Tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa juu ya timu ya watu inayounda 'Mamlaka za Uteuzi' nchini

Nmesoma nmepata kchefuchefu haswa huyu jamaa n mdin sjapata by the way watu wamekujbu Sina haja namj nijibu
 
Hakuna uthibitisho wa hilo, unayo credible information kutoka mamlaka za Tanzania zinazothibitisha hilo?
Current statistics on the relative sizes of various religions in Tanzania are limited because religious questions have been eliminated from government census reports since 1967. A 2010 survey from the Pew Research Center found that 61% of the population are Christian, 36% are Muslim, 2% practice traditional religions and 1% are unaffiliated.
 
Hoja ya kutokuwepo Waislamu wasomi ni hoja Muflisi, hapa chini nakuwekea list ya Waislamu wenye PhD.
Waislamu wenye masters wako wengi, wenye figrii ya kwanza bdo usiseme—Sasa watakosekanaje waislamu wa kutosha ndani ya watu 20, 30 au hata 100 wanaoteuliwa?









 
Kwa hizi teuzi mbili tu , ambazo huyu mama amefanya Kuna kila dalili ya kwenda kufeli vibaya sana huko mbele ( massive failure ) Kama nilivyosema kwa Jiwe kuhusu uongozi wake na huyu mama yanaenda kumkuta hayohayo .
 

Mkuu, hebu tutumie common sense na reason.

Sasa hivi Rais ni Muislam, Waziri Mkuu Muislam, mkuu wa Tiss ni Muislam, Katibu Mkuu Kiongozi pia ni Muislam
Hawa watu ndio Wana influence teuzi zinazofanywa na Rais, so hawa wanaweza wakawa wanapendelea Wakristu na kukandamiza Waislam wenzao? Ili iweje? Inakuingia akilini?

Au kuna force nyingine inayowalazimisha kuteua Waislam wachache? kama mnavyodai ni kanisa katoliki, kanisa katoliki Tanzania lina nguvu kiasi hicho? inakuingia akilini?

Mimi nimesoma shule ya bweni inayochukuwa wanafunzi nchi nzima. Kwenye ile shule wanafunzi wa Kiislam walikuwa hawazidi robo, japo ni taifa zima

Pia nimesoma Chuo Kikuu Mzumbe, ambayo ni taasisi inayochukua wanafunzi nchi nzima pia, Wamafunzi wa Kiislam walikuwa hawazidi robo mkuu

Hii inakupa picha gani? kuwa Waislam wanabaguliwa hadi kwenye elimu za msingi? Hapana, Hawazingatii elimu? Hapana. Hii inamaanisha kuwa Waislam Tanzania ni wachache kuliko Wakristo, na wala haliumizi kichwa hili, sababu ni mikoa mingapi hapa Tz ina Waislam hata nusu tu ya wakazi wote? Nadhani ni michache sana, Lindi, Zanzibar, Tanga labda na Dar. So tuache mihemko na tutumie mantiki zaidi tutaepukana na mawazo kama yako
 
[emoji3][emoji3]
 
Hizo data zinatambuliwa na Mamlaka za Takwimu za Tanzania? —Hiyo taasisi ya kusensa watu ilipata wapi kibali cha kufanya censoring?, Hizo ni takwimu feki, siyo credible
 
Hivi wewe unaamini raisi ndo anafanya kila kitu kwenye vetting? —Huyo analetewa majina tu, na yeye akiwa siyo muelewa wa picha pana ya nchi yake anasaini tu.

Huoni leo kaletewa Jina la Mwana UVCCM kamteua kuwa mkurugenzi TPDC, kelele mitandaoni zilipozidi kamtengua. Hii ni kwa sababu kuna mamlaka za Vetting zinazopeleka majina kwake, Sasa kwenye huu uzi nalia na hizi mamlaka huenda ndani yake kuna wadini waliokubuhu,, wanaopeleka majina ya mrengo mmoja kwa raisi.

Hii hoja ya ubaguzi kwenye teuzi haitokufa mpaka ionekane wazi hakuna motive ya udini kwenye hizi teuzi, maana haiwezekani kila teuzi zinapofanyika basi watu wa dini moja wanaonekana wanawazidi wenzao kwa ratio ya almost 80:20,Hizi mamlaka za Vetting lazima zichunguzwe!
 
Mama aliweka wazi kuwa ataangalia record ya mtu, hawa ndugu wanaoteuliwa si kwa ajili ya kusaidia dini flan au kanda flani bali ni kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote wa tanzania, merits first.
Ukitaka azingatie hicho kigezo Cha dini utakuta kumbee hizo dini na zenyewe zimegawanyika
 
Hizo data zinatambuliwa na Mamlaka za Takwimu za Tanzania? —Hiyo taasisi ya kusensa watu ilipata wapi kibali cha kufanya censoring?, Hizo ni takwimu feki, siyo credible
Ha ha ha ha, mkuu, achana na mambo ya Dunia, mtafute Allah uione pepo.
Maana sasa unapinga kwa jazba tu,
Hilo gazeti lako la idadi ya Muslims lilipata kibali kukusanya hizo takwimu au waliangalia prospects za vyuo wakiwa vyumabani?

Tukileta gazeti la wasomi wa kikiristo litakawa na mamilion ya majina.
Tuache hizi mambo
 
Kwa sensa zipi ndugu?
[emoji1542]Kama umewahi kusoma, kuanzia elimu ya msingi, sekondari mpaka elimu ya juu (zingatia madarasa yako husika katika hizo hatua zote), utagundua kuwa hata kwenye madarasa yako uliyowahi kusoma wakristo ni wengi.

[emoji1542]Angalia matokeo ya kidato cha nne na sita, angalia wanafunzi 10 bora kitaifa,angalia waalimu wengi mashuleni,utagundua kuwa wakristo ni wengi.

[emoji1542]Angalia mikoa inayoongoza kwakuwa na wasomi wengi (Kilimanjaro, Bukoba) kote huko wakristo wametawala.

[emoji1542]Angalia idadi ya shule za kidini Tz, utagundua kuwa ni za kikirsto.

NB:Kwa hapa Tz, wasomi wengi ni wakristo, hilo ni hakika. Hata hivyo katika swala la uteuzi,ni vyema tukazingatia weledi na uchapakazi kuliko udini.Kwangu mimi mkristo au mwislam wote ni sawa tu.
 
Rubbish Muslim tabloid paper...
Kwahiyo kila dini inachapisha majina ya wasomi wa kujigamba nao.

Kwa leo huna hoja kabisa
 
Hakuna vetting ya kueleweka kwa nini? Mbona haya mambo yanajitokeza mara kwa mara? Aibu sana sana kwa taifa. Ndio maana tunapata hadi viongozi wa juu kabisa ila wanakuwa wa hovyo.
 
Sasa ni ajabu eti vigezo ionekane wanavyo zaidi watu wa dini moja, hii inawezekanaje.

Yaani mchota maji kila siku unachota maji ya lita tano na unapochota kuna sehemu ina tanki la lita 500 na tanki jingine lina lita 1000, maji sawa yote yana sifa sawa ila wewe mchota maji kila siku unachukua maji kwenye tanki moja. Lazima itakuwepo sababu ya uamuzi wa kulipendelea tanki moja. Hoja hapo siyo kwamba tanki jingine halina maji, bali utakuwa na sababu binafsi za kufanya hivyo, huenda ni sababu za maana au za kijinga, lakini sababu zipo
 
Ungekua kiongozi nchi ingeyumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…