Tuna cha kujifunza na Uchaguzi wa Marekani?

Tuna cha kujifunza na Uchaguzi wa Marekani?

Chakujifunza ni kuelewa tu,wanasiasa wote duniani wanatofauti majina tu lakini vivuli vyao na matendo yao ni siri zao ambazo zinafanana kisirisiri
 
Sina uhakika kama huko Marekani zimeshikwa sandarusi pamoja na viroba vya kura fake!

Kwetu mamboleo hudai walikuwa wasafiri na mizigo yao. Wengine hukimbia na mabox ya kura.

Huko ndiko kwetu ambako milango ipo Ila hata madirishani watu hupita.
 
Mkuu, mbona hawajatangaza mshindi mpaka sasa? Kwenye uchaguzi wa mwaka 2000 walichakachua, kwa hiyo haitashangaza wakichakachua tena!

Safari hii kuna kura nyingi za njia ya barua ambazo Posta ya huko imechelewa kuwasilisha - yale mambo ya deportivo:


Kila kura ni shuruti ihesabiwe kupata matokeo. Kwetu vice versa ni sahihi!
 
Hapo Magufuli anamwona Trump boonge la zuzu kulalamika huku yeye ndiye Rais!!
Waafrika tulikosea sana kuwaondoa mapema wakoloni wazungu! Tungewaacha kwanza watusindikize!

Afrika kuta tu jina la rais kama hivi Magufuliiii...wanaona unastahili kunyongwa!
Eti bonge la zuzu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mabibi na mabwana, elimu haina mwisho. Je, tuna cha kujifunza kutoka kwao waliotutangualia? Au ni yale yale ya ukichwa ngumu kama mawe kuwa tunajua kila kitu?...
Screenshot_20201104-220128.png
 
Mkuu ninayo katiba ya Marekani waliyoiandaa 1789 miaka michache baada ya kupata uhuru wao, katiba ile ni bora na inayotoa majibu mara 100 ziadi ya katiba yetu ya sasa. Cha kujiuliza ilikuaje watu watengeneze katiba 1790 na mpaka sasa wameifanyia marekebisho madogo sana lakini sisi tokea 1977 mpaka leo bado katiba yetu imeacha maswali mengi bila majibu?

Uchaguzi wa kwanza wa Marekani ulikua na matokeo mazuri na ya uwazi zaidi ya uchaguzi wetu wa leo 2020, miaka karibia 60+ tokea tupate uhuru. Je shida ni kua hatujifunzi mazuri kutoka kwa waliotangulia au akili zetu ndiyo finyu?
Mwaka huu imetokea wamepata Rais "anaeogopa" kuibiwa kura.

Wakati huo huo utandawazi umetupa kujua mkuu wa Shirika la Posta USPS amehusika na upotevu wa kura za njia ya posta.
Ni Marekani hawa hawa 2000 George W. Bush alishinda kwa ushindi wa mezani mahakamani baada ya nduguye Gov. Jeb Bush kuhusika na "mipango mipango" ya kura za Florida.

Nadhani, kama kuna upekuzi wa kina utafanyika, katiba yao nayo sio kwamba iko perfect kiviilee.

Kumbuka 2016 kulikuwa na voters suppression iliyofanywa na wahavidhina wa KKK dhidi ya weusi na latino.
 
Trump analalamika kuwa ni kama kuna namna fulani anataka kudhulumiwa kura. Sasa jiulize kwa teknolojia yao na ubobezi kwenye mambo ya kupiga kura, malalamiko haya yanatoa somo gani !?

@TUJITEGEMEE
 
Teknolojia ya habari na mawasiliano inawaumbua sana viranja wa dunia
 
Matokeo ya uchaguzi wetu yalitoka mapema zaidi kuliko yao; wanachelewesha kutoa matokeo sijui wanataka kuchakachua 😂😂😂

..Tanzania waliopiga kura walikuwa 15 million. USA waliopiga kura wanakadiriwa kuwa 150+ million.

..Janga la covid-19 huko US limesababisha baadhi watume kura zao kwa njia ya posta, na wachache wapige kura ya moja kwa moja.

..hali hiyo ndiyo imesababisha matokeo ya uchaguzi huu yachelewe kutoka. kama umefuatilia chaguzi zilizopita, kwa mfano 2016, mshindi alijulikana baada ya masaa machache toka wamalize kupiga kura.
 
