Tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa juu ya timu ya watu inayounda 'Mamlaka za Uteuzi' nchini

Mkuuu nchi hii sio ya dini fulani nchi hii ni ya watanzania wote...uwe mganga wa jadi muislam,mkristo ,mbudha,wapagani na makundi mengine .Hakuna kundi lenye haki juu ya kundi lingine sisi wote ni sawa na ni watanzania ukiona mtu kila teuzi zikifanyika anaangali dini ni mpuuzi tena huyo hafai hatakiwa hata kwenye jamii aondolewe maana hawa ndo wanaleta chokochoko.Hivi mkuu kila kundi likaanza kudai kila teuzi awepo mtu wao hilo litawezekana kweli?Hebu tujenge Tanzania yetu upuuzi na udini tuuache.
 
Mbona Zanzibar ni waislamu tupu?
 
Upo sahihi, mleda uzi mbona halalamikii Zanzibar?
 
Uwezo binafsi usitake tukuteuwe na ukenge wako kisa eti wewe ni mkristo au muislamu

Na sisi ambao hatuna dini tukianza kulalamika kuwa 99% wanateuliwa wenye dini mnasemaje??

Udini ni kitu tulicholetewa na ni kibaya sana.
 
Uzi mrefu ila Umejaa PUMBA TUPUUU

Ww una amka asubuhi una blame udini ? Jinga sanaa ivi huu uhuru wa Taifa hili ungepiganiwa kwa minajili ya Udini. Leo tungekuwa na Tanzania ? Nenda zanzibar kqangalie ratio ya viongozi waislamu na wakristo ...kwan zanzibar hakuna wakristo ?

Achaga kuja na HOJA za KIPUUZI karne hii ya 21

Tena Moderator ingekuwa sahihi kama hili li PUMBA mnge FUTA huu ni KUCHOCHEA UDINI fanya jqmbo Moderator mfute hii takataka
 
Waislam hawakwenda shule
Acha upotoshaji wewe ,binafsi nilikuwa mwanafunzi UDSM degree ya kwanza , tukiangalia Majina ya wanaopata admission na graduates of postgraduates in higher degrees Waislamu hakuna?
 
Kwani dini zilizopo Tanzania ni waislam na wakristo tu? Mbona kuna dini za asili na watu wa dini za asili wako wengi tu.
 
Makabila makubwa hapo ni mawili tu
 
Upo sahihi, mleda uzi mbona halalamikii Zanzibar?
Tena mkuu mm hua inaniuzi sana kuona mtu anahangaika na udini kwenye mambo ya kiserikali.Mbona zanzibar wakristo wapo mbona haangalii huko ama kwa kua wao wako kimya .Km mm hapa sina dini nipo nipo tu je na mm nilalamike kwa nn hatuchaguliwi sisi wapagani.
 
Wewe jamaa ni mdini sana!
 
Umesema vizuri kuwa nchi hii ni ya watu wote, sasa inakuwaje teuzi nyingi huwa zinalalia kwa watu wa dini moja kwa margin kubwa mno wakati shule tunazosoma ni zilezile na watu wenye vigezo vyote wanapatikana katika dini zote kubwa nchini—Je hii ni bahati mbaya au kuna watu huwa wanahakikisha hilo litokee kwa sababu zao za udini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…