Rais aliposema tunanunua behewa used alikuwa sahihi, ni kweli toka 2020 trc iliingia mkataba na kampuni ya eurowagon wa kuleta mabehewa used toka Ujerumani, ukatokea mgogoro wa kimkataba na kuuvunja.
Wakati huo huo trc waliingia mkataba na kampuni nyingine ya Kikorea kununua mabehewa mapya, mwezi uliopita PM Majaliwa alienda Korea na kukagua maendelea ya matengenezo ya mabehewa hayo mapya, akasema kazi inaenda vizuri na baadhi yako tayari, ndiyo haya yamepokelewa hivi karibuni.
Kwa maana hiyo Masanja aliyesema mabehewa ni mapya yupo sahihi, na mama aliyesema tunanunua mtumba(ya ghorofa) yupo sahihi pia, hizo ni order mbili tofauti