Mabibi na mabwana, elimu haina mwisho. Je, tuna cha kujifunza kutoka kwao waliotutangualia? Au ni yale yale ya ukichwa ngumu kama mawe kuwa tunajua kila kitu?

Mema waliyonayo wamarekani leo hayakuja kama mvua. Yalipiganiwa na hata damu kumwagika. Sembuse kukaa mahabusu au hata kufungwa jela?

Kwani kwao TISS, NEC, ZEC au police wa huko hawapo?

Kweli hatuwezi fanya uchaguzi tukauhitimisha kwa kupongezana? Kwamba hata CUF na hata NCCR nao wanalalamika na bado hatuna sababu za kujiuliza? Dhahiri tutakuwa na matatizo.

Madai ya haki katika chaguzi yanapaswa kuwa yetu sote wakiwamo Magufuli, na hata bwana Kaijage. Nani aijuaye kesho?

Kesho thabiti ni Ile inayotokana na leo thabiti kwa mujibu wa katiba na si vinginevyo.
Yapo mengi ya kujifunza sisi kama watanzania kwaajili ya chaguzi zijazo:
1. Kura za mapema ni halali ili kupunguza mlundikano wa wapiga kura vituoni. Mfano Marekani kura za mapema zilianza Septemba, nasi tujifunze ili makundi maalum kama wazee, wafanyabiashara, walemavu, wanawake, maafisa wa Tume, mawakala wa vyama, wagombea na vyombo vya ulinzi wapige kura mwezi mmoja kabla.
2. Sio kila mpiga kura anapaswa kuamua nani awe Rais. Tumeona kule Marekani, Taifa lenye wapiga Kura zaidi ya Mil. 100, wanaoamua kiti cha URAIS ni watu 58. Hii inaepusha waovu kuwezesha mwovu mwenzao kuingia Ikulu. Huku Tanzania tumewapa watanzania wote haki ya kuamua nani awe RAIS, kwa mtindo huu, mwaka huu Mabeberu na mashoga walitaka kutupandikizia RAIS. Tujifunze kutoka Marekani
Hayo yanatosha kwa sasa
 
Yapo mengi ya kujifunza sisi kama watanzania kwaajili ya chaguzi zijazo:
1. Kura za mapema ni halali ili kupunguza mlundikano wa wapiga kura vituoni. Mfano Marekani kura za mapema zilianza Septemba, nasi tujifunze ili makundi maalum kama wazee, wafanyabiashara, walemavu, wanawake, maafisa wa Tume, mawakala wa vyama, wagombea na vyombo vya ulinzi wapige kura mwezi mmoja kabla.
2. Sio kila mpiga kura anapaswa kuamua nani awe Rais. Tumeona kule Marekani, Taifa lenye wapiga Kura zaidi ya Mil. 100, wanaoamua kiti cha URAIS ni watu 58. Hii inaepusha waovu kuwezesha mwovu mwenzao kuingia Ikulu. Huku Tanzania tumewapa watanzania wote haki ya kuamua nani awe RAIS, kwa mtindo huu, mwaka huu Mabeberu na mashoga walitaka kutupandikizia RAIS. Tujifunze kutoka Marekani
Hayo yanatosha kwa sasa

Ni wazi kuwa huna ulichojifunza wewe na labda hata kwa chama unachowakilisha kwa mawazo yako.

Mafunzo na UCHAGUZI wa Marekani yako wazi mno lakini kama ilivyo kwa mwanafunzi utayari kujifunza ni suala la msingi. Ni kawaida kwa wasio tayari kujifunza kutumia chochote ili kujitafutia fursa zaidi za kuhalalisha ubinafsi wao.

Nikilinganisha na kile ulichoandika:

1. Marekani kuliko na tume huru ya UCHAGUZI, Uhuru kamili wa mihimili ya utawala yaani mahakama, bunge na executive (serikali); mipangilio yao ikiwamo ya uchaguzi ni ya uwazi ili kufanikisha matakwa halisi ya watu. Kwenye mustakabala wa chaguzi kura huwakilisha matakwa halisi ya wapiga kura ambako kila kura ni lazima ihesabiwe.

Tofauti na funzo la wazi lililopo hapo kama kawaida yenu, wewe na wenzio mmejikita kwenye kutafuta fursa zaidi za kupanua wigo ili kuhalalisha wizi zaidi wa kura.

