Yapo mengi ya kujifunza sisi kama watanzania kwaajili ya chaguzi zijazo:
1. Kura za mapema ni halali ili kupunguza mlundikano wa wapiga kura vituoni. Mfano Marekani kura za mapema zilianza Septemba, nasi tujifunze ili makundi maalum kama wazee, wafanyabiashara, walemavu, wanawake, maafisa wa Tume, mawakala wa vyama, wagombea na vyombo vya ulinzi wapige kura mwezi mmoja kabla.
2. Sio kila mpiga kura anapaswa kuamua nani awe Rais. Tumeona kule Marekani, Taifa lenye wapiga Kura zaidi ya Mil. 100, wanaoamua kiti cha URAIS ni watu 58. Hii inaepusha waovu kuwezesha mwovu mwenzao kuingia Ikulu. Huku Tanzania tumewapa watanzania wote haki ya kuamua nani awe RAIS, kwa mtindo huu, mwaka huu Mabeberu na mashoga walitaka kutupandikizia RAIS. Tujifunze kutoka Marekani
Hayo yanatosha kwa sasa
Ni wazi kuwa huna ulichojifunza wewe na labda hata kwa chama unachowakilisha kwa mawazo yako.
Mafunzo na UCHAGUZI wa Marekani yako wazi mno lakini kama ilivyo kwa mwanafunzi utayari kujifunza ni suala la msingi. Ni kawaida kwa wasio tayari kujifunza kutumia chochote ili kujitafutia fursa zaidi za kuhalalisha ubinafsi wao.
Nikilinganisha na kile ulichoandika:
1. Marekani kuliko na tume huru ya UCHAGUZI, Uhuru kamili wa mihimili ya utawala yaani mahakama, bunge na executive (serikali); mipangilio yao ikiwamo ya uchaguzi ni ya uwazi ili kufanikisha matakwa halisi ya watu. Kwenye mustakabala wa chaguzi kura huwakilisha matakwa halisi ya wapiga kura ambako kila kura ni lazima ihesabiwe.
Tofauti na funzo la wazi lililopo hapo kama kawaida yenu, wewe na wenzio mmejikita kwenye kutafuta fursa zaidi za kupanua wigo ili kuhalalisha wizi zaidi wa kura.
Hivi kura za mapema za ZEC zilikuwa na tija ipi, iwapo waliopiga kura ya mapema za ZEC walirejea tena siku iliyofuata kwa ajili ya kura za kawaida za NEC?
Makwetu macho kumchuzi. Ujanja ujanja tu. Yaani wizi wizi tu.
2. Marekani kila kura inahesabiwa. Majimbo yanapewa uzito tofauti idadi ya watu jimboni ikihusishwa. Hii haina maana ni kura za John, Harry au Tom kwa majina au vyama vyao tu zenye kuamua mustakabala wa uongozi nchini humo.
Tofauti na funzo la wazi kuwa huko hakuna chama wala mtu aliye na hati miliki ya uongozi au mustakabala wa uongozi, unataka kulazimisha mustakabala wa uongozi ni wa kubumba bumba usiojali matakwa ya wapiga kura kama makwetu usizonjeni!?
Unathubutu kusema "mngepandikiziwa rais." Kwani nyinyi nani? mbona wengine sasa wanaona wamepandikiziwa rais ambaye hata ameivuruga nchi hii vilivyo kutoka katika misingi imara ya kidemokrasia iliyoachwa na mwalimu Nyerere (rip)?
Kuna habari kuwa huyu bwana ana asili tata na wala si msukuma kama anavyojinasibu.
Pana wengi wenye mtizamo kuwa pana mtu ambaye uadilifu wake pale ikulu siyo. Kwamba huenda tuna mwovu pale.
Aaminiwe nani kwenye tuhuma za kibaguzi baguzi, kiramli ramli nk, kama hizo? Nyinyi au hawa wengine na kwa vigezo vipi?
Mkuu nimeangalia hayo mawili tu, tokea katika uliyoandika. Ama kwa hakika wewe ni mmoja wa wale wanaodhani hawana cha kujifunza. Wanajua kila kitu.
Vichwa mawe hawawezi kujifunza hata kwa watu waliowatangulia mno! Watu kama nyie ni msiba kwa taifa hili.
Ungeeleweka tu mkuu kwa kuweka wazi ulichokuwa unakitafuta:
"Mmeona fursa zaidi mnazoweza kupotosha ili kuhalalisha wizi zaidi kwa mgongo wa kuwa mmejifunza sasa tokea Marekani."
Yote yana mwisho na mwisho huo hauko mbali!