Tunajua Mengi tunanyamaza, Lissu kudharau Mamlaka ya Ikulu kumefanya kufifisha juhudi zilizopangwa na Rais Samia kuleta maridhiano

Upuuzi mtupu

Kwa hiyo ndiyo maana Mbowe akabambikiwa kesi?

Msemaji wa Chadema ni Mwenyekiti, kwa nini Ikulu haikumtafuta Mwenyekiti ikamtafute Lissu?

Hata kama Ikulu iliamua kumtafuta Lissu, Lissu still yuko sahihi, lazima ujipange kabla ya kuongea na raisi, ushauriane na wenzio kitu cha kupresent, uandae nondo, evidence na points, siyo kukurupuka
 
Hivi kwa kauli ile ya Samia pale BBC kuwa wenzake Mbowe walishahukumiwa na wanatumikia kifungo sasa bado mnamsema Magufuli ndiyo alidraft ile kesi? Mbona mnasingizia sana Marehemu! Upinzani hapa nchini hawajui wanataka nini, wenyewe wapowapo tu upepo ukivuma hivi nao wanaenda hivi basi tu ila acheni kumsingizia marehemu kwani gajaingia kinywa cha mtu pale.
 
CCM ni wanyama ila kuna wakati hata upinzani kuna mambo unashangaa imekuaje anasema huyu ....Lissu anaongea mno mno na kibaya zaidi anajua kila kitu.
Lissu naturally ni talkative ila walichomfanyia kimemfanya kuwa mtu mwenye hasira sana. Matokeo yake hachagui maneno wala tone ya kuyaongelea.
 
Niko kwenye ajenda yako uliyosema rais akisema basi inatakiwa kufanywa. Ndio nikakuuliza akikuambia ufanye yale ambayo ni kinyume na msimamo wako utafanya kwa sababu rais kasema? Hii sio nchi ya kifalme kaka yangu.
Mimi sijasema ufanye kitu anachotaia Rais.

Ninachopinga hapa ni kujili,jaliza kama mbwa koko baada ya kupigwa kwenye vita uliyojiingiza mwenyewe.

Kama huwezi battle, kaa pembeni.
 
Habari hii ina uongo mwingi sana.... hivi kama watu wote hao walibambikiwa case zote hizo na wengine wanakimbia... kwanini Rais asizifute na afanye juhudi warudi? kwanini tumtee Samia kwa kumsingizia Lissu na chadema? Hivi kweli Lissu na Chadema ndio wamezuia Rais kufuta hizo case zinazo itwa za kubambikwa? Hivi kwa hiyo Rais asipo kutana na Lissu ndio case ya Mbowe itaendelea? Kwani lazima akutane na Lissu kwanini asikutane na chadema? nini kinamzuia? halafu hiyo case ya Mbowe Rais si alisema wengine wameshakiri makosa na kuhukumiwa na sasa wanatumikia vifungo?
Hivi kwanini watu wasiseme Rais hajui cha kusimamia? anaogopa nini? kwanini matendo yake yasihakisi maneno? kwanini ana jaribu kuonesha yeye ni mwema? anaogopa nini kuwa moto au baridi?
 
Pamoja na kwamba Chadema walikuwa wamesha surrender kwa Magufuli ambaye katangulia mbele ya haki sasa , ndani ya Serikali na CCM Kuna watu bado wana mawazo chanya waliona itakuwa si vema kuongoza nchi bila maridhiano,
Wewe sio Britanicca; mwandiko wa Britanicca unafahamika humu JF.
Kama kawaida yake ya kuuza jina, kakuuzia wewe ulete uchafu hapa, bila shaka bila ya yeye kujali.

Sasa tueleze, nimechukua tu hicho kipande kimoja tu hapo juu kama mfano wa mtindio wa akili yako ulivyo. Tueleze ni jinsi gani CHADEMA walikuwa wamejisalimisha kwa Magufuli?

