Tunakwama wapi? Malawian Airlines (ndege 2) Vs Air Tanzania (ndege 11)

umeongea kitalaam kabisa,sijajua kwann ATC wanashindwa kuwa na international destn. Hizi 787 hawazitendei haki kabisa,wanafeli wapi sijui!!
Hizo destination zote tajwa hapo juu ATC tayari wanazo labda kuongeza zaidi utilization hasa wa hizo B 787 ulizotaja.
 
Nafikiri tunashare some commons
But nasikitika jamii yangu sehemu kubwa ipo kwenye “vacuum”
 
ATC wangechangamkia DAR-JNB- (with a stop in LSK/HRE then DAR) Wangepiga hela sana
 
Wewe umenishangaza sana. Umeweza kutafuta data za Malawian Air lakini umeshindwa kuzitafuta za ATCL.

MAJUNGU katika ubora wake.

ATCL kwa sasa inaenda Comoro, Lusaka, Zimbabwe, Mumbai, Guanzhou, Entebbe, Bujumbura na mwezi huu wanaanza kwenda Nairobi.

Kwa siku ATC inapiga flights si chini ya 30 ndani na nje ya nchi. Hao Malawian Air wataweza kufika idadi hiyo kwa huto tundege tuwili!?
 
Punguza vijembe Dada. Tulia soma tena ukiwa umetulia.
 
ATC ni Zaid ya ilivyo Sasa. Wapunguze matumizi. Ule mjengo pale Mjini wote wa nn? Wakodishe sehemu, wapunguze wafanyakazi baadhi ya service ya wa"out source". Wafikirie kufanya CODE SHARING na leading airlines, loyalty programs etc.
 
Unajua ukiwa muongo elewa na uelewa .wa wenzako. Route za ATCL nje ninanvyofahamu ni Mumbai, Lubumbashi, HRE, LSK, Comoro, Ndola, Bujumbura, Entebbe, Nairobi kuanzia kesho, Guangzhou ipo na hata Joburg ipo! Ungeweka na 8dadi ya abiria wa Malawi ingesaidia
 
ATC ni Zaid ya ilivyo Sasa. Wapunguze matumizi. Ule mjengo pale Mjini wote wa nn? Wakodishe sehemu, wapunguze wafanyakazi baadhi ya service ya wa"out source". Wafikirie kufanya CODE SHARING na leading airlines, loyalty programs etc.
Twiga miles kwa kiingereza ndio loyalty programme !
 
Hahahahaha
 
Kiwango chetu cha upumbavu kimeenda juu ghafla, watu wanakuja na hoja za kitoto. Unafikiri kwenda International ndio kutengeneza profit? See how big is our country, compare it with Malawi halafu tafakari upumbavu wako.
Kwa hiyo dreamliner Inaweza kuzunguka hapa ndani ikatengeneza profit?
Wacha ushabiki wa CCM wa kijinga kisa tumbo
 
Unajuwa ni ukweli hatuna business plan lakini haina maana basi tukae kimya tuweke hili sawa. Biashara ya ndege ngumu sana na hasa ukijuwa kuwa mashirika makubwa kama EK,Qatar, Fly Dubai na hata Ethiopia ukiacha mashirika kama Kenya na Rwanda ushindani mkubwa. Kushindana na hawa ngumu ila unaweza kuwa feeder wa hizi kampuni kwa kuingia share code kufanya route nchi ambazo mashirika haya hayafanyi biashara kwenda kwa maana mtu anakata ticket toka comoro to Dubai kama ticket moja air Tanzania na Emirates au Fly Dubai au Qatar hili moja lingine kama unataka kushindana kivyako basi bei zako ziwe chini kiasi mtu anaona ndio EK shirika kubwa lakini AIr Tanzania hapa na save dola 200 washinde kwa bei zako ila best way kuungana nao sisi kuwa feeder wao kuwaletea wateja Dar kutoka mfano Lubumbashi, Bujumbura sijui Comoro na miji ambayo hawana huduma hizo na flight time schedule ivutie kwa maana transit muda mchache. Maarifa tu ya kupanga ratiba za ndege kama feeder.
 
Zanzibar tupewe mgao wetu kwenye hizo ndege. Kila mtu akapambane kivyake. Mambo ya kuja kulaumiana baadae hatutaki kwenye hizo ndege 11 sisi tupeni zetu 5 tutapambania Watalii waje Unguja
Huko sahihi, sisi wadanganyika malofa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…