Tuna hatari zaidi kwa Vyombo vya Habari kuliko wakati mwingine...

Tuna hatari zaidi kwa Vyombo vya Habari kuliko wakati mwingine...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna kitu hakiko sawa. Inapotokea kuwa watawala wanashukuru, wanasifia, wanaunga mkono na wanaonekana kuwa wametulia na kuenjoy uhusiano wao na vyombo vya habari ni lazima tushtuke kidogo. Kwenye nchi zote zenye demokrasia ya kweli na zinazojaribu kujenga au zinazojenga utawala wa sheria mgongano kati ya vyombo vya habari na watawala ni matokeo ya lazima.

Inapotokea vyombo vya habari (vile vya zamani na hivi vya mitandaoni) vinajaribu kuwasiliana na watawala na kupeleka habari zake ili zihakikiwe basi tuna tatizo. Kama habari ikiandikwa halafu mtu anasema "itoeni hiyo habari" na chombo cha habari kwa kuogopa kuudhi au kwa kuhofiwa kuudhiwa kinakubali basi tatizo linazidi kukua.

Kuna watu wanaamini kabisa kuwa si lazima kuwe na ugomvi kati ya vyombo vya habari na serikali. Nakumbuka wakati wa mtawala fulani vyombo vya habari vilisifika sana kwa kupokea "bahasha". Matokeo yake nakumbuka mchorani vikatuni wa Kenya Bw. Gado alichora picha ikionesha vyombo vya habari vikimlamba miguu mtawala wa wakati ule. Inawezekana tumerudi pale tena?

Lakini cha kutisha zaidi ni kuwa kama watu ambao hata hawako serikalini na si watawala labda wana utajiri wa kutupa tu nao wanaweza kuamua nini chombo cha habari kinafanya au kinasema basi kile kinachoitwa "uhuru wa vyombo vya habari" si kingine bali ni kugeuka kuwa "kunguru wa habari". Wanaruka ruka, kula, na kupiga kelele, za hapa na pale, huku wakidonyoa donyoa kile wanachopewa. Hawatakiwi kuudhi watu au kumuudhi mtu.

Tunajuaje kuwa tuna uhuru wa vyombo vya habari; watu wengine wanasema sasa hivi vyombo vya habari na waandishi hawafokewi, hawapigwa, hawatekwi, hawaumizwi, wamekaa kwa starehe wanafikiri kuwa hili ni jambo zuri. Ni zuri kwa nani? Ni lazima uwepo mgongano kati ya vyombo vya habari na watawala.

Jukumu la vyombo vya habari si kuunga mkono serikali au kuipa maneno mazuri. Kile ambacho watu walisema kinatokea wakati wa JPM ndiyo hicho hicho kinatokea tena wakati huu wa SSH. Ukiangalia utaona kuwa ni shilingi ile ile ila upande mwingine tu. Sikuwahi kuwa na tatizo hata kidogo na watu au waandishi waliokua wanaikosoa na kumkosoa Magufuli.

Kuna watu wanafikiri tulimuunga mkono Magufuli halafu tukaegesha akili zetu pembeni wenyewe tukaondoka. Niliandika mada hapa ya kumtaka Rais Magufuli Ajiuzulu kama aliona kazi ya Urais ni ngumu (nina uhakika kuna watu hawakumbuki wanafikiri tulikuwa tunaimba sifa tu!). MADA HII HAPA BONYEZA HAPA.

Na mada hiyo nakumbuka ilipigiwa chapo na mkongwe MAYALA kwenye mada yake hii NYINGINE BONYEZA HAPA.
Ni lazima tuwe na uhuru wa kusema kisichopendeza, kuonesha kisichotakiwa, na kukataa kinachopendwa na wengine. Inapofika vitendo vya kifisadi vinahaririwa kwanza basi kile kinachoitwa uhuru wa vyombo vya habari hakipo tena. Ngoja tuone ili tufanye maamuzi saa hii. Nimeweka tena mada ya mwelekeo mpya wa ufisadi Tanzania uliorudi kwa nguvu.

UsiDOWNLOAD hii attachment; na ukidownload usiseme kilichomo.
 

Attachments

Kwanza hongera kwa kuliona hili ingawa liko obviously ktk jamij yetu. Ila nchi hii wazee waliokuwa katika system ndiyo walohusika kutufikisha hapa.

Vijana wamewaiga wazee. Kila mtu anafahamu hili. Itahitajika miaka 20 kutoka ktk jinamizi hili. Si vyombo vya habari tu hata vyuoni siku hizi hakuna kufikirisha fikra.

Ukiona wanafunzi wa vyuo wanaingia na kutoka miaka kadhaa na hakuna migongano ya demonstration au strikes unajua kuna shida. Elimu haijawahi kutengeneza misukule itakayokula kila unga wa ndele na kufuata mdundo wa ngoma. Hao waandishi ni muendelezo wa kinachotokea vyuoni.