Britanicca, huu u-mercenary wa kuuza jina unakuvunjia heshima uliyokwishajijengea hapa. Unaporuhusu hata takataka ziletwe kwa jina lako, sijui wewe mwenyewe unajisikia vipi unapozisoma.
 
Unajichanganya mwenyewe.
Samia kakwambia anaitaka katiba mpya, au nalo ni moja ya mazingaombwe mengine utakayoleta hapa siku nyingine kuchezea akili za watu!
 
Huwezi kuongeza nchi bila ya kuwaumiza watu kwa maslahi ya nchi na watu
 
Ndugu Tundu Lissu ni "bwakubwaku".....

"Too much know" asiye na ulimi wa nidhamu wala heshima.....

Si kila MTANZANIA anaihitaji katiba mpya.....
Nakubaliana na wewe kwa 100% yule bwana ana dharau sana halafu ni mfitini kwelikweli nakumbuka katika kampeni zake za uraisi badala ya kunadi sera anaishia kum attack Magufuli personal..
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 


Rais Samia kitendo cha kutaka kukutana au kuongea na Lisu kilikuwa ni kitendo cha kiungwana Sana. Kama kweli Lisu aligoma si Jambo la kistaarabu kabisa. Kwsbb ata Kama ni mwanamke lakin tayari ni raisi wa nchi. Lisu angemsikiliza....

Lisu Kuna vitu vingine anafanya lakin ukweli kwa watu walio soma Saikolojia watagundua anaweza kuwa kwenye group la abnormal psychology.

Founder of abnormal psychology , Mr Sigmund Freud (1886), watu Kama Lisu anawaweka kwenye group la Psychotic disorders that cause abnormal thinking and perceptions.

Unakuta mtu ana mental disorder ambayo hamzuii kufanya shughuri zake Kama kawaida, Ila hizo shughuri zake ukizichunguza kwa undani zinakuwa na sintofaham nyingi...

Kwa maoni yangu, naona Lisu angeiga mfano wa kama mbowe mwenyekiti wake, pamoja na mambo mengine, mbowe ana Hekima sana ata ya maneno!!

Sasa Kama alimdharau Mama, na Hawa wenzetu ukisha wadharau tayari unawaletea inferiority comp. Wana Anza kuwaza why thz or becouse I am.......

Ila kama mtoa mada umesema kweli, Mama yetu Rais Samia, tunaomba usichape wapimzani wote kwsbb ya mental disorder ya mmoja.

Mchape huyo tu... Busara itumike. Wee mtu Kama Siro anaweza kushaur raisi nn? Mtu ambaye Hamza alikosea yeye akashambulia uzao wa wazaz utafikiri yeye hazai!!!
 
Samia amekuja naye atapita tuu kama wengine, anaweza kuwa kikwazo cha muda mfupi kwa katiba mpya, lakini at the end of the day wananchi ndio wataamua na sio CCM hiyo siku inakuja, CCM mnapoteza muda tuu kupigana na hii issue ya katiba na wahenga walisema haki ya mtu haipotei bure, ile tume ya wizi wa kura,polisiCCM na misheria kibao ya ovyo mliyojiwekea kuendelea kutawala yatakwisha, aliondoka mkoloni itakuwa CCM
 
Nakubaliana na wewe kwa 100% yule bwana ana dharau sana halafu ni mfitini kwelikweli nakumbuka katika kampeni zake za uraisi badala ya kunadi sera anaishia kum attack Magufuli personal..
Juzi Ushetu kulikuwa na mgombea wa Chadema?
Lissu alikuwa anasema madhaifu ya mgombea mpinzani mlitaka amsifie?
 
Wakati mwingine vizuri kujipa faraja ili upate japo lepe la usingizi. Lakini ukiamka ukweli unakusubiri kwamba hii nchi siyo yenu pekeenu. Nyie hamna nguvu kubwa kuliko waliyokuwa nayo makaburu. Ndio maana mmebaki kuvizia akina mama wanaokwenda jogging kwa afya zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…