Tunafahamu ni utandawazi ila hii sio sawa!

Tunafahamu ni utandawazi ila hii sio sawa!

Nimekutana na video moja kwenye mtandao wa Facebook, inaonesha watoto bila shaka ni watoto wa chekechea kwa hakika sidhani kama hii imekaa sawa.
View attachment 3222541

Ni jambo zuri watoto kupata muda wa kufurahi na kujifunza ila sio kucheza mitindo hii tena mbali zaidi kufanya challenge za mitandao ya Facebook na Tiktok.
Binafsi kwangu hii ni BIG NO!
Hii ni shida kubwa.
Afande Sele alisema;
Maendeleo yanakuja na mambo Leo.
 
Basi na uendelee kuwapigania wabongo tulishachoshwa na unafiki na uzandiki wa wabongo wenzetu,uchawa,wizi na ujinga wote wa kula na kuvimbiwa halafu tunawakejeli wenye shida ,matatizo na uhitaji wa kweli.
 
Ushenzi upo ila sio kama South
Ulinganifu tunaojipa na south ni upi?Ni swala la muda wasouth walisha amka na kuona mwendo sio ili mambo yaende ama kuwadhibiti wavamizi wa fursa zao ama watwawala wao.Sisi tumejikita kushibisha tumbo la chawa mmoja mmoja kwa imani kuwa atawadhibiti wenye njaa na mahitaji na kusahau shida zao.Japo mimi sioni kama ndio dawa .ila dawa ni kuacha ujinga na kufanya yaliyo sahihi na kwa manufaa ya wengi na sii wachache au yale manufaa ya makundi ya twawala.
 
Nimekutana na video moja kwenye mtandao wa Facebook, inaonesha watoto bila shaka ni watoto wa chekechea kwa hakika sidhani kama hii imekaa sawa.
View attachment 3222541

Ni jambo zuri watoto kupata muda wa kufurahi na kujifunza ila sio kucheza mitindo hii tena mbali zaidi kufanya challenge za mitandao ya Facebook na Tiktok.
Binafsi kwangu hii ni BIG NO!

Ni sawa tu, Kama walimu wamethubutu ina maana wazazi hawana noma, shida yako nini sasa? Ila ingekuwa ni wangu ingekuwa balaa nzito!
 
Afu unakuta huyo ndo alikuwa kinara kupinga usaili 😂
walimu ni wengi sana hivyo mchujo uwe mlaki zaidi kwa manufaa ya kizazi kijacho

ikibidi kuwe na upimaji wa walimu hata baada ya kuajiriwa mtu afai apishe wanaofaa elimu na afya si vitu vya kuleta mzaa
 
walimu ni wengi sana hivyo mchujo uwe mlaki zaidi kwa manufaa ya kizazi kijacho

ikibidi kuwe na upimaji wa walimu hata baada ya kuajiriwa mtu afai apishe wanaofaa elimu na afya si vitu vya kuleta mzaa
Waalimu wakiona hii Comment wanaweza kukuachia laana 😂
 
Back
Top Bottom