Tunapambana lakini tunaishia kupata pesa za kodi na kula tu

Tunapambana lakini tunaishia kupata pesa za kodi na kula tu

Hiyo hali ilinikuta miaka 20 iliyopita nikafanya maamuzi magumu nikapiga chini kazi ya kuajiliwa nikaingia kitaa nikapata msoto miaka 5 baada ya hapo nimeajili watu kibao. Na mimi wembe uleule nawalipa mshahara wa kuwasogeza siku 10. Siku nyingine 20 ni mwendo wa kukopa, kutembea kwa mguu daadeki! Ubaya ubwela!
Kuacha kazi mkuu inaitaji ujasiri mkubwa sana,na ujasiri tunao. lakini tunawawaza walionyuma yetu itakuaje,kuna watu wanakula na kusoma kupitia sisi,icho icho kidogo tunachopata tunagawana nao.sasa ukifanya maamuzi ya kuacha kazi uingie mtaani upambane miaka 5,hawa watu wataishije?
 
Kuacha kazi mkuu inaitaji ujasiri mkubwa sana,na ujasiri tunao. lakini tunawawaza walionyuma yetu itakuaje,kuna watu wanakula na kusoma kupitia sisi,icho icho kidogo tunachopata tunagawana nao.sasa ukifanya maamuzi ya kuacha kazi uingie mtaani upambane miaka 5,hawa watu wataishije?
Kuna msemo mmoja wa kizungu unasema "bora ufe ukiwa umesimama kuliko kuishi ukiwa umepiga magoti",
Ni bora kufa ukiwa huru na mwenye msimamo kuliko kuishi maisha ya unyonge, udhalili au utumwa.

Kwa ufupi, msemo huu unahimiza:

Kusimama kwa ajili ya haki na utu wako, hata kama ni hatari.

Kukataa kuishi kwa hofu au kunyenyekea kwa mabavu ya mtu au mfumo usio wa haki.

Ujasiri wa kupigania uhuru badala ya kuishi maisha ya aibu au ya kunyanyaswa.

Ni msemo unaotumika sana kwenye harakati za haki za binadamu, mapambano ya kisiasa, na hata maisha binafsi ya mtu anapokataa kudhalilishwa.
 
tupo wengi aisee tena Bora ninyi ambao mmebahatika kusoma, sisi wengine tuliishia darasa la 7 tukaamua kuingia kitaa kwasababu maisha magumu kupata experience mapema.

lakini mambo si rahisi kama tulivyo fikilia
unajitahidi mungu anasaidia unamiliki kigoli lakini mambo yanakua mengi muda mchache, Kuna wazazi, ndugu wanakutegemea inakua ni patashika.

unaajitahidi basi uongeze kipato unaamua kuvuta vijana wenzako ili msaidiane maisha ili angalau upige hatua lakini vijana nao wizi na uvivu vinakua nivikwazo vya kupiga hatua.

yaani kuna muda natamani kukufulu,
ushauri wangu kwako ulie na kazi au una kigoli na majukumu yamekua mengi usiache kazi au kuacha unacho kifanya, chamsingi jitahidi kuongeza mianya ili kuongeza kipato hatakama tunapitia changamoto
 
Sisi tunaoishi kwa mama zetu wadogo tuna raha sana sichangii chochote na kabla ramadhani ananiolea mke
 
Hayo mapambano yanakutengenezea msingi bora wa kesho.! Msikate tamaa.. Kesho yenu ni kubwa kuliko leo
Bado tuna imani na kuamini hii kauli,lakini kuna muda yanatushinda tunabaki na sonona mioyoni mwetu.Mungu atusaidie
 
Back
Top Bottom