Tunaopitia hii changamoto tupeane ushauri

Tunaopitia hii changamoto tupeane ushauri

CONTROLA,
Inauma sana kuona mtu ambaye kila mtu anamkimbilia na kumuamini wewe anakwambia angejua wakati anakuzaa angebana miguu ili ufe kabisa.inaumiza sana.
 
Endapo utashindwa kumcontrol kwenye hizo ishu za hela hakika utasumbuliwa sana mbeleni. Kwa kuwa ushaelewa mama yako ni mtu wa aina gani, ishi nae accordingly. Anapoomba kila wakati na unampa anazidi kupata kiburi na kuona zipo. Siku ukipata kazi utajuta, maana kila siku atakuomba hela. Ifike mahali hata kama unazo anapoomba usimpe, muache aongee tu so long as hataongea maneno mapya yote yatakuwa ni yale yale.
 
Inauma sana kuona mtu ambaye kila mtu anamkimbilia na kumuamini wewe anakwambia angejua wakati anakuzaa angebana miguu ili ufe kabisa.inaumiza sana.
inauma inauma lakini maneno hayaui wala hayatoboi,unasikiliza linaingilia sikio hili linatokea kule yani hamna kuhifadhi kitu moyoni.

mtu anayeweka yale maneno (laana) za wazazi moyoni ndio huwa wengi huamini wamelaaniwa na kweli hawafanikiwi kwasababu akili yake imeshajijenga kalaaniwa.

Ataanzisha biashara ya kuuza miguu ya kuku na vichwa kisha ataenda kukodi frem MASAKI,automaticaly hatopata wateja biashara itamdodea,alivyomjinga atasema kimoyo moyo (mimi nimelaaniwa mimi)

Wakati shida ni yeye kafungua biashara sahihi ila kaipeleka kwa watu wasio sahihi,yeye angepeleka biashara yake hiyo akakodishe frem Buguruni au tandale kwa tumbo huko halafu auze miguu ya kuku na vichwa tuone ile laana kama itafanya kazi.

Laana ni itafanya kazi kama ukiamua kui ishi hiyo laana ila mimi nasema Hamna Laana duniani labda ashuke Mungu Live nimuone ndio ntasema kuna laana,ila hakuna mwanadamu wakuweza kukufanya usifanikiwe au uishi bila amani kisa tu ya ulimi wake na maneno yake HAKUNA na hayupo huyo mwanadamu chini ya JUA.
 
Kwenye koo yenu hakuna wakubwa???
Waendee uwaeleze..watamwita watamsikiliza na wewe utasikilizwa.Hapo watajua tatizo liko kwa nani...!
Nimesikiliza upande wako tu bado upande wa mama..Kwa hivyo swala la mama kukushauri ni ngumu sana.Mpaka nimsikilize nae mama.Nadhani unaujua upendo wa mama?

Shukuru kwa elim ya st.kayombo ulioipata nyuma ya mgongo wa mama....usipoweza kushukuru kwa kidogo uwez shukuru kwa kikubwa...asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama yangu nakuomba sana usijekuwa kama mama yake cc pisi kali maana sijui itakuwaje ila pole sana dad kwa unayopitia ila ushauri wa controla n mzur zaid

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ambition plus,

Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake!!! Namshukuru kwa mengi tu sio elimu tu pia kunizaa kunilea na mambo mengine mengi lakini haileti sababu ndio iwe fimbo ya kunichapia, namshukuru na bado naendelea kumshukuru na kumpenda

Nikiwa charts zetu hapa kila mtu atabaki akishangaa ni mama wa aina gani

Anyways

Nimepokea ushauri wote hopeful nitayafanyia kaZi kwa uwezo wa M/mungu
 
Ngoja niandike kwa herufi kubwa labda unaweza nielewa ;


TENDA WEMA USIOKUUMIZA...

Muheshimu Mama ila Usimuogope , kwa jinsi unavyomuogopa na kuwa na hizo mindset za laana unajiweka kwenye mazingira magumu ya kuathirika kisaikolojia halafu mnaanza kui-overate laana ... Hakuna upuuzi kama laana duniani.


Katika maisha yako hakikisha Chanzo Cha furaha ni wewe ... Toa na saidia pale mkono wako unapoishia... Kama huna jifunze kusema huna na kuwa tayari kupokea Maneno ya shombo kwa majibu yako ila kumbuka Chanzo Cha furaha ni wewe ( kiwe ndani yako ).... Hi tabia ya kufanya vitu kufurahisha watu ili watusifie tufurahi inatuharibia Sana vijana ... Kama huna sema huna ...Kama huna na unajua utapata mwambie utampa baada ya siku au wiki kadhaa ... Kama huna na hutaweza kutoa sema hunaaaaaaaa....


