Tunaotegemea kugombea ubunge 2025 njooni tuweke mikakati yetu hapa binafsi nagombea jimbo la Mbozi

Shikiria hapohapo usiogope kugombea ni haki ya kila mtanzania. Vijana amkeni amkeni.
 
Mimi kiukweli nachohitaji ni kuwatumikia wananchi wa jimbo la Mbozi. Kuwaletea mabadiliko ya kweli.
Ningekuwa mimi ndio nawapitisha, ningepitisha hili azimio; uza vitu vyako vyote unavyomiliki na uwagawie wapiga kura wako wote ili wajikomboe na umasikini; kisha ndio uchukue fomu ya kugombea.
 
Tukagombee ndugu zangu. Tuhakikishe tunauhisha kadi zetu na uanachama wetu, yawezekana tukashika nyadhifa hasa sisi jobless. Serikali imetisahau baadhi yetu, bora kwenda kua active kwenye siasa,kuliko kubaki tukisubiria huruma za wanasiasa ambao wengi wao ni waongo tu.

Fikiria hatuna mitaji ya maana,tunajitafuta hatujipati, wanatupiga kalenda tu kua 'serikali ya mama Samia Suluhu Hassan imetoa kibali cha kuajiri watu elfu 23', uongo mtupu, toka mwakajana wanarudia kusema hivyo. Twendeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…