CONTROLA
JF-Expert Member
- Sep 15, 2019
- 7,001
- 23,449
Asante,yalishapita nampenda mama sana.Pole sana na hongera kwa kuvuka majaribu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante,yalishapita nampenda mama sana.Pole sana na hongera kwa kuvuka majaribu
Muhimu usijibizane nae tu huwezi pata radh kama unamtendea wemaMpaka hapa navumilia mengi nikiongea vyote havitoshi
inauma inauma lakini maneno hayaui wala hayatoboi,unasikiliza linaingilia sikio hili linatokea kule yani hamna kuhifadhi kitu moyoni.Inauma sana kuona mtu ambaye kila mtu anamkimbilia na kumuamini wewe anakwambia angejua wakati anakuzaa angebana miguu ili ufe kabisa.inaumiza sana.
Ikiwa huna makosa, radhi sijui laana haikupati....
Na wazazi wetu wengi hawana neno shukurani.
.....
Sent using Jamii Forums mobile app
Mama yangu nakuomba sana usijekuwa kama mama yake cc pisi kali maana sijui itakuwaje ila pole sana dad kwa unayopitia ila ushauri wa controla n mzur zaid
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama Laana zingekua za kweli na zinamfikia mtu basi leo hii mimi ningekua naokota makopo njiani,nazurura nadondosha mate naongea mwenyewe njia nzima.
Mama yangu alishanitamkia maneno magumu na mfano wa 1 ambalo nalikumbuka mpaka na kesho aliniambiaga "wewe najuta hata kukuzaa ,natamani ile siku nakuzaa ningebana miguuu ufe kabisa"
asee mimi hamna laana sijatamkiwa na mama,ila nikwambie kitu mamilooo "kaza buti songa mbele" huyo si mama ako sasa huyo ni shetani anaemtumia mama.
Nakwambia hivyo kwa sababu yule mama angu aliyenilaani mimi,na mimi nilimwambiaga MUNGU kuanzia leo MUNGU nakwambia kwa mdomo wangu kuwa SINA MAMA nitajihesabu nina baba tu.
basi nili m cancel mama nikawa staki story zake wala kumsikia,Nilipambana nikasema siku 1 ataniona kwenye tv ama kunisikia kwenye radio ama kunisoma kwenye gazeti,kisha nika kaza zangu Mama yangu akawa MUNGU nikitaka kitu namwambia MUNGU nikitaka kudeka namdekea MUNGU yes ndio alikua mama yangu.
Baada ya miaka mi 5 siku 1 nipo ofisini natoka nafata gari nisepe zangu nilimuona mama yangu akinifata kwa Magoti akitokea getini akiingia huku analia unajua nilihisi ni movie ya kihindi au macho hayaoni,nilifikicha macho kuangalia vizuri yes ni Mama controla.
anakuja kwa magoti analia kwa uchungu "nisamehe mwanangu" hakua anatamka neno jingine zaidi ya "nisamehe mwanangu" asee unajua ile kum miss mama muda hujamuona then mnakuja onana mama anakulilia umsamehe.
Mimi ni nani nisimsamehe mama asee ile siku tulijaza Raia pale nnje maanaa nililia kama mtoto mama alilia kama mtoto,ni mzee mmoja alikua kutubeba na kutupeleka ndani na kuanza kazi ya kutunyamazisha.
Mama yakaisha na hadi leo nilipofika asee zile laana zilikua kama KICK ya kunipitisha,pamoja na changamoto zote ila nakwambia Sina siku nililala njaa,sina siku nilikosa nguo,sina siku nilikosa sadaka kanisani,Mungu alikua MAMA kwangu.
Huyo mama yako si yeye nakwambia tena si yeye mtambue shetani na hila zake kisha mwambie hakuwezi nakuhakikishia usiponasuka kwenye huo mtego wa MAMA umepotea. Kunja sura kaza mwendo songa mbele mwambie live mama "siwezi" mwambie "sina" mwambie "nipo vibaya" Akikulaani tu, KATA Mawasiliano nae.
Saa zingine kuwalinda watu tunaowapenda zaidi ni kukaa mbali nao.
Mama yupo tu hafi leo wala kesho so usimuendekeze hata kidogo,kaza buti asikuyumbishe hata kidogo atabaki kuwa mama na milele utamuheshimu ila ktk swala la yeye kukurudisha nyuma "USIKUBALI" kataa kwa maneno na vitendo.