Tumshauri kijana huyu cha kufanya, muda bado upo

Tumshauri kijana huyu cha kufanya, muda bado upo

Nchi hii kubwa bado inahitaji nguvu kazi ya wasomi. Hata hivyo ajira inahitaji mtu mwenye ufahulu wa juu mwenye maharifa kiasi hata ukimfanyia interview utajua kuwa hiki ni kichwa. Sasa wengi wanaenda chuo wakishapata boom wanasahau kilichowapeleka na kuishia kupata GPA ya PASS Gentlemen! Sahau kuajiliwa! Komaa kitaa kamanda
Sawa Mywangu.
 
Shda ni pale mtu anaishii kwa kujifananisha na watu wengne ...kila mtu atapata alichoandikiwa... hata ukipora itapotea....subira ndoo kila ktu hata Reginald mengi alipata mapacha akiwa na miaka 70......calm down pray...socialize with pipo good things is coming tomorrow
Mawazo Uchwara ya kujifariji na kukwepa uhalisia
 
Juzi nikikuwa DIT pale jengo flani hivi refu sana nilienda kuwatafuta wanafunzi wenzangu kule juu,sasa siwafahamu,na mimi ndio nimeanza mwaka wa kwanza,nikwmuuliza dada flani,samahani unasoma kozi gani,akanijibu Mechanical,mwaka wa ngapi wa mwisho,anajibu kwa madaa kabisa yule kahapa nikasema kanajiona ,fresh street is waiting for you with joy
Mkuu wewe mbona umeenda kuanza mwaka wa kwanza, kisha unasema huyo sister "Street is waiting for her"

Je wewe mtaa haukusubiri au?
 
Amemaliza chuo kikuu ngazi ya Shahaada mathalani 2015. Amejitahidi kusaka ajira serikalini na kwenye sekta binafsi tangu wakati huo, mpaka sasa bila bila, na anaelekea kukosa sifa za kuajirika kwa mujibu wa sheria kutoka na kigezo cha umri na uzoefu.
Mambo ni mengi na ni Magumu, na muda ni mchache.

Uzuri wa kijana huyu, ni kwamba hajakata tamaa hata kidogo, ila anaelekea huko taratibu maana mvi zimemzonga hasa.

Na kinachomchochea kukata tamaa ni kwamba, anajiuliza hana hata ka plot au shamba, kijijini kwao wala mjini, hana mchumba wa uhakika wala hata mtoto wa kusingiziwa, faraja yake kwa muda mrefu huenda ni ilikua kujichua tu. Alikua na matumaini ya kupata ajira awe na kipato na mchumba mzuri pia.

Umri umesonga, fedha ngumu haoni cha kufanya, kodi ni shida, kula ni shida, anakwepa hata kushiriki mambo ya kijamii kama vile ndoa na misiba. Ni mnyonge sana hana ujasiri kabisa.

Kijana anasononeka mno, anajuta, ananung'unika na kujisemea mwenyewe moyoni alikosea wapi, mbona kama ni yeye pekeyake tu, anapitia masaibu haya.

Kijana anaona haya na aibu hata kurudi kijijini kwao kwenye maziwa na asali za kutupwa. Rika lake na wadogo zake wa shule, wameoa na kuolewa, wana nyumba nzuri, maisha mazuri, biashara kubwa, kipato kikubwa, wamezaa watoto wazuri, wakubwa wanawasomesha maeneo mbalimbali. Hili linampasua kichwa zaidi kijana huyu.

Kijana akitafakari hayo, moja haikai wala mbili haikai. Umri umesonga, mvi ndio kama zote, anaanza kuchuja na kukongoroka. Anahisi kama ana mkosi, hapendeki wala haitajiki tena kwenye jamii, roho ya kukata tamaa ina mnyemelea na kumkaribia zaidi....

Wapendwa maisha hayana Extra time.
Hebu tusaidiene, tuelimishane, tuelekezane, tupeane moyo na njia katika hili, tumkwamue kujana huyu mpendwa alipokwama.

Asipotee bali apate mwanga na Nuru ya kutoka kimaisha Salama.

Wasalam.
Tokea 2015 mpaka sasa kwavile hajafa njaa, maana yake hela anaingiza. Je, anafanya mishe gani kwa sasa?

Anaishi wapi?
 
Tokea 2015 mpaka sasa kwavile hajafa njaa, maana yake hela anaingiza. Je, anafanya mishe gani kwa sasa?

Anaishi wapi?
mathalani 2025.
It might also be before or after that yr, kijana yupo kitaa na mambo bado haisongi hata....
 
Nikipita maeneo ya vyuo vikuu i.e UDSM,TIA,SAUT etc nikaona wanafunzi wanaenda madarasi kusoma hua nasikitika Sana.

Yajayo hayatawafurahisha.
Kweli ni hatar sana yaan matumain hamna kabisa. Sasa tufanyeje maana hili tatizo linazidi kukua na limeshafika mpaka milangoni mwetu na kwingine limeshaingia sebulen kabisa. Linawapata wadogo zetu, wajomba zetu na linakuja kwa watoto wetu...jamaaan...
 
Sasa hapa ndio umejibu nini mkuu?. Msingi wa swali langu ungeweza kujibiwa bila hata kujua mwaka husika.
ok sawa, sory mkuu,
Mshauri basi jamaa afanyeje,
hana mishe tangu amalize chuo miaka ya nyuma huko na alikua anatumaini kuajiriwa lakina mpaka sasa bila bila, umri unaenda na muda unasonga pia
 
Back
Top Bottom