Tunamuimba Rais kila kona, Je, yupo kwenye mioyo ya Watanzania Au mtaamua kufumba macho?


Lakini pia usisahau aina ya wabunge waliopitishwa Kwa nguvu 2020 chini ya JPM.

Angalia wale waliopita kwa mbinde kama Bashe wako smart sana na hata uwaziri wanautendea haki. Wengine hata uteuzi wa Mawaziri unampa kazi sana Mama SSH. Yaani kupata Mawaziri na MANAIBU WAZIRI ni ngumu sana mana wabunge waliopo ni tatizo sana.

Ndio Sasa tutaona umuhimu wa kuwa na katiba inayotenganisha Ubunge na uwaziri. Nje ya wabunge wapo watu wengi sana wenye uwezo na ubunifu kuliko wale wabunge waliopata Ubunge Kwa kuruka sarakasi na kutumia wasanii wa miziki kutangaza sera za kukata viuno majukwaani badala ya sera. Wote walikuwa hawawezi kuweka mdahala hata sekunde Moja na kupambanishwa na magwiji wa siasa kama akina Rwaitama , Shivji , Ulimwengu na wengine . Tukapata wabunge wa ajabu na Mawaziri wengi wakawa hawana uwezo zaidi ya kujikuta wameogelea kwenye pesa za tozo na Uvico.
Ulimuondoa Bashe na Nape, Mawaziri wengine ni wakutafuta na tochi.
 
Kwako wewe yupi ana unafuu?

Mimi JPM maana kipindi cha uomgozi wake ndy nilitoboa maisha na sasa hivi ndy natembelea rim.. mwalimu kashasha hapa,vp kwako Jesse John?
 
Huyu mama yupo moyoni mwa mafisadi na wapiga dili nchini!!!
Nilimdharau alipotumia fedha za covid 19 kujenga madarasa nchini halafu wakati huo tozo JUU!
Tusubiri hatma!!
Huwa kuna kauli zinanichekesha sana; ninapomuona choka mbaya akimtamkia, 'ninamdharau sana', mtu aliyemzidi kila kitu tangu kitambo sana huwa nacheka sana!
 
Haaaahaaa sasa mkuu samaki utaibaje?, Ila huko ziwani au Bahraini wavuvi huwa wanaibiana taa au betri mkuu.
 
Mitandaoni MNA 7 Kwa 0

Nje ya mitandao mno 0 Kwa 100!

Endeleeni!!

Unasema JPM Alifanikiwa kuwahadaa watu wakati wana macho ya kuona na masikio ya kusikia....?

Mnamdanganya sana kiongozi wetu, Hakubaliki Kwa 90% ila anaomuda wa kurekebisha!!

Vijini ile sabuni ya mche kipande kilikuwa kinauzwa mia mbili, Kwa sasa ni 700 halafu unataka akubalike??

Jinga kabisa
 
Hivi unajua hadi vikongwe wa huko vijijini hawaitaki ccm na hasa Rais aliyepo???

Hawataki kusikia jina lake hata kidogo, na limenishangaza hilo Kwa sabb vikongwe wengi wa nchi hii ilikuwa ukiwaambia vyama vingine ilikuwa ni rahisi Kwa wao kusema eti tunataka kuleta vita kuondoa amani iliyoachwa na Mwalim Nyerere!!

Nenda sasa vijini uwaulize hilo mdo utapata majibu yao!!
 
nimegundua mda huu humu JF kuna watu mnalipwa kuzungumzia vibaya utawala wa awamu ya 6 maana ni uzi juu ya uzi kumparura bimkubwa tu bila point!! imekuwa too much mnaboa sasa!!

hamna stori zingine wakuu? hata Mayele kuifunga Simba jumamosi na wananchi kutetema hamzungumzi? au Miwani Makengeza bin Mmbowe kupagawa na Joyce hadi kuanguka na kupasuka kule Dodoma nayo imeekaaje?
 
Sera zipi ziliwasaidia hao maskini kuepukana na umaskini wao?

