SoC03 Tumtafute Mungu sana pia tutafute pesa kwa bidii

SoC03 Tumtafute Mungu sana pia tutafute pesa kwa bidii

Stories of Change - 2023 Competition

Mkandarasi mdogo

New Member
Joined
Jun 1, 2023
Posts
2
Reaction score
4
MUOMBE MUNGU SANA TAFUTA PESA KWA BIDII:
ayo mengine ACHANA nayo kwanza. Maisha yamebadilika Sana, nakumbuka wakati na kua, nyumbani kwetu, kulikua na desturi kuwa siku ya juma pili huwezi kwenda kwa mkristo ukamkuta anafanya kazi ngumu kama vile kulima, kukata majani ya ng'ombe pia hata shunguli za ujenzi hazikufanyika biashara pia hazikufunguliwa.

Watu walikwenda kusaga jumamosi walifanya maandalizi yote kwaajili ya siku ya ibada, siku hiyo ya jumamosi.

Hata hivyo siku ya ibada, tulibandika makande ahsubui na kwenda ibadani, baada ya kutoka ibadan tunakuta chakula tayari ni kula tu na kupumzika hakuna kazi siku hiyo.

Tulipata muda wa kukaa na wazazi na saa ingine pia kuwatembelea wazee tukiwa pamoja na wazazi wetu, siku hiyo Basi hatakama ulifanya kosa huwezi adhibiwa ilikua ni siku tulivu. Ukiwa na redio yako ya kaseti utanunua betry unaweka kanda unasikiliza kwaya ya Rose Mhando na Bahati bukuku.

Ikifika jion tunajiandaa kwenda shule na wazazi wanaanza kupanga mipango ya jumatatu, mapambano yanaaza siku ya jumatatu yanaishia jumamosi.

Hii ilichangia zaidi kupunguza mmomonyoko wa maadili kwani unapo kaa na wanao inaweza kuchunguza na kujua ikiwa Kuna tabia zisizo faa wameiga na kuikemea Mara moja.

Hali imebadilika sana. Tofauti kubwa sasa hivi na kipindi hicho, watu ibadani wanakwenda tu kuonekana, heshima ya ibada hakuna tena , kitu cha kushangaza zaid nipale unakuta hata viongozi wa dini wamekua wa kivunja Sheria na kuruhusu watu kufanya kazi siku hiyo ya saba, kwasababu wameweka pesa mbele kuliko kutii neno la Mungu.

Nimepita maeneo mengi na kukuta makanisa yanajengwa siku ya jumapili, inakuaje kiongozi wadini unahubiri ndani nje fundi anagongagonga hii inatuletea utata Sana, hafadhali umkute muumini anafanya kazi siku hiyo kuliko kiongozi, maana msimamizi wa Sheria haruhusiwa kuvunja sheria.

I kumbuke amri ya Mungu ya tatu inasema ishike kitakatifu siku ya Mungu, siku hiyo nisiku ya kupumzika siku ya kustarehe, siku ya kutafakari ukuu wa Mungu. Siku hiyo unaweza kuitumia kukaa na watoto wako kufurahi nao, kujua changamoto wanazo pitia mashulen au majumbani ili kujipanga kuchukua hatua.

Kutafuta pesa ni kuzuri ila usisahau kumuomba Muumba wako, kama unahuzuria ibada nenda kaabudu kweli, usisikilize watu, najua Kuna Mambo yanakatisha tamaa ila kaza buti omba Sana.

Juzi nlihudhuria ibada ya mazishi, kwenye mazishi hayo nlijifunza kitu nligundua kuwa nitafute pesa kwa bidii huku nikimuomba Mungu. Baada ya mwili wa Marehem kufika tuliupokea na kuupeleka mahali palipo andaliwa kwaajili ya ibada hiyo, baada ya hapo utaratibu ulianza kwa kusomwa historia fupi ya marehem, niliisikiliza kwa Makin, marehem aliku afisa ugavi hospital ya mkoa wa simiu, marehemu aliacha wajane wanne na watoto watano, hili lilinifanya nianze kuwaza kwanini marehem aache wajane wa nne? Yeye ni mkristo na hakua na ndoa na hao wanawake hata mmoja wao.

Basi historia iliisha watu tukiwa na maswali mengi. Kwenye ibada waliuhudhuria viongozi wa kubwa wa dini, pamoja na wa serikali kutoka maeneo aliyowai kufanya kazi.