Wewe ndio unamlea na umesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha hiyo tabia ya Bi Mkubwa.



Unamfahau Mchezaji wa Zamani wa Arsenal , Emmanuel Adebayo ??? ... Alikuwa mstari wa mbele kusaidia familia Yale lakini ndio wakawa wa kwanza kumzunguka na kutokuwa na shukrani akiwemo mama Yale... Nakuwekea barua liyoandika kipindi Yuko Madrid ...
IMG_20200105_204907.jpeg
IMG_20200105_204940.jpeg
IMG_20200105_205003.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naam

Huu uzi unaweza kufungwa sasa.
Kama Laana zingekua za kweli na zinamfikia mtu basi leo hii mimi ningekua naokota makopo njiani,nazurura nadondosha mate naongea mwenyewe njia nzima.

Mama yangu alishanitamkia maneno magumu na mfano wa 1 ambalo nalikumbuka mpaka na kesho aliniambiaga "wewe najuta hata kukuzaa ,natamani ile siku nakuzaa ningebana miguuu ufe kabisa"

asee mimi hamna laana sijatamkiwa na mama,ila nikwambie kitu mamilooo "kaza buti songa mbele" huyo si mama ako sasa huyo ni shetani anaemtumia mama.

Nakwambia hivyo kwa sababu yule mama angu aliyenilaani mimi,na mimi nilimwambiaga MUNGU kuanzia leo MUNGU nakwambia kwa mdomo wangu kuwa SINA MAMA nitajihesabu nina baba tu.

basi nili m cancel mama nikawa staki story zake wala kumsikia,Nilipambana nikasema siku 1 ataniona kwenye tv ama kunisikia kwenye radio ama kunisoma kwenye gazeti,kisha nika kaza zangu Mama yangu akawa MUNGU nikitaka kitu namwambia MUNGU nikitaka kudeka namdekea MUNGU yes ndio alikua mama yangu.

Baada ya miaka mi 5 siku 1 nipo ofisini natoka nafata gari nisepe zangu nilimuona mama yangu akinifata kwa Magoti akitokea getini akiingia huku analia unajua nilihisi ni movie ya kihindi au macho hayaoni,nilifikicha macho kuangalia vizuri yes ni Mama controla.

anakuja kwa magoti analia kwa uchungu "nisamehe mwanangu" hakua anatamka neno jingine zaidi ya "nisamehe mwanangu" asee unajua ile kum miss mama muda hujamuona then mnakuja onana mama anakulilia umsamehe.

Mimi ni nani nisimsamehe mama asee ile siku tulijaza Raia pale nnje maanaa nililia kama mtoto mama alilia kama mtoto,ni mzee mmoja alikua kutubeba na kutupeleka ndani na kuanza kazi ya kutunyamazisha.

Mama yakaisha na hadi leo nilipofika asee zile laana zilikua kama KICK ya kunipitisha,pamoja na changamoto zote ila nakwambia Sina siku nililala njaa,sina siku nilikosa nguo,sina siku nilikosa sadaka kanisani,Mungu alikua MAMA kwangu.

Huyo mama yako si yeye nakwambia tena si yeye mtambue shetani na hila zake kisha mwambie hakuwezi nakuhakikishia usiponasuka kwenye huo mtego wa MAMA umepotea. Kunja sura kaza mwendo songa mbele mwambie live mama "siwezi" mwambie "sina" mwambie "nipo vibaya" Akikulaani tu, KATA Mawasiliano nae.

Saa zingine kuwalinda watu tunaowapenda zaidi ni kukaa mbali nao.

Mama yupo tu hafi leo wala kesho so usimuendekeze hata kidogo,kaza buti asikuyumbishe hata kidogo atabaki kuwa mama na milele utamuheshimu ila ktk swala la yeye kukurudisha nyuma "USIKUBALI" kataa kwa maneno na vitendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikikumbuka nlivokua naenda shulen form1 mpaka form four Kila siku wazaz wangu walinipa her ya chai mia3 na nauli mia4 kwa miaka mi4
Nilipoanza chuo walinipa 1000 Kila siku kwa miaka mi3
Sikumoja natoka mishemishe zangu....zakuhangaika
Mama ananiita sebuleni akanambia mwanangu jiandae j5 interview. nauliza wapi naambiwa Ni.............
MUNGU mwema nkaenda nkafanya nkapata!
Money ikiingia tu...hua nakumbuka wao kabla hata yangu mwenyewe
Nimesoma maelezo yako Hadi moyo umeniuma....nakumbuka navyokulaga blessings za msua na maza
MUNGU awabariki Sana wazazi wangu!
#mungu akutie moyo ndugu yangu

kelphin kepph
 
Back
Top Bottom