Tunaitaka Tanganyika yetu! Wakati ni huu...

Tunaitaka Tanganyika yetu! Wakati ni huu...

Kinachoniuma zaidi ni hawa wasomi Maprofesa ambao wengi wao wamesomeshwa na fedha za walipakodi watanzania kupata hiyo elimu... Anayenitia kichefuchefu ni Prof. Tibaijuka, msomi, mwanamama aliyeshika nafasi kubwa UN... Nilitegemea kwa usomi na uzoefu alioupata kwenye anga za kimataifa utasaidia kutoka hapa tulipo lakini mawazo na michango yake hayasadifu kabisa na usomi na uzoefu wake... Anazidiwa na mtoto mdogo kama Ester Bulaya mwanasiasa kijana lakini mzalendo...

Kwa kweli huu wasomi wetu hasa hawa maprofesa wetu elimu yao haijasaidia kabisa taifa hili... Ni hasara na mizigo ya taifa...

Lakini CCM ndiyo inakata roho... waliambiwa wajiandae kisaikolojia bado wanashangaa...
Najiuliza profesa Kapuya kapata wapi ujasiri wa kwenda nje na msimamo waliouweka akina Wasira?
 
angalao profesa kapuya alisema wanayoyataka watanzania yaani kura ya siri.
 
Tanganyika njoo mbozi na huku chunya wanahaja nawe nchi yao uliyetokomezwa kusiko julikana wanataka kukuona
 
Katiba mpya yaweza kuwa ni pigo la mwisho la CCM. Hawawezi kusoma alama za nyakati na kugundua mapema maoni ya Wananchi walio wengi. Hata sasa CCM hawajui kuwa Muundo wa serikali tatu si maoni ya Warioba wala Chadema bali ni maoni ya Wananchi wengi. Wao wangetakiwa kuyashika, kuyaongoza na kutengeneza mabadiliko kutoka serikali mbili kwenda tatu kwa muono wao. Kwa vile hawaoni wala hawasikii maoni ya walio wengi, sasa wamejiingiza katika mtego wa kupingana na majority. Sidhani kama watapona! Hata wakitumia mabavu kubadilisha rasimu ya Katiba ya Watanzania chini ya tume ya Warioba, badi hawatapona! Tunaweza kuyaona baadaye yale ya Tunisia, Libya na Misri. Hata wakisema kura iwe wazi, bado hawatapona. Siamini kama wamefaulu kuwanunua wabunge kutoka Zanzbar, kwani sidhani kama 2/3 yao watataka serikali mbili. Kikwete anajua hilo. Kuna wakati aliwashauri wenziwe ndani ya CCM kujiandaa kisaikolojia kukubali mabadiliko lakini hawakumwelewa na pia naye hakuwa katika nafasi ya kukubaliana na maoni ya waliowengi. Pole CCM! Bye bye! Mnapitia njia ileile ya KANU ya Kenya na UNIP ya Zambia! Salaam zao.
 
Inaonekana viongozi wa ccm zanzibar wanawashawishi wa bara waendeleze muungano, ccm visiwani wanajiona kabisa kuwa muungano unawabeba kwa kupata uongozi bara, ccm bara msiwaone aibu viongozi wenzenu wa visiwani , " wambieni kuwa wanzanzibar hatuutaki muungano"
 
mkuu hivi kuna nini kimejificha kwenye huu muungano maana maana naona nguvu kubwa Sana inatumika. hahahahah Tanganyika kwanza
 
Profesa anasema Tanzania ni muungano wa Zanzibar na Tanzania bara. Hata yule wa elimu alisema Tz ni muunganiko wa zanzibar na madagascar
 
Najiuliza profesa Kapuya kapata wapi ujasiri wa kwenda nje na msimamo waliouweka akina Wasira?
haha..CCM ni ugonjwa...Kaputa kaanza amini sheria lini wakati juzi tuu kaapindisha sheria kwa mbwembwe...nilichoakuwa nashangaa ni kwamba kafika vipi pale na kesi mbaya vile.Alikuwa akipua hadi mic inachukua na kufikisha ktk TV.
 
