Karibu Jf Members tupate maarifa kisha tufanye maamuzi sahihi.
Ikiwa upo kwenye ujenzi au unatarajia kujenga ni muhimu kufahamu mambo machache kuhusu mfumo wa kusambaza maji safi/salama na maji taka kwenye mjengo wako.
Mifumo hii ya kusambaza maji salama na maji taka unajulikana kwa jina la plumbing system, na mtu anayefanya kazi ya kufunga na kurekebisha hii mifumo anajulikana kwa jina la kitaalamu ni plumber.
Kihistoria mifumo hii ya kisasa ya leo ni matokea ya maendeleo ya karne nyingi ambapo mifumo imara inagunduliwa kutokana na changamoto zilizojitokeza kwa nyakati hizo. Mifumo hii ilianza kuendelezwa na warumi ambao walikuwa wanatumia pipe za material ya lead (lead pipe), sasa lead kwa kirumi wanaita
plumbum na mtu aliyefanya kazi hizi akaitwa
plumberius, Sasa baada ya mifumo hii kwa karne nyingi kuzidi kuenea duniani likaibupa neno la plumber, ambaye ndio proffessional anayetambulika hadi sass kwenye maswala ya kufunga na kutengeneza mifumo hii ya maji salama na maji taka na sasa dunia inatumia plastic pipe za PVC (Polyvinyl Chloride) ambazo ni salama zaidi.
Tunaposema mfumo imara ni vile ufungaji wa pipe za maji, uliofikia kiwango cha kukukinga na magonjwa na kuleta comfortable ndani ya nyumba kwa maana mifumo imara ya kusambaz maji ufanya mazingira kuwa safi wakati wote, hairuhusi backflow yaani, maji taka kuchanganyika na maji salama au maji taka kurudi ndani ya nyumba wala hairuhusu upotevu au uvujaji wa maji usioeleweka au kutambulika.
Mifumo imara ya maji ni muhimu sana kwenye majengo japo watu wengi hudharau, mifumo bora na ya kisasa inaweza kukusaidia kupata maji salama kwa matumizi ya kunywa, kuoga, kupikia na kulinda nyumba yako au biashara yako na majanga ya moto, lakini pia inaweza kukusaidia katika utunzaji wa bustani.
Mfumo imara pia unaweza kukuepusha na upotevu wa maji unaopelekea kuletewa bili kubwa ya maji.
Kama ilivyo ujenzi unahatua, pia uwekaji wa mifumo ya maji salama na maji taka unahatua tatu, na ikiwa kipato chako ni kidogo unaweza kufanya kwa hatua moja moja hadi unakamilisha mfumo mzima.
Hatua ya kwanza, hapa ni kudesign na kulocate njia ya usambazaji wa maji kuingia na kutoka ndani ya nyumba yako ,pia hatua hii fundi atakufanyia na gharama za material ya bomba.
Hatua ya pili (top-out) ni ukishanunu material za bomba fundi atakuja kutoboa channel alizodesign au alizolocate na kufanya installation za bomba zote.
Hatua ya tatu ni finishing, fundi atakufungia plumbing fixtures mfano sinki la kunawia, sink la choo, shower, koki, water heater, water purification system, n.k
Pia ili mfumo wako uendelee kufanya kazi kwa ufanisi ule ule, weka mpango wa fundi kufanya repair mara moja unapohisi kuna tatizo dogo usingoje tatizo liwe kubwa utatumia gharama kubwa kufanya matengenezo.
Mwisho nawakaribisha wote kupata huduma zetu zinazozingatia utaalumu zaidi, zinazohusiana na maswala ya maji, kuanzia mifumo ya maji safi na majitaka, kufunga plumbing fixtures mfano water heater, water purifier, sink, shower, n.k. Pia tunatoa huduma ya tafiti ya vyanzo vya maji , kuchimba kisima cha mkono na mashine.
Ujachelewa wasiliana nasi sasa sms/call 0757914770
whatsapp 0759600809
Tupo DSM na mikoani tunafika kukuhudumia.