Tunachimba visima vya maji popote Tanzania

Tunachimba visima vya maji popote Tanzania

Gharama za upimaji kwa maeneo/mikoa mbalimbali kwa kutumia mashine ya kisasa inayoweza kutambua wingi,aina ya maji( maji chumvi au maji baridi), kina (Mita) na mikondo ya maji iliyopo ni kama ifuatavyo;
1.DSM 600,000
2.Morogoro 800,000.
3.Dodoma 1,000,000,
4.Singida 1,200,000.
5.Mikoa mingine Maelewano,
Mawasiliano 0744572145

Mimi nipo Dar Survey ni 200,000 tu!

Bila shaka mikoa hiyo uliyoitaja ni uongo pia!

Hatari sana![emoji849]
 
Milion Kam sab kwa mitambo
Pia kama mtu hana pesa kwa wakati mmoja, anaweza kununua materials kidogo kidogo, taratibu kisha akishakamilisha materials anabakiwa na swala la uchimbaji tu,..
 
Hizi gharama pia inategemea mashine ya kufanyia vipimo inatoka wapi, kwa kuwa kampuni nyingi zipo DSM inapelekea gharama kuwa kubwa kwa mikoani.
Kwa range ya harakaharaka DSM ni 300k- 400k, Pwani 400k- 500k, Tanga,Moro ,Dodoma 600k - 900k,
Kwa ujumla kadili unavyozid kwenda upcountry ndivyo gharama inazidi ila hii gharama unaweza kuipunguza ikiwa tu mkoa uliopo kuna kampuni inatoa hii service, au kuvizia au kukutana na kampuni imepata tenda mkoani then unawadandia wapitie na kwako, watakufanyia kwa bei nafuu zaidi
Nashindwa elewa, hivi kama bei ndio hizi kwanini miradi ya serikali unakuta bei ni kuanzia 50mil to 200mil?
 
Maji yapatikana mkuu hata kama kuna miamba vipi, kikubwa ni kufanya survey kujua yapo kwenye kina gani?
Sawa sawa ningependa kujua surgery ni bei gani hasa kwa huku wilayani sengerema mwanza...?
 
Nashindwa elewa, hivi kama bei ndio hizi kwanini miradi ya serikali unakuta bei ni kuanzia 50mil to 200mil?
Moja ya mambo yanayochangia bei ya miradi ya serikali kuwa kubwa ni kawaida walioijenga watumishi kwa kuchelewesha malipo sasa unakuta mzabuni anapiga hesabu hadi za delay za malipo ndio unakuta bidhaa ya elfu 50 anaandika laki 2.....
 
Mtoa mada ungeweza fanya biashara sana kama ungekuwa muwazi kwenye bei, dunia ya leo wateja wakishaona unaficha ficha bei wanakukimbia ata first instance.

Weka bei na sifa za bidhaa yako, utaona unapata leads nyingi zinazoishia kuwa customers. Yani lead unayopata sio ya mtu anayetaka kujua bei, bali ni ya mtu aliyeona bei ya bidhaa zako, akaridhika nayo, sasa anakufuata akiwa asha ridhika na bei.

Kuna ugumu gani ukifanya kama hivi
Sprinkler 3/4"
1. Material1 Bei xxxx Coverage xMeters
2. Material2 Bei xxxx Coverage xMeters
3. Material3 Bei xxxx Coverage xMeters
Hapa chini unaweza tumia nafasi kulinganisha hizo bidhaa kiubora kiufupi sana.

Sprinkler 1"
1. Material1 Bei xxxx Coverage xMeters
2. Material2 Bei xxxx Coverage xMeters
3. Material3 Bei xxxx Coverage xMeters

Sprinkler 1.5"
1. Material1 Bei xxxx Coverage xMeters
2. Material2 Bei xxxx Coverage xMeters
3. Material3 Bei xxxx Coverage xMeters

Sprinkler 2"
1. Material1 Bei xxxx Coverage xMeters
2. Material2 Bei xxxx Coverage xMeters
3. Material3 Bei xxxx Coverage xMeters

Sprinkler 2.5"
1. Material1 Bei xxxx Coverage xMeters
2. Material2 Bei xxxx Coverage xMeters
3. Material3 Bei xxxx Coverage xMeters

Umepata nafasi ya bure ya kutangaza jf. Basi tumia nafasi vizuri.
 
Naomba kujuwa garama za uchimbaji kisima naishi dar es salaam ilala kitunda
 
Inategema na mkoa unaotaka kisima kichimbwa, ila kwa takwimu za DSM, bei inarange 50k to 75k inategemea na kampuni na urefu wa kisima.
Kwa Pwani inarange 80k - 100k, onategemea na kampuni na urefu wa kisima pia. Kwa mikoani ya bara mara nyingi 120k - 200k inategemea na umbali, kampuni husika na urefu wa kisima.
Hizo bei ni kwa mita moja,
Hizi bei kwa kwa kila mita moja?
 
Kwa ujanja wa bongo hapa napo unaaweza kuangishiwa kitu kizito yaani laki 6 kupima, anakuja anazunguka zunguka saiti baadae anakwambia tayari nimepima kuna maji au hakuna maji anaodoka na laki 6. Baada ya hapo wakati wa kuchimba unakuja unachimba mpaka futi elfu 10 ndo unakutana na maji. Si bora waje waanze kuchimba tubaatishe tu hivo hivo. Hii ni sawa na wakati simu zimeanza kuingia nchini miaka ya 90+ simu ikiharibika unapeleka kwa fundi anakwambia kucheki tu elfu 5 na uko kucheki ni kufungua tu kisha anafunga na raba bendi alafu unaacha elfu tano. Haahahahahaaaaa
Hilo neno .. TUBAHATISHE.. ndo linabeba utaalamu wote. WHat if umebahatisha halafu hujapata maji, utalipa gharana za kuchimba?
 
Naomba kujuwa garama za uchimbaji kisima naishi dar es salaam ilala kitunda
Mita moja inachimbwa kwa elfu 60 , na kujua uchimbe mita ngapi inabidi ufanye underground water survey ,gharama yake ni 200,000/=
 
Back
Top Bottom