Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Mada nzuri hii, vema kujikumbusha,itatusaidia pia kuunganisha dots za yanayotokea leo!

kweli kabisa.

kwa mfano nani alikuja kuwa waziri mkuu immediately baada ya Moringe? Kwa nini?

mfano: ulikuwa ni utashi wa nyerere kwamba Mwinyi awe Rais mtarajiwa au Nyerere alishinikizwa?
 
Tuendelee kujikumbusha zaidi.........

 
Kumbe ndiye aliyesababisha watu wamwage sukari mtoni badala ya kuwapa watu...

Huyu sokoine alikuwa hafai, wala haelewi kati kazi binafsi na kazi ya umma..

Huwezi kulazimisha wafanyabiashara kugawa bidhaa kwa wananchi kwa bei uipendayo..

Basics of the business..alikuwa mweupe sana.
 
Tunaye Sokoine aliye Hai- EL, kijana, mchapakazi, mmasai. Anajua kutoa maagizo na kufuatilia. Huchukia mambo yakienda vibaya. Si unaona anavyosimamia ujenzi wa madarasa?

nani kasema Lowassa ni mmasai? hizi propaganda ndizo zinazomfanya asijihamini kule Monduli kwani wamasai wanamjua na ndiyo maana hununua wapinzani kila uchaguzi..huyu bwana mkubwa ni Mmeru au mchagga na siyo mmasai
 

Yule mkimbizi fara dereva wa gari lililosababisha ajali sitakaa na kumsahau kwa jina: Anaitwa Dumisan Dube yani hata leo kama bado yupo hai na yeye akiletwa ktk wale wakongwe wa rika lake hata kama amezeeka vp nitamtambua kwa sura tu. Hata kama anatembea kwa mkongojo.
 
Sioni cha kumsifia mtu ambae alikuwa akitekeleza mfumo wa kuididimiza Tanzania shimoni.

Kifo ni kifo na zingine hubaki kuwa ni sababu. Lakini ukitazama kwa makini kifo cha Sokoine kilisababishwa na ajali barabarani, Barabara walioshindwa kuijenga (Yeye na Bosi wake) na ilikuwa mbovu kiasi haipitiki kwa usalama.

Alisababisha watu wengi kutiwa ndani na kufia jela bila hatia. Eti uhujumu uchumi, huo uchumi wa kuhujumiwa ulitokea wapi? wakati hata kandambili zilikuwa hakuna? watu tunavaa "makata mbuga".
 
jamani embu mtujuze ukweli kuhusu kifo cha edward moringe sokoine wengine ndiyo tulikuwa wadogo wengine hata kuzaliwa ilikuwa bado wenye kufahamu watujuze
 
Umafia ndani ya ccm ndiyo ulisababisha kifo chake,uchu wa madaraka
 
likufa kwenye ajali ya gari. Akiwa anatoka Bungeni Dodoma gari lake liligongwa/liligongana na gari lililokuwa linaendeshwa na Mkimbizi mmoja toka South Africa akiitwa Dumisan Dube. Kuna theory zingine ambazo hazijathibitishwa kama hiyo hapo juu No. 2
 
Hata mimi hili sili elewi vizuri juzi juzi hapa nilikuwa na kundi la wastaafu katika story za mauji nchi wakamgusia sokoine...mstaafu wa magerza alitamka kuwa ndani ya gari ile alikuwapo EL....baada ya kugngana wali mmalizia kwa risasi...aliemuua alikuwa huyo bwana EL...NA huyo mzee kila ukimtaja EL anakwambia huyo alimuondoa mwenzake huyo.... anaejua ukweli wote embu atufungue macho naona xyz nyingi mno................
 
Ngoja wadau watakuja!!

Huyu alikuwa kamanda wa ukweli!
Nahisi hatatokea ndani ya sisiem mpiganaji kama huyo kamwe!
 
Nendeni mkamuulize profesa shaba anajua ukweli . Yeye ndo aliufanyia uchunguzi mwili wa sokoine .
 

hiyo siyo kweli dada . Haiwezekani pm afe mkuu wa kaya asijue . Tafiti zaidi utajua ukweli.
 
Kuna sredi ya long time hili swala lilijadiliwa mno . Lipo kwenye upande wa intelejensia.
 
Acheni kumung'unya mchonga anahusika kwa asilimia 100 ya kifo cha sokoine.Mzee kadedisha wengi sana alikuwa dikteta
 
,Edo,alitaka cheo cha katibu mkuu wa CCM kipigiwe kura na siyo mtu kupewa bila ya idhaa ya wananchi! unajua wakati ule katibu mkuu wa ccm alikuwa mara mbili ya waziri mkuu kwa cheo.

mshikaji wake Yona mwakasendo naye alipigwa sindano ya sumu ! nakuambia heri kufa kwa ukomunisti maana nchi hii ilikuwa inatisha kwa watu kupotea kisirisiri. wewe ona kifo cha kanali Andrew Shija mpaka leo hakieleweki! KIfo cha koliimba kutetetmeka katika spika wakati anajieleza! KIfo cha sokoine kupata ajali hakieleweki!

Haya yote yatakuja eleweka tuu na wahusika kuanikwa wazi wapende wasipende!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…