka plot au shamba, kijijini kwao wala mjini, hana mchumba wa uhakika wala hata mtoto wa kusingiziwa, faraja yake kwa muda mrefu huenda ni ilikua kujichua tu. Alikua na matumaini ya kupata ajira awe na kipato na mchumba mzuri pia.
Umri umesonga, fedha ngumu haoni cha kufanya, kodi ni shida, kula ni shida, anakwepa hata kushiriki mambo ya kijamii kama vile ndoa na misiba. Ni mnyonge sana hana ujasiri kabisa.
Kijana anasononeka mno, anajuta, ananung'unika na kujisemea mwenyewe moyoni alikosea wapi, mbona kama ni yeye pekeyake tu, anapitia masaibu haya.
Kijana anaona haya na aibu hata kurudi kijijini kwao kwenye maziwa na asali za kutupwa. Rika lake na wadogo zake wa shule, wameoa na kuolewa, wana nyumba nzuri, maisha mazuri, biashara kubwa, kipato kikubwa, wamezaa watoto wazuri, wakubwa wanawasomesha maeneo mbalimbali. Hili linampasua kichwa zaidi kijana huyu.
Kijana akitafakari hayo, moja haikai wala mbili haikai. Umri umesonga, mvi ndio kama zote, anaanza kuchuja na kukongoroka. Anahisi kama ana mkosi, hapendeki wala haitajiki tena kwenye jamii, roho ya kukata tamaa ina mnyemelea na kumkaribia zaidi....
Wapendwa maisha hayana Extra time.
Hebu tusaidiene, tuelimishane, tuelekezane, tupeane moyo na njia katika hili, tumkwamue kujana huyu mpendwa alipokwama.
Asipotee bali apate mwanga na Nuru ya kutoka kimaisha Salama.
Wasalam.