Taja sera zilizobadilishwa.. Hao maskini hawana mchango wowote kwenye uchumi zaidi ya ulalamishi usio na msingi..

Jiwe aliwapeleka wapi hadi waseme hivyo? Walipata ahueni kwa kuwa served na nature zaidi kuliko Utawala kufanya mambo ya kuwasaidia..

Hakuna anaeweza eleza bayana maskini walivyosaidiwa awamu ya 5.
 
Wenyewe wanasema ni miongoni mwa watu 100 duniani wenye ushawishi. Ngoja tusubiri 2025 kama atagombea tuone atatushawishi nini.
Magufuli alishapanda mbegu ya kunajisi box la kura. Hivyo hakuna kiongozi mwingine yoyote wa CCM atategemea tena kushawishiwa wapiga kura, zaidi ya kupendelea vyombo vya dola ili vimlindie uchaguzi wa wizi.
 
Wakaswma wanataka chama gani au wanamtaka nani? Weka jibu maana na mimi ninalo jibu .
 
Kwako wewe yupi ana unafuu?

Mimi JPM maana kipindi cha uomgozi wake ndy nilitoboa maisha na sasa hivi ndy natembelea rim.. mwalimu kashasha hapa,vp kwako Jesse John?

Kama ulikuwa kwenye lile kundi lake la watu wasiojulikana ilikuwa lazima utoboe. Kwa sasa kundi lenu bibi mkojani kalipotezea.
 
Yaan mi nikishaona mtu akisema mfumuko wa bei ni kutokana na vita ya ukraine naacha kumsikiliza naona kama hana akili sawa sawa!!..
Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 za africa ambapo mafuta n ghari zaid na ziko nchi 54
hyo vita inapiganiwa tz?
Itakuwa vita vya Ukraine na Russia vinapiganiwa Dodoma
 
Nimewahi kushuhudia asubuhi asubuhi akina mama wakimshusha kwenye bajaji mwanaume mmoja aliyejifanya anamsifia Mama. Kisha wakamwambia dereva, aendeshe watamlimpia waliyemshusha!
 
Ni sukuma gang hao wako busy kutafuta justification ya kupachika jizi lao jingine.
Ni lini utaacha ujinga huu wa kudhani kila asiyekubaliana na mpakwa mafuta wako ni sukuma gang?

Kama wote wasiokubaliana na Sera zake ni sukuma gang, basi ni hatari mno, maana ni wengi mno, na kama wewe ni mshauri wa mama, ni miongoni mwa washauri wabovu kuwahi kutokea, au mmeamua kumdanganya mama
 
Nilikuta kijiwe kimoja kina Mama wauza vitafunwa daa wanavyolalamika mmm niiashangaa mpaka huku ,nikauliza mbona nijinsia yenu kwanini asipewe ushirikiano wee walipinga haswa, sisiemu ni wale wale wanajuana kwa vilemba, mwingine eti tuongeze lugha nyingine, mwingine wanawake tukae kwenye bodaboda upande utazani hizo barabara kaziwekea lami wakati zimejaa mashimo
 
You can be a fool but you can't fool us.
 
Kwakweli mimi SSH yupo moyoni mwangu kabisaa, kuroho safi. Namwombea afanikiwe maana mafanikio yake ndio mafanikio ya nchi.

JPM alikuwa na mazuri yake lakini dah... Ile ilikuwa noma.
Unamwelewa kwa lip? Na je mafanikio gani ambayo we umeyaona machinga walio wengi kuondolewa na mkafurahishwa wachache wenye vyeti feki
 
Hapendwi huyo mama!! Elewa tuu hivyo, sasa kazi ni kwako kuita watu sukuma gang
Kuwa Rais haihitaji kupendwa ila kinachotakiwa ni ku deliver..

Nyerere aliwahi waambia wajinga kama wewe kwamba kama unampenda mtu nenda kanywe nae chai sebuleni kwako..

Na mimi nakwambia wewe kama unapendwa nenda katege buttocks kwa unaempenda ..

Mwisho mbona humtaji anaependwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…