Tunapambana lakini tunaishia kupata pesa za kodi na kula tu

Tunapambana lakini tunaishia kupata pesa za kodi na kula tu

Umeongea kwa uchungu sana mkuu.
Ni kweli kupambana tunapambana lakini tunaishia kupata pesa ya kodi na kula tu.hakuna maendeleo yeyote tunafanya.hatukui.hatusogei tupo pale pale.majukumu yanaongezeka tunashindwa kusaidia familia.tunaonekana tunafanya kazi lakini kipato hakitoshi kutatua hata chabgamoto ndogo za familia.tunadhalilika sana.Mungu atusaidie sana
 
ni
Si bora hata wewe unapata hata hela ya kodi na kula ...

Kuna mwamba juzi katupiwa vyombo nje ...

Hela ya kodi haipatikani hela ya kula nayo haipatikani
Ni kweli mkuu,na ndo kitu ambacho kinanipa subra nikiwawaza wengine ambao nimehitimu nao chuo tangu 2021 hadi leo hawajapata kazi yeyote ya kufanya.
wengine tumebahatika kupata kazi lakini kazi zenyewe ni mtihani tu mishahara midogo majukumu mengi,mzazi anakuangalia wadogo zako bado familia yako bado ndugu wa karibu waliokushika mkono.Mungu atusaidie sana tunaishi kwa mawazo sana
 
Ndio maisha ya mjini mkuu, mtu akijenga nyumba na akipata usafiri. Sisi kama ndugu lazma tuwe tunapita pita kupata unafuu

Ila nilichojua mkuu, kuna mtu anafanya kile kile unachokifanya na anapata hizo pesa unazoota. Tofauti tu ni watu waliokuzunguka, kama wote ni hohehahe na mnaongelea 50k, jaribu ujipenyeze kwa watu wanaoongelea 10 million ili upate deals za thamani hiyohiyo.

Hata machawa wa wanasiasa na wasanii usidhani wanapenda, ni kujiweka katika hizo circle kwa namna ambayo hatuielewi
 
Mkuu mfumo wa MAISHA umeandaliwa hivyo kuishi kwa ajili kupata end meet , kwahiyo either upambane na mfumo au ukae ndani ya mfumo.
Screenshot_20250406-212757_1743998348556.jpg
 
Mwanangu ishu ni kuloga tuu maana hata mimi juzi nilojiuliza hvi watu wanapataje pesa za kujenga..

Watu wanapataje pesa za kununua magari nikaja gundua kuna kuloga pia kuna bahati ila kingine kwa mwanaume ili ufanikiwe lazima uwe huna nguvu za kiume.. simanishi shoga hapana maana kuna watu wajinga humu watajua namanisha ushoga laaa...

Lazima uwe hauna nguvu za kutia tia mara kwa mara....
 
Umeongea kwa uchungu sana mkuu.
Ni kweli kupambana tunapambana lakini tunaishia kupata pesa ya kodi na kula tu.hakuna maendeleo yeyote tunafanya.hatukui.hatusogei tupo pale pale.majukumu yanaongezeka tunashindwa kusaidia familia.tunaonekana tunafanya kazi lakini kipato hakitoshi kutatua hata chabgamoto ndogo za familia.tunadhalilika sana.Mungu atusaidie sana
Hiyo hali ilinikuta miaka 20 iliyopita nikafanya maamuzi magumu nikapiga chini kazi ya kuajiliwa nikaingia kitaa nikapata msoto miaka 5 baada ya hapo nimeajili watu kibao. Na mimi wembe uleule nawalipa mshahara wa kuwasogeza siku 10. Siku nyingine 20 ni mwendo wa kukopa, kutembea kwa mguu daadeki! Ubaya ubwela!
 
Back
Top Bottom