Alisimama mchungaji mkuu wa kanda, jina nimesahau na alianza kuhubiri, (nikisema tutafute hela muwe mnanielewa), alianza vizuri kwa kusoma neno linalo sema Heri wenye moyo safi maana hao watamuona Mungu. Aliendelea kuhubiri , alituchanganya zaidi pale alipo sema anazungumza na sisi ambao hatujafunga ndoa na tunaishi na wanawake akikemea vikali kitendo hicho na kusema kuwa "ukifa huna ndoa unaishi na mtoto wa watu wachungaji hatuji kukuzika utafukiwa tu hakutakua na ibada" sasa hapo ndo nkajua kumbe ukiwa na pesa, ukifa ww utazikwa vizuri na ibada itafanyika, ila kama huna hela ww funga tu ndoa maana kweli hawaji kukusalia. Nahii nimeishuhudia Mara nyingi watu wakizikwa bila kuombewa. Kwaiyo lile jopo la wachungaji walikuja kwasababu marehem alikua mtumishi na alikua na nafasi nzuri kazin, kwaiyo walisahau kuwa marehem hakua na ndoa, embu tujiulize Marehem asingekua na cheo je wangemuombea? Je! angezikwa tu? Au walitumia kigezo gani kuja kumzika? Basi jibu linabaki tu kuwa tutafuta pesa kwa bidii.

Lakin hebu tujiulize je! Wale wajane Wana haki ghani? watawezaje kuwalea wale watoto na je watoto wanahaki ghani kwenye famili, kwa ninavyojua mimi ni kwamba mtoto wa nje ya ndoa hana urithi kwenye familia kisheria.

Kwa mawazo yangu Mimi naona dini sasa hivi ni biashara wala hatuabudu kama zamani, kashfa kwa viongozi wa dini zimekithiri Mara huku padri kafumaniwa na mke wa mtu, huku mchungaji anaimba singeli kanisan, inakatisha tamaa hasa ukiwaza mchungaji huyohuyo aliye mtia muumini mimba ndo ankuwekea mikono kichwani anakuombea. Bora umuombe tu Mungu kivyako usimtegemee mtu akuombee.

Unashangaa unaenda kanisani mchungaji pekee ndo mwenye gari alafu unaambiwa njoo uchukue upako uwe tajiri ndugu zangu uo ni utapeli kama mchungaji angekua anauwezo wa kutoa utajiri basi angejitajirisha yeye kwanza, asinge taka sadaka na kufanya biashara ibadani. Nasema Tutafuta pesa tuache kuanguka kanisani wakati wa maombi.

Shetani ameliteka kanisa, dini zimekua za kitapeli wachungaji wanaenda kinyume namaandiko, wanatafuta pesa na sio kufundisha, ndio mmomonyoko wa maadili unaongezeka, kama ukiwa na pesa basi unanunua hadi viongozi wa dini, nasema tutafute tu pesa.

Ukiwa busy kutafuta pesa hata huwezi kufanya Mambo ya ajabu kwenye jamii, pia huwezi jikuta unaingia kwenye matatizo, na utaheshimika, ila kama huna pesa ndugu yangu hatakama unahudhuria ibadani, na ndoa umefunga mchungaji anaweza akashindwa kuja kukufanyia ibada kwasababu akija hapati kitu hivyo anaweza kupata zarura, we Muombe tu Mungu.

Muombe Mungu wako Sana utapata maisha mazuri, Mtu anayemtumikia Mungu huishi kwa raha Sana hana wasiwasi kwasababu anaamini Mungu yupo, kinachotakiwa niimani tu.

Mwisho nimalizie ushauri kwa viongozi wa dini , fundisheni ukweli tendeni haki, acheni kuitukuza pesa, Hubiri Maandiko matakatifu, muwe mstari wa mbele kutuonyesha njia sahii,mnatupotosha hatujui wapi sahihi pakuelekea.

Ikiwa Mwalimu aingii darasani kwa kutumia mlango akaingia kwa dirshani hata wanafunzi nao watafata tu. Hivyo viongozi wa dini ni waalim wakiendelea na tabia zisizo faa basi hatuwezi kudhibiti mmomonyoko wa maadili.
Tumuombe Mungu kwa pamoja awaokoe viongozi wa dini awalinde na majaribu ya shetani ili na sis tusalimike.

TUMUOMBE MUNGU HIZI NI NYAKATI ZA MWISHO.
 
Upvote 4
Back
Top Bottom