mbu wa dengue
JF-Expert Member
- Jun 2, 2014
- 8,860
- 11,554
Tuna kasumba ya uoga kwenye kila tukio,sio hili tu peke yake.Hii ndio Tanzania......na watanzania ni watu wanaopenda ngono sana. Uliona kelele nyingi sio kwamba tukio lile liliwaumiza bali lilizua hisia za ngono ndio maana likasambaa sana.
Kama unadhani liliwaumiza mbona hatusikiii kelele za Haki itendeke?
Mimi nilitegemea mawakili wangekuwa mstari wa mbele kwenye kila hatua ya kesi na kutupa taarifa wananchi kwamba sasa hivi kesi iko mahali fulani na ipo kwenye hatua fulani,pia wananchi tutaomba ushirikiano wenu endapo tutakwama kwenye hatua fulani iwe kipesa au kivyovyote.
Lakini cha ajabu hakuna mwenye uhakika wote tulibaki tunakisia tu kwamba huenda walishikwa au huenda waliachiwa au huenda walikamatwa watu wengine tofauti.
Mbona kwenye kesi za wakina mdude nyagali huwa zinafuatiliwa hatua kwa hatua na wananchi wanashirikishwa na kuchanga pesa chapchap iweje kwenye hili kila mtu anaongelea shimoni.