Tunaposema Diamond ni mnyonyaji muwe mnaelewa. Inasemekana kipindi cha Bartender kimepigwa ''stop''

Tunaposema Diamond ni mnyonyaji muwe mnaelewa. Inasemekana kipindi cha Bartender kimepigwa ''stop''

Yani umeenda kukopy mawazo na maelezo ya mtu katika mada ukaja paste hapa mpe credit mkuu sio vzr ufanyavyo


Sent from my iPhone using JamiiForums
Mi uwa natoa Credit hila hii nimetoa kwenye interview ya muhuusika, na Baghdad mwenyewe nimemtaja katajwa sana hapo kwenye mada..

Kwamba Sky sports wakiwai kupost habari ya Pepe waliyoitoa kwenye page yake, BT sports Wakija kuipost baadae unataka wampe sky sports Credit?
 
Msanii Baghdad aliwahi kusema kuwa wazo la kipindi cha The Bartender lilikuwa ni lake na mwanzo wazo lilikuwa TheCounter au The Bartender na alilisajili COSOTA na kubaki na hatimiliki yake. Alishangaa kuona kipindi kinatangazwa wakati makubaliano hayakuwa yametimizwa na kukubaliana. Baghdad anasema kuwa makubaliano yalikuwa ni apate 13% ya mapato yatokanayo na show na idea zote ambazo ataziweka pale Wasafi kuliko kuajiriwa, yaani awe na life-time contract na Wasafi Media.

Baghdad anaendelea kusema kuwa wakiwa katika mchakato wa kusaini mkataba ambao ilionekana kuwa 13% ni kubwa na ishuke hadi 5% ghafla akashangaa kuona promo ya The Bartender, anasema aliamua kuwasiliana na Diamond, cha ajabu Diamond hakuwahi kupokea simu wala kujibu meseji zake. Anasema ilimstua na kuamua kumtafuta Babu Tale, Tale alimsihi sana Baghdad kuwa mtulivu wakati anaongea na Diamond juu ya hili. Alimsihi pia kutofanya chochote mathalani interview popote. Baada ya siku kadhaa Tale na Baghdad walichekiana na kumchana kuwa Diamond kasema fanya chocote unachoweza.

Baghdad aliamua kwenda COSOTA kutafuta haki yake kwa maana hata wazo la Jogoo ni miongoni mwa madini aliyoyatoa Wasafi. Anazidi kusema kuwa, COSOTA waliwaita ili kuwasuruhisha japo Diamond alikuwa akituma wawakilishi, mazungumzo yalifanyika kwa siku kadhaa bila mafanikio na Baghdad kuamua kwenda Mahakamani ili tu haki yake ipatikane.

Kwakeli huu ni utapeli wa kuaminika. Jamaa hawana ubunifu wowote ni wazee wa Kucopy na ku-paste. Walimsema sana Ruge hawa; sasa yule mtoto aliyekua analialia kuonewa kawa mtoto mbaya.
Kuiga iga sana. Inakera, kwani hamko wabunifu?

Kwa nini cha kiswahili kisiwe na jina tangulizi la kiswahili?

Kwanini WASAFI Fm Msije na mipango yenu, viwango vyenu na utamaduni wenu?

Watangazaji wote mliowachukua hawana jipya, zaidi ya kubadili mawimbi ya sauti zao (kutoka frequency ya awali mpaka ya sasa).

Pikeni watu wenu, waje na vitu vipya nasi tuzungumze kuhusu wasafi.

Mnakera kwa kukumbatia uzamani.

Hivi hata mna menejimenti ya watu makini kweli? (Makini: sifa na ujuzi).

Tunawapenda, ila boresheni huduma zenh kuanzia namna mnadahili wafanyakazi, maslahi yao, na ubunifu wako katika kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bartender ni kipindi ambacho hata marekani kipo?

Hati miliki kwenye kuiga?
Mimi huwa na shangaa sana. Hizi idea 99% tunatoa kwenye mtandao na Dstv leo mtu anakuja analia lia... So diamond anaweza kuamua kubadili jina la kipindi akaliita the pub..... Wewe utamzinguaje hapo.... Na ukileta za kuleta si anaenda na yeye kusema idea ameitafuta dstv.

So mambo mengine ni kumalizana kiutu uzima na sio kishari na stress

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We ni jinsia gani mkuu au ndo Juma lokole. Inakuuma sana huyo mzazi mwenzenu mnataka aongelewe kwa mazuri tu wakati kuna mabaya kibao anafanya..

Usinipangie cha kupost wala usinipangie mda wa kupost,. Wewe andika mazuri ya huyo mzazi mwenzako, mi ntaandika ambayo nyie hamwezi kuyaandika kisa ushabiki maandazi, Imekuuma utapeli wake kuwekwa wazi,.

