1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
JPM alifanikiwa kwa propaganda zake za kiwaita watu wanyonge huku akinuonga kila aliyejaribu kwenda kinyume naye. SSH anapiga propaganda za kurudisha hali kuwa shwari huku akiwaaahidi wafanyabiashara na matajiri hali nzuri ya uchumi. Ukiangalia kiundani wote hawa hakuna zaidi ya wanachofanya zaidi ya kutengeneza matatizo kisha wao wenyewe wanajifanya kutoa suluhu.
Lakini pia usisahau aina ya wabunge waliopitishwa Kwa nguvu 2020 chini ya JPM.
Angalia wale waliopita kwa mbinde kama Bashe wako smart sana na hata uwaziri wanautendea haki. Wengine hata uteuzi wa Mawaziri unampa kazi sana Mama SSH. Yaani kupata Mawaziri na MANAIBU WAZIRI ni ngumu sana mana wabunge waliopo ni tatizo sana.
Ndio Sasa tutaona umuhimu wa kuwa na katiba inayotenganisha Ubunge na uwaziri. Nje ya wabunge wapo watu wengi sana wenye uwezo na ubunifu kuliko wale wabunge waliopata Ubunge Kwa kuruka sarakasi na kutumia wasanii wa miziki kutangaza sera za kukata viuno majukwaani badala ya sera. Wote walikuwa hawawezi kuweka mdahala hata sekunde Moja na kupambanishwa na magwiji wa siasa kama akina Rwaitama , Shivji , Ulimwengu na wengine . Tukapata wabunge wa ajabu na Mawaziri wengi wakawa hawana uwezo zaidi ya kujikuta wameogelea kwenye pesa za tozo na Uvico.
Ulimuondoa Bashe na Nape, Mawaziri wengine ni wakutafuta na tochi.