Enzi fulani kama ya akina Zitto, Mtatiro, Mnyika na wachache wengine zinaisha. Lakini tunajua zilianzia universities.
Kwa hiyo, nionavyo, si waandishi tu peke yao. Ni suala la jamii mzima na mifumo yetu ya elimu, vyeo na uongozi. Leo, mtu anayesifu pasi na sababu "chawa" anaweza kupata cheo kikubwa serikalini kuliko mwenye sifa aliyejiandaa kitaaluma au kiutumishi.

Sasa basi hao waamdishi ni muendelezo tu wa kile mfumo wa kisiasa umetufiksha. Kesho utawala ukibadilika wote wanahamia timu iliyoshinda.
 
Wandishi wa habari njaa tupu

Sakata la sukari bila Mpina lilitakiwa kuonwa na waandishi wa habari kabla ya mtu yeyote

Sakata hili linatisha vibaya sana, lakini huwezi kuona tarifa hiyo popote zaidi ya kumnukuu Mpina na ama Lissu

Wao wapo kupewa milungula!

Kwa TANZANIA bado saaana hii tasnia
 
Wandishi wa habari njaa tupu

Sakata la sukari bila Mpina lilitakiwa kuonwa na waandishi wa habari kabla ya mtu yeyote

Sakata hili linatisha vibaya sana, lakini huwezi kuona tarifa hiyo popote zaidi ya kumnukuu Mpina na ama Lissu

Wao wapo kupewa milungula!

Kwa TANZANIA bado saaana hii tasnia
Ndiyo linaloshtua...nimesoma ushahidi wa Mpina..ile ingekuwa habari kwenye gazette au hata hapa JF..na ushahidi wote u gewekwa. Sidhani kama mtu anaweza kuleta ushahidi hapa bila kupitiwa na kamati maalum ya JF na kuwauliza wahusika kwanza.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna kitu hakiko sawa. Inapotokea kuwa watawala wanashukuru, wanasifia, wanaunga mkono na wanaonekana kuwa wametulia na kuenjoy uhusiano wao na vyombo vya habari ni lazima tushtuke kidogo..
Mkuu si uje na wewe uanzishe chombo chako kitakachokuwa kinapishana na Serikali. Kwani unafeli wapi?

Yaani mtu ametoa mtaji wake kama Family ya Reginald Mengi kujenga empire ya vyombo vya habari. Anatengeneza ajira kwa maelfu na kulipa kodi, wewe unataka aandike habari za kufurahisha wanaharakati!!
 
Naikumbuka kauli ya Lisu alivyo sema mwanzoni mwa uongozi huu kwamba tusishangilie sana au kuwa na matarajio sana na yeye , maana kwa wakati huo ilikua ni kama honey moon tu, pindi ikiisha tunarudi tulipo kuwa.
Na sasa tupo kikamilifu pale tulipotoka jana.
 
Mkuu si uje na wewe uanzishe chombo chako kitakachokuwa kinapishana na Serikali. Kwani unafeli wapi?

Yaani mtu ametoa mtaji wake kama Family ya Reginald Mengi kujenga empire ya vyombo vya habari. Anatengeneza ajira kwa maelfu na kulipa kodi, wewe unataka aandike habari za kufurahisha wanaharakati!!
Kwani ni lazima nianzishie nikiwa huko?
 
Penye Udhia Rupia inapenyezwa..., Samia Aliwaambia wakimfanya nini sijui atawapapasa na wakimfanya ndivyo sivyo atawaparura...

Anyway binafsi naamini Media inaweza kuwa muhimili stronger kushinda hata Bunge...

 
Penye Udhia Rupia inapenyezwa..., Samia Aliwaambia wakimfanya nini sijui atawapapasa na wakimfanya ndivyo sivyo atawaparura...

Anyway binafsi naamini Media inaweza kuwa muhimili stronger kushinda hata Bunge...

kha... kupepesana na kuparuana ndio mtindo wa kisasa? Maana kula na kulipa ulikuwa ni mtindo wa zamani...
 
Kinacho itesa tasnia ya habari Tanzania ni haki ya matangazo,Na ikumbukwe kuwa matangazo ndo chanzo kikuu cha mapato kwenye vyombo vya habari na mtangazaji mkuu ni serikali.Hii imepelekea ukasuku na sycophancy reporting.

Pia Kuna mgongano wa kimaslahi,itikadi na taaluma.Wamiliki wengi wa vyombo vya habari ni wafuasi wa vyama vya siasa,hivyo habari yoyote ambayo ni kinyume na itikadi ni ngumu kupata airtime kwenye air room au space kwenye magazeti na hii imeleta changamoto nyingi kwenye taaluma ya uandishi wa habari.

Kulingana na utafiti uliofanywa na Twaweza,MISA-TAN,Jamii Forum na TAMWA asilimia 50% ya waandishi wa habari hukumbana na vitisho,ukatili na unyanyasaji wa kijinsia nchini.
 
Back
Top Bottom