kwa hiyo unawachukia sana makamanda wa chadema mohamed mtoi na said mohamed kwa sababu ni waislamu waswahili?
Tatizo lenu hakuna tofauti na WISHES ZAKE NA FIKRA ZAKO..hizi ndizo wishes zako ktk daily wish list..mwehu wewe. Utabaki ukitamani sana iwe hivyo hadi ufe.Mtoi anachapa mwendo..na siku moja utamsikia ,,..utaishia badili hadith ktk mafanikio yake na kumwita kibaraka hadi siku anachukua top position. Si ndio nyie kutwa mnawaiata watu walio open ktk dunia ya Mungu kuwa si waislama kamili...
 
Profesa anasema Tanzania ni muungano wa Zanzibar na Tanzania bara. Hata yule wa elimu alisema Tz ni muunganiko wa zanzibar na madagascar
CCM ni kansa..na speed speed govonor ya ubongo yenye switch ya kuzima tuu ubongo na si kuuwasha.
 
Siku Tanganyika ikirudi nitafanya Re-birth party ya Tanganyika! Mpaka leo najiuliza hata sipati jibu kwa nini Nyerere aliiua Tanganyika yetu.
 
Siku Tanganyika ikirudi nitafanya Re-birth party ya Tanganyika! Mpaka leo najiuliza hata sipati jibu kwa nini Nyerere aliiua Tanganyika yetu.

Sababu kubwa za Nyerere kuuwa Tanganyika ilikuwa ni ile ile inayowafanya ccm leo waogope serikali tatu.

Ndani ya serikali tatu, ccm itapata tabu sana kushinda chaguzi na kwenye mijadala ndani ya bunge. CCM wanategemea sana siasa za kikanda, kidini nk ili kupambana na upinzani na kuwalaghai watz. Zanzibar wanapata nguvu kwa kutmia hoja za kidini na huku bara wanatumia zaidi hoja za kikabila na ukanda kutishia watu. Nyerere alilijua hilo. Tatizo ni kwamba Tanzania ni sehemu ya world integration ambayo is driven by western capitalist. Kwa hiyo its so much bound to so many social dynamics zinazotokea sehemu nyingine duniani. CCM hawataki kulifanyia kazi hilo vizuri na Nyerere hayupo kuwasaidia.

Mabadiliko yoyote ya muungano ndani ya TZ yatakayopelekea kuwepo kwa serikali tatu and bunge la Tanganyika itakuwa ni pigo Kali sana la kiuongozi kwa CCM. Inaonyesha ni jinsi gani walivyofail kusolve mambo ya msingi ya watz.
 
Mfamaji, Nara,

..basi na nyinyi mjizuie kutumia neno bara, au Tanzania Bara.

..mlitumie jina Tanganyika, na siku zote mjitambulishe kama wa-Tanganyika.

..wenzetu hujitambulisha kama wa-Zanzibari, halafu baada ya hapo ndiyo hutoa maelezo kuwa wanatoka Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Ukweli mwingine ni kwamba cheche zimeanza kuonekana. Naibu spika, Ndugai anaonyesha hasira za wazi dhidi ya kauli za wajumbe toka visiwani. Na kwa usalama wao ni bora watenganishwe wajumbe toka pande hizi mbili

Namuunga mkono Ndungai kwa sababu, katiba inayo andikwa hapo haihusiani na Zanzibar, inaihusu Tanganyika. Zanziba wanayo katiba yao sasa sijui wanatuandikia sisi Watanganyika kwa kuwa hatujui kuandika au?
Utaandikaje ya muungano wakati wale waliosema wameungana na Zanziba hawana katiba? Leteni kwanza ya Tanganyika, ifufueni Tanganyika ndipo mlete muungano kati ya nchi mbili, Tanganyika na Zanznziba. Ndipo liundwe bunge la katiba ya muungano. CCM acheni kuweka kitu kisichokuwepo kihalisi. Muungano huu ulivunjika siku CCM iliporuhusu Zanziba kuwa na katiba yake. HAKUNA MUUNGANO WOWOTE HAPA. Ni ndoto tu
 
Back
Top Bottom