Nyie ndo wale hata jamaa akipost sink la choo Mnaenda kukoment viemoj vya moto huku mkibana pua Chibu akee, simbaa akee, hizo pigo peleka huko hapa tunaongea mambo ya kiume, Utapeli haukubaliki
Eti sink la choo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi uwa natoa Credit hila hii nimetoa kwenye interview ya muhuusika, na Baghdad mwenyewe nimemtaja katajwa sana hapo kwenye mada..

Kwamba Sky sports wakiwai kupost habari ya Pepe waliyoitoa kwenye page yake, BT sports Wakija kuipost baadae unataka wampe sky sports Credit?
Toka hapa.... umecopy thread moja twitter ukaileta hapa au tuilete kama unabisha?

we mwenyewe mwizi wa idea, yaani unashupalia ya wenzako wakati you are doing the same thing, jinga kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Write your reply...KING KIBA PIA WALIMUIBIA VIPINDI VYAKE KWENYE KIBA TV SEMA TU AKAAMUA AZIME MITAMBO AKAIFANYA IWE INAPATIKANA KWAKE TU AKAINDOA KABISA DSTV


DOMO AJIFUNZE KWA KIBA .KIBA HAPENDAGI SHOW OFF
 
Write your reply...KING KIBA PIA WALIMUIBIA VIPINDI VYAKE KWENYE KIBA TV SEMA TU AKAAMUA AZIME MITAMBO AKAIFANYA IWE INAPATIKANA KWAKE TU AKAINDOA KABISA DSTV


DOMO AJIFUNZE KWA KIBA .KIBA HAPENDAGI SHOW OFF
 
watu wanasema wasafi wanacopy na kupaste na waache kuchukua watangazaji wa vituo vinginevyo,
huo ni wivu tu na dalili ya kushindwa kushindana na wasafi kununua watangazaji

Hivi wao hao clouds walitengeneza hao watangazaji wao,watangazaji Kama
# Musa Hussein, mamy baby, Kennedy the remedy,adam mchovu,George Bantu,millard ayo,mina ally,dj sinyorita,dj muba, kina Jeff Lea,fredwaa,
list ni ndefu sana Je hao si wote wamenunuliwa au hamuoni kule ni wasafi tu?
 
E-fm walionunuliwa
Gerard hando,maestro,jabir,gea habibu wa uhondo, Musa kipanya,oscar Oscar, ssebo,mtiga abdallah,jonijoo,dokii,Tunu,seba wa lala by,

sasa sioni Kama kuna redio iliyotengeneza hapo wote hao wengi wanatengenezwa sehemu zingine redio ndogo ndogo za mikoani.

E-fm wamewatengeneza kingwendu na Steve Nyerere basi.
 
Robidinyo,

Domo ni mwizi na kila mwenye akili timamu analiona hilo.

Kaiba na anaendeleakuiba nyimbo za watu.

Anakopi na kupaste kuanzia kweny Nyimbo, watangazaji mpaka vipindi vya media.

Aisee wazee shule MUhimuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

We shule yako imekusaidia nn!! mwenzio ana copy na ku paste na ana pesa mlima...
 
Tatizo la usafini ni ubunifu na ile tabia ya kukwapua watangazaji vituo tofauti wasio na mawazo bunifu, mfano Zembwela iv yule ana ubunifu upi aliiua Uswazi ya EATV baada ya Mussa Hussein kutoka. Maulid Kitenge naona alpoishia ndo hapo hana ubongo mpya wa kutanua ubunifu, Lil Ommy yuko vizuri ila naona kapwaya The Switch maana hajaja pale na ubunifu mpya. Pale watu wenye maono ni Ambangile na nahisi akimtumia vizuri anaweza leta impact kubwa, Aaliyah, na Edo Kumwembe ingawa yupo kimasilahi zaidi lakini akibadili mindset Edo ana akili kichwani.
Ambangile Ni yupi huyo unayemzungumzia?
 
Mi uwa natoa Credit hila hii nimetoa kwenye interview ya muhuusika, na Baghdad mwenyewe nimemtaja katajwa sana hapo kwenye mada..

Kwamba Sky sports wakiwai kupost habari ya Pepe waliyoitoa kwenye page yake, BT sports Wakija kuipost baadae unataka wampe sky sports Credit?

Kumtaja mtu kwenye mada sio kumpa credit aya maanishi umekopy umu jamii forum ni vyema ungeandika kua umekopy kutoka kwa mtu ukitaka nkuletee uzi hapa zaidi ya aya hakuna maneno yako apo ata moja mkuu zaidi ya kupaste tu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mi uwa natoa Credit hila hii nimetoa kwenye interview ya muhuusika, na Baghdad mwenyewe nimemtaja katajwa sana hapo kwenye mada..

Kwamba Sky sports wakiwai kupost habari ya Pepe waliyoitoa kwenye page yake, BT sports Wakija kuipost baadae unataka wampe sky sports Credit?

Weka clip ya iyo interview acha porojo na maneno ya kusadikika ukishindwa fanya ivyo izo ni porojo na uongo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom