Tz mbongo
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 13,332
- 7,351
Nyerere alizowea kuishi kwa uongo.Nakazia: "Mandela (rip), Nyerere (rip) na hata Kikwette (kama mfano tu) hawakuwa hivyo."
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nyerere alizowea kuishi kwa uongo.Nakazia: "Mandela (rip), Nyerere (rip) na hata Kikwette (kama mfano tu) hawakuwa hivyo."
Hujaona wale waandamanaji wa TRUMP wa 'count all votes! Na kwingine 'stop the count!?Cha kujifunza ni kwamba kule Marekani mgombea anayeona hajatendewa haki anakimbilia mahakamani sio kuandamana.
Marekani incumbency may not help you!Kwahiyo Trump anazo power kama walizonazo marais wa africa ila hazitumii?
Hawajaambiwa na Trump waandamane.Hujaona wale waandamanaji wa TRUMP wa 'count all votes! Na kwingine 'stop the count!?
Trump anazo hizo power kama walizonazo marais wa afrika? Kwa sababu marais wa afrika wanafanya hayo wanayoyafanya kwa sababu wanazo power za kufanya hivyo iwe ndani ya katiba au nje ya katiba,je Trump akiamua kufanya kama marais wa afrika atafanikiwa?anao uwezo huo?Marekani incumbency may not help you!
Africa huku hiko ni kichaka
Tunajifunza kwamba sio afrika tu ndio kuwa watu hupenda madaraka bali hata huko watu hupenda madaraka,hivyo na huko nako kungekuwa na mazingira kama ya huku afrika basi nao wangefanya kama viongozi wetu huku afrika.Trump alijua mapema kuwa kushinda mwaka huu itakuwa ni kazi nzito!
Hivyo akaanza kujihami mapema kwa kumteua mkuu mpya wa shirika la Posta. Mkuu huyu badala ya kuboresha huduma za shirika yeye akaziharibu ili kuzorotesha upigaji wa kura kwa njia ya barua.( Wengi wa wapiga kura hizi ni wale wa rangi ya blue).
Mapema kabla ya uchaguzi alianza kujihami kuwa hatokuwa tayali kutoka WH kwani Demo’ wameshaiba kura kwa njia ya barua.
Usiku wa kupiga kura akajitangaza kuwa kashinda uchaguzi.
Na sasa anakwenda Mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi!
Hii yote inatufundisha nini?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hatuna cha kujifunza maana nako anaeshindwa hakubali analalamika kuibiwa kura sawa na wagombea wetu tu
Kwahiyo Trump anazo power kama walizonazo marais wa africa ila hazitumii?
I dont think soTrump anazo hizo power kama walizonazo marais wa afrika? Kwa sababu marais wa afrika wanafanya hayo wanayoyafanya kwa sababu wanazo power za kufanya hivyo iwe ndani ya katiba au nje ya katiba,je Trump akiamua kufanya kama marais wa afrika atafanikiwa?anao uwezo huo?
Kwanza Trump hata akishindwa bado ana miezi mitatu madarakani kabla Rais mpya hajaapishwa. Kwa namna hiyo muda upo wa kutosha kabisa kushughulikia malalamiko yoyote kama yapo kwa njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na mahakama. Marekani hawakimbilii kumwapisha rais harakaharaka kama tunavyofanya hapa kwetu hata kama malalamiko ya msingi yapo.Hatuna cha kujifunza maana nako anaeshindwa hakubali analalamika kuibiwa kura sawa na wagombea wetu tu
Sawa mmarekani wa mtandaoni, kwahiyo?Kwanza Trump hata akishindwa bado ana miezi mitatu madarakani kabla Rais mpya hajaapishwa. Kwa namna hiyo muda upo wa kutosha kabisa kushughulikia malalamiko yoyote kama yapo kwa njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na mahakama. Marekani hawakimbilii kumwapisha rais harakaharaka kama tunavyofanya hapa kwetu hata kama malalamiko ya msingi yapo.
La pili, Rais kulalamika kwamba kaibiwa kura hapa Afrika ni ndoto isiyowezekana kwani kwa Afrika Rais ni mungu mtu. Rais ndiye anaamua mgombea gani ashinde, kura ziibwe wapi na kwa njia gani, vyombo vya dola vitumike vipi kuwezesha ushindi wake na kila aina ya dhulma ina baraka zake. Kama hapa huoni chochote cha kujifunza basi sisi ni watu wa ajabu sana.
La tatu, huko nyuma Wamarekani wamepitia hali tete kuliko hii tunayoishuhudia leo lakini wakavuka salama. Ziko chaguzi zilikuwa na sintofahamu na tata kuzidi hii na watu wasioifahamu Marekani walikuwa na wasi wasi kuwa labda Marekani itasambaratika lakini haikutokea hivyo. Wanayo misingi imara isiyoyumbishwa na isiyoyumbika hovyo kwa matukio kama haya.