Tunaelekea wapi jamani? Mfuko wa saruji(cement) umefikia Sh. 15,500/= Kigamboni

Tegeta, bunju, kiwanda kiko hapa hapa lakini mfuko ni 14000......yapo mengi sana viipi petrol kwa sasa? Kwakwel tunakoelekea ni njia yenye utelezi na kiza nene kisha malaika akitufutia na upanga
 
 
 
Tegeta, bunju, kiwanda kiko hapa hapa lakini mfuko ni 14000......yapo mengi sana viipi petrol kwa sasa? Kwakwel tunakoelekea ni njia yenye utelezi na kiza nene kisha malaika akitufutia na upanga
Jana nimeitafuta sikupata nikaja ipata shs 16,000 kwa mfuko.....kiwanda cha wazo kipo mita 800 toka nilipo!!!!.....hawa wenye viwanda watakuwa wameanzisha cartel yao????
 
Ukiwa Dubai au Pakistan mfuko wa cement ni shilingi elfu 6 hadi elfu 4... Haya maisha bhana watu wanapiga hela halafu wanaenda kuwekeza ulaya
 
Alafu kuna watu wanashangilia kupungua bei ya bei huku ya cement ikiwa juu jaman
 
Nipo Jirani kabisa na kiwanda cha wazo ila kwa sasa siwezi kupata access ya kupata cement. Kwa sasa mzigo tunachukulia Ubungo kwa mhindi na yenyewe inabidi uwahi saa Tisa usiku ili uhesabiwe mamba.........
Hahahahah..., aaagh...!!? Tumefikia huko?
 
Kwanini Dangote haleti Cement Dar?
 
Punguza kidogo UONGO mkuu. Saruji haijawahi kufika sh 19,000 kwa mfuko Mtwara katika hicho kipindi ulichowasilisha.
 
tuna mpango wa kuanzisha viwanda vya cement kila wilaya.
 
Punguza kidogo UONGO mkuu. Saruji haijawahi kufika sh 19,000 kwa mfuko Mtwara katika hicho kipindi ulichowasilisha.
Mkuu unataka tuanze kubishana??Nilikwepo huko kipindi ambacho saruji ilifika 19,000/- mpaka niliingiwa na tamaa ya kuanza kusupply manake hata kama ningeweza kununua mfuko Dsm kwa 14,500/- bado nilikuwa naweza kupata faida ya 3,500/- kwa kila mfuko kwa maeneo ya Tandahimba na Nanyamba by that time ingawa baadaye nilighairi kufanya.
 
Wewe ulikuwepo kimatembezi, mimi baadhi ya shughuli na kazi zangu ziko maeneo haya ya Kusini. Kwa hiyo naongea kiuhalisia na uelewa zaidi. Binafsi huwa sio mtu wa mabishano, umri umenifundisha mengi. Hayo maeneo uliyotaja Tandahimba na Nanyamba hizo zilikuwa ni bei za walanguzi na wahuni wachache. Ndio maana mleta mada ameleta hoja/taarifa ya Bei ya kigamboni na sio ya Dar es salaam nzima.
Kila la kheri kamanda.
 
Hizo bei zilikuwa ni za kipindi kile Dangote Cement industry amesimamisha uzalishaji,
Hing demand ~Less supply= inflation rate.
NB;Kwa uzee huu nilionao sio tena kamanda, niite mkuu inatosha, ukamanda tumewaachia vijana wetu na wajukuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…