Kadogosa amekubaliana na Kigwangalla kuwa kila behewa moja wamenunua kwa TSh 2 billion kwani behewa 59 wamezinunua kwa USD 59.6 million sawa na TSh 120 billion.
Je, yupo anayejua bei ya behewa jipya la electric sgr linauzwa bei gani huko duniani na hilo used linauzwa ngapi? Hii inaweza kutusaidia kujua kama hayo mabehewa tuliyonunua ni used au ni mapya au zaidi ya mapya?
Katika pekua pekua yangu nimekuta kitu hiki India kwamba bei ya behewa moja la axle 25 axle load linauzwa Rs 2.5 million sawa na TSh 71 million. Inawezekana bei hii ni ya mabehewa yasiyo ya kisasa ya umeme kama yalivyo yetu na pia labda ni used. Sawa, hata kama hayo waliyonunua wahindi si ya kisasa na ni used, tofauti ya bei haiwezi kuwa kubwa kiasi hiki: kutoka TSh 71 million hadi 2 billion!
With 100% electrification, poised to become a net zero carbon emitter by 2030
wap-business--standard-com.cdn.ampproject.org