Tuna hatari zaidi kwa Vyombo vya Habari kuliko wakati mwingine...

Tuna hatari zaidi kwa Vyombo vya Habari kuliko wakati mwingine...

Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna kitu hakiko sawa. Inapotokea kuwa watawala wanashukuru, wanasifia, wanaunga mkono na wanaonekana kuwa wametulia na kuenjoy uhusiano wao na vyombo vya habari ni lazima tushtuke kidogo. Kwenye nchi zote zenye demokrasia ya kweli na zinazojaribu kujenga au zinazojenga utawala wa sheria mgongano kati ya vyombo vya habari na watawala ni matokeo ya lazima.

Inapotokea vyombo vya habari (vile vya zamani na hivi vya mitandaoni) vinajaribu kuwasiliana na watawala na kupeleka habari zake ili zihakikiwe basi tuna tatizo. Kama habari ikiandikwa halafu mtu anasema "itoeni hiyo habari" na chombo cha habari kwa kuogopa kuudhi au kwa kuhofiwa kuudhiwa kinakubali basi tatizo linazidi kukua.

Kuna watu wanaamini kabisa kuwa si lazima kuwe na ugomvi kati ya vyombo vya habari na serikali. Nakumbuka wakati wa mtawala fulani vyombo vya habari vilisifika sana kwa kupokea "bahasha". Matokeo yake nakumbuka mchorani vikatuni wa Kenya Bw. Gado alichora picha ikionesha vyombo vya habari vikimlamba miguu mtawala wa wakati ule. Inawezekana tumerudi pale tena?

Lakini cha kutisha zaidi ni kuwa kama watu ambao hata hawako serikalini na si watawala labda wana utajiri wa kutupa tu nao wanaweza kuamua nini chombo cha habari kinafanya au kinasema basi kile kinachoitwa "uhuru wa vyombo vya habari" si kingine bali ni kugeuka kuwa "kunguru wa habari". Wanaruka ruka, kula, na kupiga kelele, za hapa na pale, huku wakidonyoa donyoa kile wanachopewa. Hawatakiwi kuudhi watu au kumuudhi mtu.

Tunajuaje kuwa tuna uhuru wa vyombo vya habari; watu wengine wanasema sasa hivi vyombo vya habari na waandishi hawafokewi, hawapigwa, hawatekwi, hawaumizwi, wamekaa kwa starehe wanafikiri kuwa hili ni jambo zuri. Ni zuri kwa nani? Ni lazima uwepo mgongano kati ya vyombo vya habari na watawala.

Jukumu la vyombo vya habari si kuunga mkono serikali au kuipa maneno mazuri. Kile ambacho watu walisema kinatokea wakati wa JPM ndiyo hicho hicho kinatokea tena wakati huu wa SSH. Ukiangalia utaona kuwa ni shilingi ile ile ila upande mwingine tu. Sikuwahi kuwa na tatizo hata kidogo na watu au waandishi waliokua wanaikosoa na kumkosoa Magufuli.

Kuna watu wanafikiri tulimuunga mkono Magufuli halafu tukaegesha akili zetu pembeni wenyewe tukaondoka. Niliandika mada hapa ya kumtaka Rais Magufuli Ajiuzulu kama aliona kazi ya Urais ni ngumu (nina uhakika kuna watu hawakumbuki wanafikiri tulikuwa tunaimba sifa tu!). MADA HII HAPA BONYEZA HAPA.

Na mada hiyo nakumbuka ilipigiwa chapo na mkongwe MAYALA kwenye mada yake hii NYINGINE BONYEZA HAPA.
Ni lazima tuwe na uhuru wa kusema kisichopendeza, kuonesha kisichotakiwa, na kukataa kinachopendwa na wengine. Inapofika vitendo vya kifisadi vinahaririwa kwanza basi kile kinachoitwa uhuru wa vyombo vya habari hakipo tena. Ngoja tuone ili tufanye maamuzi saa hii. Nimeweka tena mada ya mwelekeo mpya wa ufisadi Tanzania uliorudi kwa nguvu.

UsiDOWNLOAD hii attachment; na ukidownload usiseme kilichomo.
Mmh bora liende tuu lakn kiukwel kuna jambo haliko sawa
 
Mkuu si uje na wewe uanzishe chombo chako kitakachokuwa kinapishana na Serikali. Kwani unafeli wapi?

Yaani mtu ametoa mtaji wake kama Family ya Reginald Mengi kujenga empire ya vyombo vya habari. Anatengeneza ajira kwa maelfu na kulipa kodi, wewe unataka aandike habari za kufurahisha wanaharakati!!
Kweli nimeamini Reasoning ya Mtanzania iko chini sana.
 
Kweli nimeamini Reasoning ya Mtanzania iko chini sana.
Wewe ambaye siyo Mtanzania na unayejua ku reason nikuulize; Je chombo chako cha habari kiko wapi?

Acheni kuwajazia nzi watu kwenye biashara zao
 
Siku zote na amini kama hakuna siasa safi katika jamii, hakuna sector itafanya vizuri.

Kuna tofauti kubwa kati ya uandishi wa habari na, uanaharakati.

Unaandika habari, unaanza kusakamwa kuanzia na boss wako, chama mpaka na watu wa suti nyeusi, mara futa, omba radhi usirudie haya yote nani anayataka?

Ndo mqana wengi wameamua kufanya linalo wezekana.
 
Back
Top Bottom