Hivi kura za mapema za ZEC zilikuwa na tija ipi, iwapo waliopiga kura ya mapema za ZEC walirejea tena siku iliyofuata kwa ajili ya kura za kawaida za NEC?

Makwetu macho kumchuzi. Ujanja ujanja tu. Yaani wizi wizi tu.

2. Marekani kila kura inahesabiwa. Majimbo yanapewa uzito tofauti idadi ya watu jimboni ikihusishwa. Hii haina maana ni kura za John, Harry au Tom kwa majina au vyama vyao tu zenye kuamua mustakabala wa uongozi nchini humo.

Tofauti na funzo la wazi kuwa huko hakuna chama wala mtu aliye na hati miliki ya uongozi au mustakabala wa uongozi, unataka kulazimisha mustakabala wa uongozi ni wa kubumba bumba usiojali matakwa ya wapiga kura kama makwetu usizonjeni!?

Unathubutu kusema "mngepandikiziwa rais." Kwani nyinyi nani? mbona wengine sasa wanaona wamepandikiziwa rais ambaye hata ameivuruga nchi hii vilivyo kutoka katika misingi imara ya kidemokrasia iliyoachwa na mwalimu Nyerere (rip)?

Kuna habari kuwa huyu bwana ana asili tata na wala si msukuma kama anavyojinasibu.

Pana wengi wenye mtizamo kuwa pana mtu ambaye uadilifu wake pale ikulu siyo. Kwamba huenda tuna mwovu pale.

Aaminiwe nani kwenye tuhuma za kibaguzi baguzi, kiramli ramli nk, kama hizo? Nyinyi au hawa wengine na kwa vigezo vipi?

Mkuu nimeangalia hayo mawili tu, tokea katika uliyoandika. Ama kwa hakika wewe ni mmoja wa wale wanaodhani hawana cha kujifunza. Wanajua kila kitu.

Vichwa mawe hawawezi kujifunza hata kwa watu waliowatangulia mno! Watu kama nyie ni msiba kwa taifa hili.

Ungeeleweka tu mkuu kwa kuweka wazi ulichokuwa unakitafuta:

"Mmeona fursa zaidi mnazoweza kupotosha ili kuhalalisha wizi zaidi kwa mgongo wa kuwa mmejifunza sasa tokea Marekani."

Yote yana mwisho na mwisho huo hauko mbali!
 
Hakuna cha kijifunza... Wanasiasa wote ni wale wale...



Cc: mahondaw

Mkuu:

1. Wengine viroba hubebea maiti au kura za wizi.
2. Wengine huuwa wapinzani wao.
3. Wengine huzima mitandao.
4. Wengine ni mijizi.
5. Wengine wauwaji.
6. Wengine dhulumati.
7. Wengine hawafuati wala kuheshimu kati ba.
8. Wengine ni wabinafsi.
9. Wengine ni waroho wa madaraka.
10. Wengine wakabila.
11. Nk, nk.

Mandela (rip), Nyerere (rip) na hata Kikwette hawakuwa hivyo.
 
Mkuu:

1. Wengine viroba hubebea maiti au kura za wizi.
2. Wengine huuwa wapinzani wao.
3. Wengine huzima mitandao.
4. Wengine ni mijizi.
5. Wengine wauwaji.
6. Wengine dhulumati.
7. Wengine hawafuati wala kuheshimu kati ba.
8. Wengine ni wabinafsi.
9. Wengine ni waroho wa madaraka.
10. Wengine wakabila.
11. Nk, nk.

Mandela (rip), Nyerere (rip) na hata Kikwette hawakuwa hivyo.

Wanasiasa wote ni wauchu na waroho wa madaraka...



Cc: mahondaw
 
..Trump ambaye ni Raisi aliyeko madarakani analalamika.

..anadai atakwenda kushitaki ktk mahakama kuu ya Marekani.

..sasa unajiuliza, kwanini hatumii vyombo vya DOLA wakati yeye ni Amiri Jeshi Mkuu?

..tatizo la hapa kwetu malalamiko ni ya upande mmoja tu, wakati upande mwingine ukichekelea na kufurahi siku zote.

cc tindo
Kwahiyo Trump anazo power kama walizonazo marais wa africa ila hazitumii?
 
Back
Top Bottom