Tunamuimba Rais kila kona, Je, yupo kwenye mioyo ya Watanzania Au mtaamua kufumba macho?

Tofauti ya Samia na magufuri ni,Samia anaumiza wengi ananufaisha wachache,magufuri kiuchumi wengi wa chini walinufaika wachache waliumi hasa majizi,alijitaidi kudhibiti mifuko ya Bei hata kipindi Cha covid 19
Sio kweli.
 
Sisi tumekubali kwenda na Rais Samia. Hao Raia wa Hali ya chini na wao waende na rais wanayeona anafaa. Full stop tuache kupigiana makelele
Hahaa, kauli tata hii, ninyi ni 10% wa kipato Cha chini ni 90%.
Atatoboaje sasa!! Kama Bado mnawaza goli la mkono TUMESTUKA. Tunataka KATIBA mpya kabla ya uchaguzi wowote.
 
JPM anakubalika na watu kitaani SSH anakubalika mitandaoni ndio tofauti kubwa .
Sema anakubalika na wanaharakati wa mtandaoni lakini sio watu wa kawaida wanaotumia mitandao
 
Hahaa, kauli tata hii, ninyi ni 10% wa kipato Cha chini ni 90%.
Atatoboaje sasa!! Kama Bado mnawaza goli la mkono TUMESTUKA. Tunataka KATIBA mpya kabla ya uchaguzi wowote.
Wakati wa Magufuli bado hiyo 10% ndio ilitawala na itaendelea kutawala.

Ule wizi wa uchaguzi ulikuwa wa nini kama ana sapoti ya 90%?
 
Gharama za maisha mbona kitu cha kawaida tu. Fanya kwzinuweze kuzimudu acha kulalamika.
 
Ila kuhusu kupanda bei, vitu vimepanda kabla ya Vita. Labda tuseme sababu ya corona
 
Makasiriko ya Chief Hangaya pale alipogundua kuwa Watanzania wengi hawampendi wala hawako nae😁😁😁
 
Wakati wa Magufuli bado hiyo 10% ndio ilitawala na itaendelea kutawala.

Ule wizi wa uchaguzi ulikuwa wa nini kama ana sapoti ya 90%?
Unanikumbusha Ile kauli ya bibi Eti ''CCM ITASHINDA HATA KAMA HAITAPIGIWA KURA!""

Hoja ingine ni kuwa mnakiri kuwa JPM aliingia Kwa kuiba uchaguzi, Alieiba uchaguzi ameondoka bt alioingia nao ktk WIZI huo wapo, Kila kosa wanamtupia asieweza kujitetea.

Kama kiongozi atashindwa kuwin trust ya watu wa kipato Cha chini ambao ni 90% bas asitegemee uchaguzi huru na HAKI lazime awaze kuiba tu. TUMESTUKA, SANDUKU LA KURA limetiwa najisi.

KATIBA mpya tunaitaka kabla ya UCHAGUZI wowote. AMEN
 
Unachukia madarasa kujengwa? We mbinafsi sana.
Mkuu
Sichukii madarasa kujengwa

Wabunge walipitisha Tozo zitumike kujenga vituo vya afya na madarasa

LAKINI fedha za uviko zikatumika kule kule tena!!
Ndugai akauliza ikala kwake

Hatuambiwi tena tozo ni sh. Zimekusanywa na zinafanya Nini!!!

Bora tozo zingepelekwa KWENYE mafuta kuliko kukopa tena KWA ajili ya mafuta ingewasaidia Sana watu na vitu kupanda bei!!!
 
Akisitisha hiyo miradi Pro JPM watamnanga mpk basi.. wacha aimalizie tu ingawa ni kweli hiyo miradi ni mzigo kulinganisha na hali ya uchumi ya sasa dunian
 
Magufuli alishapanda mbegu ya kunajisi box la kura. Hivyo hakuna kiongozi mwingine yoyote wa CCM atategemea tena kushawishiwa wapiga kura, zaidi ya kupendelea vyombo vya dola ili vimlindie uchaguzi wa wizi.
Kabla ya Magufuli mlikuwa mnshindwa kihalali eti ee?
 
Hahaa, kauli tata hii, ninyi ni 10% wa kipato Cha chini ni 90%.
Atatoboaje sasa!! Kama Bado mnawaza goli la mkono TUMESTUKA. Tunataka KATIBA mpya kabla ya uchaguzi wowote.
10% Vs 90% kazi kweli kweli !!!
 
Matajiri ndo kila kitu dogo. Ukikumbatia maskini na nchi unakuwa maskini mwisho wake unakuwa rais kupinduliwa kwa sababu hataweza kulipa mishahara wanajeshi kama ambavyo tulikuwa tunaelekea kipindi kilichopita Cha jpm.
 
Kama ulikuwa kwenye lile kundi lake la watu wasiojulikana ilikuwa lazima utoboe. Kwa sasa kundi lenu bibi mkojani kalipotezea.
Ni ujinga kufikiri kila rangi inayong'aa ni nyeupe ukiwa kwa mbali kisha ukaishia kuridhika na na vile unavyodhani..ni busara kusogea karibu ili kujiridhisha na kuwa na uhakika usio na mawaa!!

Upo mbali na vile unavyodhani..asante
 
Aliyeongeza mshahara kwa 23.3% huyo ndo yuko moyoni mwangu. Samia Suluhu Hassan atosha
Kuongeza mishahara ni jambo zuri. Watumishi wote walioajiriwa na Serikali wanaonufaika na ONGEZEKO Hilo Kwa Takwimu hawafiki Lak 5, au 500,000.

Wakulima na wachuuzi Kwa Takwimu Nchi hii ni zaidi ya 80% katika idadi ya wananchi zaidi ya 50milioni.

Mbolea imeongezeka Bei Kwa zaidi ya 250%, Bei za mafuta ONGEZEKO lake ni zaidi ya 300% ukilinganisha na Bei za march 2021. Impact ya INFLATION hiyo Kwa Bei ya vitu mtambuka ni mbaya sana ktk UCHUMI.

Kwanini Serikali haiwazi kupunguza MATUMIZI yake inawaza KUKOPA kutatua matatizo halafu nani alipe??

Bado tunasikia Kuna WIZI wa fedha katika miradi mbalimbali ya serikali ktk wakati ambao kuko kwenye tatizo la kifedha kama Nchi. Kwann Viongozi Si wakali Kwa waizi?? Ripoti ya CAG why imetupwa kapuni?

Mnatoka KUSIFIA wakati tatizo KUBWA halijatatuliwa, tunaokosoa ndio tunaosaidia Nchi kuliko ninyi wenye VISION finyu, kiongozi wetu Bado anayo KAZI KUBWA ya kufanya Bado, msimpotoshe.
 
Tofauti ya Samia na magufuri ni,Samia anaumiza wengi ananufaisha wachache,magufuri kiuchumi wengi wa chini walinufaika wachache waliumi hasa majizi,alijitaidi kudhibiti mifuko ya Bei hata kipindi Cha covid 19
Magufuli alinufaisha wengi akina nani? Aliwanufaisha kwa lipi? Lipi jipya alikua anafanya viongozi waliopita hata wakoloni hawakufanya?
 
Magufuli alinufaisha wengi akina nani? Aliwanufaisha kwa lipi? Lipi jipya alikua anafanya viongozi waliopita hata wakoloni hawakufanya?
Hukunufaika wewe sisi wafanyabiashara alitusikiliza na kufanya Kaz ushauri wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…